Hopitali ijengewe uzio ili kuimarishwa ulinzi

HALMASHAURI ya mji Njombe imetenga zaidi ya milioni 100 kwa mapato ya ndani kwa lengo la kujenga Uzio ya hospitali ya Kibena ambayo kuto kuwapo kwa Uzio kunasababisha kelo kwa wagonjwa wanaopata huduma.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kubainikuwa kuna ulinzi hafifu katika hospitali hiyo ya halmashauri ya mji Njombe ya Kibena kutokana na kuto kuwapo kwa uzio mwenyekiti wa halmashauri hiyo Edwin Mwanzinga alisema kuwa halmashauri imeliona tatizo hilo na kutenga fedha kwaajili ya kujenga uzio.

Alisema tatizo hilo sio la leo waja jana ni tatazo la miaka mingi tangu kuwapo kwa hospitali hiyo licha ya miaka ya nyuma Maendeleo ya ujenzi wa makazi ya watu haukuwepo na kulikuwa na msitu ulikuwa kama uzio.

“Unajua tatuzo la uzio katika hospitali ya Kibena halijaanza leo lilikuwepo toka mika ya nyuma lakini sasa linaonekana ni tatizo kubwa kutokana na mazingira kubadilika makazi ya watu yamesogea hadi hospitalini na watu wanafuga mbwa na wanyama wengine watakatisha hovyo hovyo hospitalini,” alsema Mwanzinga.

Alisema halmashauri imetenga shilingi milioni 130 mapato ya ndani kwaajili ya kuanza ujenzo wa uzio katika hospitali hiyo na kuwa ujenzi utaanza kwa upande wa nyuma ya hospitali hiyo.

Mwanzinga alisema hospitali hiyo kutokanana kuwapo kwa wanyama wanao katisha hospitalini hapo watajenga uzio kwaajili ya kuwadhibiti na kuimarisha ulinzi kwa wagonjwa wanao pata huduma na hata Kudhibiti wagonywa wanao weza kutoroka.

Aidha baadhi ya wadau wameitupia lawama halmashauri hiyo kwa kutojenga Uzio kwa mda mrefu sasa tangu kuanzishwa kwake na kusababisha wagonjwa kuwa hatalini kuvamiwa na wezi, majambazi na hata vibaka.

Alatanga Nyagawa ni mmoja wa wadao ambao wamekuwa wakilipigia kelele suala hilo na kuwa kuna siku aliingia hospitalini hapo na mgonywa usiku na kuingiza kila kona bila kuulizwa na mtu yeyote.

Alisema kuwa; “Siku moja niliingia hospitalini nilizuguka kila kona na hakuna aliye niuliza nilipo fika katika shumba cha kuhifadhia maiti nikakutana na pabu wa miaka zaidi ya 70 akiwa na kisongo (Kirungu) amejikunyata kutokana na baridi namuuliza babu vipi ananiambia ni mlinzi nilishangaa kuona hospitali kubwa ya halmashauri kulingwa na kikonge na huku hata uzio hakuna, kunahaja ya halmashauli kushugulikia suala hilo,” alisema Nyagawa.

Alisema kuwa halmashauri inawajibu wa kuchukua hatua za haraka kuhusiana na ujenzi wa uzio hatakama itajengwa wa Nyavu kwanza ili kumimalisha ulinzi hospitalini hapo ambapo malaika (watoto wadogo) wanazaliwa.