Showing posts with label 2017 at 06:15PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 06:15PM. Show all posts
Zitto Kuzibwa Mdomo na Serikali…..Wanaokihushisha ACT Wazalendo na CCM Wamefeli

Zitto Kuzibwa Mdomo na Serikali…..Wanaokihushisha ACT Wazalendo na CCM Wamefeli

CHAMA Cha Act-Wazalendo Mkoa wa Kagera kimesema kuwa wanasiasa wanaolitumia jina la chama na Kiongozi wa Chama hicho Zitto Kabwe kwa ajenda za Propaganda mbaya wamefeli.
Propaganda hizo ni pamoja na kukihusiha chama hicho na Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja kumtaja na kiongozi kuwa atapewa nafasi kubwa kwenye Serikali ili kukiua chama hicho.
Hayo yamelezwa na Katibu wa Vijana wa Chama hicho Mkoa huo Khalfani Fadhili kupitia ukurasa wake wa mtandao wa picha wa Instergram (@ khalfani_fadhili) ambapo amesema kuwa Chama hicho hakitarudi nyuma na kwamba hawatayumbishwa na Propaganda za wanasiasa wenye nia ovu na chama hicho.
Amesema kuwa baadhi ya kauli za wanasiasa kuwa Zitto Kabwe atafungwa na Mdomo kwa kupewa nafasi ndani ya Serikali kuwa sio za kweli na hazina afya kwenye siasa nchini.
“Zitto sio mmiliki wa ACT wazalendo bali ni mwanachama wa ACT na ni mbunge mwenye dhamana ya chama pia ni kiongozi mkuu katika chama.Hivyo ukikuta mwanasiasa mwenye nia ovu kwa kauli zao za kuwaaminisha watu kuwa Zitto yuko mbioni kupewa Uwaziri ili Act-Wazalendo ife jua huyo ni mwanasiasa aliyefilisika”Amesema kuwa wapo wanaowamisha watu kuwa Act-Wazalendo ni sehemu ya CCM ilhali chama cha Act kina sera za kulijenga taifa , ujamaa na uzalendo kwa kushirikiana na watanzania wote bila kujali itikadi zao.
“Sikatai kuwa haiwezi kuwa akapewa nafasi nyeti katika serikali hii inayoonyesha kuguswa na viongozi wa ACT.bali nakataa wale wanaolazimisha watu waamini kuwa ACT ni sehemu ya CCM.Yanaongelewa mengi kuwa Mh.Zitto atafungwa mdomo kwa kupewa nafasi ya juu ili anyamaze.hayo ni maneno ya chuki dhidi ya chama chetu kwani hata wao wanazitamani nafasi tulizozipata ACT katika kuilitumikia taifa hili.”

from Blogger http://ift.tt/2sAZHle
via IFTTT


Magufuli Amtaja Mbunge wa CCM Aliyejaribu Kufanya Njama za Kuizuia Kamati ya Pili Isiwalisishe Ripoti Yake

Magufuli Amtaja Mbunge wa CCM Aliyejaribu Kufanya Njama za Kuizuia Kamati ya Pili Isiwalisishe Ripoti Yake

Rais John Pombe Magufuli (JPM) amesema aliyekuwa Kamishna wa Madini, Dk Dalaly Kafumu alikwenda kujaribu kufanya ujanja ili ripoti ya pili ya mchanga wa madini ibadilishwe lakini hakuweza.
Kafumu kwa sasa ni Mbunge wa Igunga(CCM) ambaye alijiuzulu kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini mapema mwaka huu.
Rais Magufuli, ameyasema hayo leo Jumatatu wakati akipokea ripoti ya pili ya mchanga wa madini Ikulu na kueleza kuwa ameyasoma na kuyakubali mapendekezo yote yaliyotolewa na kamati hiyo.
“Ninawashukuru viongozi wa vyama mbalimbali ambao mmetoa ushirikiano katika hili, hizi fedha ni nyingi sana na zikienda hospitali zinawatibu wote,” amesema.
“ Haya madini hayana vyama.” Aliongeza.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sU8OeA
via IFTTT


Aliyeunguzwa na Mumewe Amshukuru Rais Magufuli..!!!

RAIS Dk. John Magufuli, amepongezwa kwa moyo wake wa kujitoa na kuwajali wanyonge hasa wagonjwa wasiojiweza na wenye mahitaji ya gharama za matibabu.
Neema Wambura, maarufu kama ‘Mgonjwa wa Magufuli’ alisema hayo jana alipotembelewa na waandishi wa habari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alilazwa kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada ya kupata majeraha ya moto.
“Ninamshukuru sana Rais Magufuli kwa msaada wake katika matibabu yangu. Hivi sasa nina maendeleo makubwa, naweza kuzungumza, kula na hata kugeuza shingo yangu.
Nitamwombea Rais Magufuli mpaka siku naingia kaburini, Mungu ambariki,” alisema.
Akisimulia mkasa uliompata, Neema alisema alimwagiwa maji ya moto na mumewe baada ya kuchuma mahindi mawili shambani bila ya ruhusa yake.
Mumewe huyo alitoweka na ndugu zake walihofia kumchukua kwa kuogopa kudaiwa mahali iliyolipwa na mumewe kama taratibu za kumuoa.
“Hakuna ndugu yangu hata mmoja aliyejitokeza kunisaidia kipindi chote cha matibabu.
Walihofia kama ningefariki dunia ingempasa huyo ndugu kurudisha mahali ambayo mume wangu alitoa. Nilikuwa nasaidiwa na majirani tu, nilikata tamaa ya kuishi na nilikuwa nasubiri siku yangu ya kufa ifike,” alisema.
Neema pia aliwashukuru watumishi wa Muhimbili wodi ya Mwaisela wakiwamo wauguzi na madaktari kwa upendo na msaada mkubwa waliompatia tangu siku walimpokea mpaka sasa wakati anatarajia kurudi nyumbani.
Akielezea maendeleo ya afya ya Neema, Mkurugenzi wa Upasuaji wa MNH ambaye pia ni Daktari bingwa wa upasuaji, Dk. Ibrahimu Mkoma, alisema mgonjwa huyo alipokewa hospitalini hapo Julai 6, 2015 akitokea Musoma mkoa wa mara huku akiwa na majeraha ya mwaka mmoja toka aunguzwe.
Alisema mpaka sasa ameshafanyiwa oparesheni tatu kwa nyakati tofauti, zilizohusisha kutenganisha baadhi ya viungo kwa kuwa shingo, kifua na mkono wa kushoto vilishikana.
Pia alisema ilibidi kutoa ngozi ya sehemu ya mwili ili kufunika sehemu zile zilizoathirika zaidi.
“Ni katika kipindi hicho cha matibabu, Rais alimwona Neema na kuguswa na hali yake na kuamua kumsaidia mpaka hivi sasa mnavyomwona. Neema sasa amepona na ataweza kuihudumia familia yake vizuri,” aliongeza Dk. Mkoma.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2nvpxlS
via IFTTT


Kategori

Kategori