Showing posts with label 2017 at 12:39PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:39PM. Show all posts
Kamanda Sirro Aapishwa Rasmi Kuwa IGP Mpya

Kamanda Sirro Aapishwa Rasmi Kuwa IGP Mpya

Rais John Magufuli amemuapisha mkuu mpya wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro aliyeteuliwa jana kuchukua nafasi ya Ernest Mangu.
Hafla hiyo imehudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Waziri wa Mambo ya Ndani , Mwigulu Nchemba na makamishna mbalimbali wa jeshi hilo.
Sirro baada ya kuapishwa amekula kiapo cha maadili mbele ya Rais Magufuli kwa ajili ya kutekeleza majukumu yake mapya.

from Blogger http://ift.tt/2rNzPCD
via IFTTT


Picha: Mji huu Jimbo la Oregon Marekani unauzwa TZS 8 bilioni

Picha: Mji huu Jimbo la Oregon Marekani unauzwa TZS 8 bilioni

Mji wote wa Tiller, katika jimbo la Oregon nchini Marekani unauzwa, bei yake ikiwa $3.8 milioni (TZS 8,439,040,000).
Mji huo unapatikana eneo ambalo halina watu wengi ambalo lipo umbali wa kilomita 362 kusini mwa mji wa Portland.
Miongoni mwa vitu vinavyouzwa, kuna nyumba sita, jumba moja lenye vyumba vingi vya makazi, kituo cha petroli na duka moja.
Wakazi takriban 250 huishi maeneo yaliyo karibu na mji huo.
Wakazi walianza kuuhama mji huo baada ya kudorora kwa biashara ya mbao na kufungwa kwa kiwanda cha kupasulia mbao.
Mji wa Tiller ulianza kuuzwa mara ya kwanza mwaka 2015 shule ya msingi ya zamani haikuwa imejumuishwa miongoni mwa vilivyokuwa vinauzwa.
Ni wakazi wawili pekee ambao kwa sasa bado wanaishi katika mji wa Tiller wenyewe. Wakazi hao ni mwalimu wa zamani ambaye anaishi karibu na shule iliyokuwa ikitumiwa zamani, pamoja na mhubiri wa kanisa moja.
Vipande vyao vya ardhi haviuzwi.Mji wa Tiller umezingirwa na milima na msituMaporomoko ya maji ya South Umpqua yanapatikana karibu na mji wa TillerNyumba moja mjini TillerDuka kuu mjini Tiller bila linauzwa, lakini linauzwa kandoWapenzi wa filamu ya Walking Dead wanaweza kupendezwa na duka hiliShule hii ya msingi ya zamani pia inauzwa, pamoja na paa anayeishi humoChumba cha kufanyia mazoezi ya viungo shuleni humo
Mbona mtu atake kuishi humo?
“Pesa kutoka kwa serikali kuu za kutumiwa katika biashara ya kupasua mbao zilipoanza kupungua, kiwanda kilifungwa,” anasema Garrett Zoller, mmiliki wa shirika la Land and Wildlife.
“Na kiwanda kilipofungwa, wengi wa wapasuaji mbao walianza kuondoka.”
Familia inayomiliki mji wa Tiller kwa sasa ilinunua mji huo kipande kwa kipande familia nyingine zilipoendelea kuhama.
Miongoni mwa walioonesha nia ya kutaka kununua mji huo ni wawekezaji kutoka China, pamoja na watu wanaotaka kuanzisha taasisi za matibabu au kukuza miti.

from Blogger http://tztown.blogspot.com/2017/03/picha-mji-huu-jimbo-la-oregon-marekani.html
via IFTTT


Mtuhumiwa ajiua akiwa Mahabusu ya Polisi

Mtuhumiwa anayedaiwa kupatikana na meno ya tembo yenye thamani ya Shilingi milioni 500, Daudi Matola (41) mkazi wa Wilaya ya Namtumbo amekutwa amekufa akiwa mahabusu mjini Songea.
Anadaiwa kujinyonga hadi kufa kwa kutumia suruali aliyoifunga kwenye dirisha la choo cha mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Songea.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji amesema tukio hilo lilitokea Machi 9 saa 9:55 usiku.
Mwombeji amesema inadaiwa siku ya tukio Matola akiwa mahabusu alienda chooni ambako alijinyonga kwa kutumia suruali yake.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://ift.tt/2ms2574
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


from Blogger http://ift.tt/2n2pMH4
via IFTTT


Kategori

Kategori