MSANI maarufu wa nyimbo za injili hapa nchini Rose Mhando
ametuhuimiwa kutapeli zaidi ya milioni 3 pesa alizoziomba kwaajili ya tamasha
la burudani ya injili kwa wakazi wa mkoa
wa Njombe ambalolilikuwa lifanyike jumapili iliyopita na kufunguliwa kesi ya
madai polisi na waandaaji wa tamasha hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya msanii huyo
kutoonekana katika tamasha la injili alilotakiwa kutumbwiza, Mkurugenzi wa The
Comfort Gospel Promotion, Gerald Sedekia alisema kuwa Mhando alitakiwa
kutumbwiza katika tamasha ambaloliliandaliwa kwaajili ya kuanzishwa pesa
kwaajili ya mfuko wa kuchangia watoto yatima.
“Mnamo tarehe 24 may tuliwasiliana na mwimbaji wa nyimbo za
injili Rose Mhando kwaajili ya kutumbwisa katika tamasha ambalo tungekusanya
pesa kwaajili ya kuanzishwa mfuko wa watoto yatima Mkoani Njombe,” alisemsa
Sedekia.
Alisema kuwa waliwasiliana nae na kukubaliana kwa shughuli
hiyo ya tamasha alihitaji kupewa milioni tatu na kupewa pesa za awali shilingi
milinoni moja na nusu ambazo na kuwa baada ya hapo aliomba pesa kidogo kidogo
na kuwa akaamua kumpelekea mkataba.
Alisema kuwa walipo kutana mjiji Dodoma na kujaza mkataba
alihitaji kupewa pesa zote ili wasiwe wanadaiana ana walimpa pesa zote za
tamasha milioni tatu.
Alisema kuwa Rose rose siku ilipo wadaia ya kumtaka afike Mkoani
Njombe hakupatikana na alipo patikana alipigiwa simu ilipoita ilikatwa.
Alisema kuwa baada ya kuona mda umeenda sana waliamua kwenda
polisi ili kumfungulia kesi na kuwa kuna watu waliwasiliana nao walisema yupo
Dar Es Salaam anafanya kazi huko lakini baada ya muda hakuwepo.
“Kumbe Rose alikuwa anatafutwa na watu wengi tu sio sisi
pekeyetu kwa sababu hata wakati tamashaletu linaendelea kunawatu wanne walikuja
kumtafuta, kuto kuwapo kwake tumepata hasara kubwa ya zaidi ya milioni 6 na
kutukanwa na watu na kutuona sisi ni matapeli,” aliongeza Sedekia.
Aliongeza kwa kusema kuwa watatoa fundisho kwa Rose Mhando
kwa kumkamana na kufikisha mahakamani kwa kuwa wameshafungua kesi na watawaita
waandishi w ahabari ili kufuta aibu waliyo ipata.
Ametoa wito kwa wasanii wa Injili ambao wamekuwa wakiaminiwa
kuwa ni wafanyakazi wa Mungu lakini kwa picha aliyo onyesha msanii huyo haijapendeza.
Alisema kuwa katika mkataba wao ulikuwa unasema kuwa asipofika
katika tamasha atatakiwa kuirudisha pesa za gharama na asilimia 10.
Aidha baada ya kumtafuta Mhado simu yake haikuweza
kupokelewa na kila ilipo ita ilikatwa na baada ya kuida kwa muda mrefu na
baadae kuzimwa kabisa.
Sedekia Gerald Kushoto na Rose Mhando Kulia siku walipo kutana kujaza mkataba
|