Showing posts with label Injili. Show all posts
Showing posts with label Injili. Show all posts

Rose Mhando adaiwa kutapeli, Wananchi wakusanyika tamashani


MSANI maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini Rose Mhando ametuhuimiwa kutapeli zaidi ya milioni 3 pesa alizoziomba kwaajili ya tamasha la burudani ya injili kwa  wakazi wa mkoa wa Njombe ambalolilikuwa lifanyike jumapili iliyopita na kufunguliwa kesi ya madai polisi na waandaaji wa tamasha hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya msanii huyo kutoonekana katika tamasha la injili alilotakiwa kutumbwiza, Mkurugenzi wa The Comfort Gospel Promotion, Gerald Sedekia alisema kuwa Mhando alitakiwa kutumbwiza katika tamasha ambaloliliandaliwa kwaajili ya kuanzishwa pesa kwaajili ya mfuko wa kuchangia watoto yatima.

“Mnamo tarehe 24 may tuliwasiliana na mwimbaji wa nyimbo za injili Rose Mhando kwaajili ya kutumbwisa katika tamasha ambalo tungekusanya pesa kwaajili ya kuanzishwa mfuko wa watoto yatima Mkoani Njombe,” alisemsa Sedekia.
Alisema kuwa waliwasiliana nae na kukubaliana kwa shughuli hiyo ya tamasha alihitaji kupewa milioni tatu na kupewa pesa za awali shilingi milinoni moja na nusu ambazo na kuwa baada ya hapo aliomba pesa kidogo kidogo na kuwa akaamua kumpelekea mkataba.

Alisema kuwa walipo kutana mjiji Dodoma na kujaza mkataba alihitaji kupewa pesa zote ili wasiwe wanadaiana ana walimpa pesa zote za tamasha milioni tatu.

Alisema kuwa Rose rose siku ilipo wadaia ya kumtaka afike Mkoani Njombe hakupatikana na alipo patikana alipigiwa simu ilipoita ilikatwa.


“Mhando ilihitajika afike hapa Njombe mapema siku moja kabla ya siku ya Jumapili ili kuonekana kwaajili ya matangazo ya nje lakini tulipo mpigia siku alisema yupo njiani lakini mda ulivyo zidi kwenda hakupatikana, alipo patikana alisema gari inamsumbua lakini kufika jumapili ndo hakupatikana kabisa,” alisema Sedekia.

Alisema kuwa baada ya kuona mda umeenda sana waliamua kwenda polisi ili kumfungulia kesi na kuwa kuna watu waliwasiliana nao walisema yupo Dar Es Salaam anafanya kazi huko lakini baada ya muda hakuwepo.

“Kumbe Rose alikuwa anatafutwa na watu wengi tu sio sisi pekeyetu kwa sababu hata wakati tamashaletu linaendelea kunawatu wanne walikuja kumtafuta, kuto kuwapo kwake tumepata hasara kubwa ya zaidi ya milioni 6 na kutukanwa na watu na kutuona sisi ni matapeli,” aliongeza Sedekia.

Aliongeza kwa kusema kuwa watatoa fundisho kwa Rose Mhando kwa kumkamana na kufikisha mahakamani kwa kuwa wameshafungua kesi na watawaita waandishi w ahabari ili kufuta aibu waliyo ipata.

Ametoa wito kwa wasanii wa Injili ambao wamekuwa wakiaminiwa kuwa ni wafanyakazi wa Mungu lakini kwa picha aliyo onyesha msanii huyo haijapendeza.

Alisema kuwa katika mkataba wao ulikuwa unasema kuwa asipofika katika tamasha atatakiwa kuirudisha pesa za gharama na asilimia 10.

Aidha baada ya kumtafuta Mhado simu yake haikuweza kupokelewa na kila ilipo ita ilikatwa na baada ya kuida kwa muda mrefu na baadae kuzimwa kabisa.

Sedekia Gerald Kushoto na Rose Mhando Kulia siku walipo kutana kujaza mkataba

Vijana na Mapadre waonywa kuingia katika makundi ya watangaza nia


ASKOFU wa jimbo kuu la Songea Damian Dallu amewataka mapare nchini kote kuto jiweka katika makundi ya watangazania ambao wanaendelea kutangaza nia hapa nchini ili kuto kuwapo kwa mgawanyiko wa makundi na kusababisha mpasuko wa kitaifa.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa misa ya kufunga kongamano la vijana kitaifa lililofanyika Mkoani Njombe ambapo amewataka mapadre na vijana kutokujiingiza katika makundi ya watangaza nia ambao wanaendelea kutangaza nia hapa nchini.

Alisema kuwa endapo mapadre watajikita kwa makundi kwa mtangazania mmoja mmoja wata sababisha mpasuko atakapo teuliwa mmoja kugombea urais.

Askofu Dallu alisema kuwa pamoja na mapadre kuto kuwa na vyama alisema kuwa vijana nao wahakikishe wanaimalisha utaifa na sio kujikuta katika umoja wa vijana wa vyama vya siasa.

Alisema kuwa vyama vya siasa vipopo na wakiingia katika vyama hivyo wanaweza kuanza kupingana wao wenyewe cha msini ni kuungana katika umoja wa vijana wa taifa na sio wa vyama vya siasa.

“Vijana angalieni kuto kujikuta katika umoja wa vijana wa vyama vya siasa jiungeni na unganisheni taifa katika umoja wa vijana wa taifa na sio kujikita katika vyama vya sisasa,” Alisema Dallu.

Alisema kuwa Wakrel (Mabruda) wajishirikishe na siasa kwa asilimia ndogo sana na sio kujihusisha na siasa hadi kufikia hatua ya kuwa na watu wengi.

Aidha aliwataka vijana kuto jiingiza katika siasa ambayo inaweza kusababisha mgawanyiko wa taifa ambalo limetufikisha hapa.

Alisema vijana wawemakini na vijana na wanasiasa wanao taka kulivunja taifa na kuachana nao na kutoa taarifa kwa vyombo vinavyo husika ili kuepusha taifa kuingizwa katika machafuko.


WAZIRI MHE. BERNARD MEMBE ATOA RAI KWA VIONGOZI WA DINI ZOTE PAMOJA SERIKALI KUHIMIZA VIJANA WAIPENDE DINI ILI KUDUMISHA AMANI, UTULIVU NA UADILIFU

 Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ambaye alikuwa mgeni rasmi akiongea katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015. Pembeni ni Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama. PICHA ZOTE NA CATHBERT KAJUNA WA KAJUNASON BLOG.

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akiwapungia watu waliohudhuria katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe. Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka ililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia), Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki na Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na Mkewe.
Watu waliohudhuria Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akitoa vyeti vya shukrani kwa vyombo mbali mbali  vya habari vilivyoshiriki kwa miaka kumi na tano katika kulitangaza tamasha la Pasaka.
Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akishirikiana na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara (kulia) na Mchungaji Mwasota kukata keki. Aanayeshudia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki.

Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akimlisha keki Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama na mkewe.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akimlisha keki Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki. Pembeni anayeshuhudia ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Fenella Mukangara.

Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini anayefahamika kwa jina la Rebbeca Malope akitoa burudani katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.

Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini, Mchungaji Solly Mahlangu mwanamuziki nguli akiimba na kucheza  katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mwimaji Chritina Shusho akiimba katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015..
Mwimbaji Rose Mhando akiwasha moto wa kamata pindo la Yesu katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.

Wakiimba kwa pamoja...

Msanii wa Sarakasi akitoa burudani katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mwimbaji John Lissu na waimbaji wake wakiimba.
Mwimbaji wa Nyimbo za Injili, Joshua na vijana wake wakiimba.
Kwaya ya Kijitonyama wakiimba katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Kwaya ya Kijitonyama Upendo Group ikiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuimba katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Marafiki wakifurahia...
Mtangazaji wa Clouds Radio & TV, Samweli Sasali akiongea na waimbaji wa Kwaya ya Kijitonyama Upendo Group...
Taswira ikitafutwa...
Na Mwandishi Wetu, Dar.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe ametoa rai kwa viongozi wa dini zote pamoja serikali kuhimiza vijana waipende dini ili kudumisha amani, utulivu na uadilifu.
Mhe Membe amesema hayo wakati akihubutibi maelefu wa watu waliohudhuria Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly akisoma hotuba amempongeza Mhe Bernard Membe kwa kujumuika na Watanzania katika Tamasha la kumi na tano la Pasaka.
Katika Tamasha hilo la Pasaka, Kampuni ya Msama Promotions, ambao ndio waandaji wa Tamasha hilo, wamemtunuku Mhe. Rais Jakaya Kikwete kwa mchango wake katika kukuza tasnia ya Sanaa nchini.
Tuzo ya heshima ilitolewa kwa Rais Mstaafu, Mhe. Ali Hassan Mwinyi.
Mhe Bernard Membe alitunukiwa tuzo kwa mchango wake kwa shughuli za kijamii.
Tuzo zimetolewa kwa vyombo mbalimbali vya habari nchini kwa michango yao katika kutangaza Tamasha la Pasaka.
Viongozi wa Serikali waliohudhuria Tamasha hilo ni pamoja na Mhe. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Angela Kairuki, Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, naMhe. Paul Makonda, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Tamasha hilo lilihudhuriwa na viongozi wa kidini wakiwemo, Askofu David Mwasota wa Kanisa la Naioth Gospel Assembly na Mchungaji Mwasota.
Tamasha la Pasaka lilianzishwa rasmi mwaka 2000 na huwashirikisha Waimbaji wa Nyimbo za Injili kutoka nchini na nje ya nchi ambapo mwaka huu limewashirikisha waimbaji kutoka hapa nchini, Afrika Kusini, Uingereza na Zambia.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiwa na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angella Kairuki na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda wakifuatilia tamasha.
Mshehereshaji akiendesha Tamasha la kumi na tano la Pasaka, lililofanyika katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, Jumapili 5, 2015.
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Membe akiondoka pamoja na wageni wake mara baada ya kuhutubia.
Nikiripoti toka Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni Mimi Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog...
KANISA LA KISASA KUJENGWA MAKOLE DODOMA NI LA PENTECOSTAL HOLINESS

KANISA LA KISASA KUJENGWA MAKOLE DODOMA NI LA PENTECOSTAL HOLINESS

Kazi ya Ujenzi wa Kanisa jipya la Pentecostal Holiness Association mission Makole Dodoma inaendelea kwa awamu nyingine hatua tulio nayo sasa tumemwaga zege kwenye msingi kati ya nguzo na nguzo kazi hiyo imefanyika jana na wiki hii tutaanza kujenga tofali za msingi tunatakiwa kuwa na tofali zisizopungua 4500 lakini mpaka sasa tunazo tofali 1900 na mifuko ya cement inaitajika 30 mpaka sasa tunayo mifuko 10. Tuungane pamoja wenzetu mlio mbali nje ya Dodoma, Nje ya Tanzania, Nje ya Africa. Tujenge pamoja nyumba ya kuabudia. Mwampona Katibu wa Ujenzi.


Kategori

Kategori