Showing posts with label Misaada. Show all posts
Showing posts with label Misaada. Show all posts

MISS TANZANIA WATOA MSAADA HOSPITALI YA KILEMA NA MARANGU MOSHI

  

Washiriki wa Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 walitoa misaada ya kijamii katika Hospitali za Misheni Kilema na ile ya K.K.K.T Marangu baada ya kutembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro.


 Mwakilishi wa Kanda ya Ziwa katika Shindano la Redds Miss Tanzania 2014 Dorine Robert akimpa zawadi ya chandarua mgonjwa Jamila Msafiri aliyelazwa katika Hospitali ya Kilema Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro jana ambapo warembo 30 wa Miss Tanzania walitoa msaaada mbalimbali ya kijamii hospitalini hapo.
 Warembo waiangalia watoto

 picha ya pamoja ya warembo na wenyeji Hospitali ya Kilema Moshi.
 Hapa ni Hospitali ya KKKT Marangu.
 Mpigapicha wa True Vision John Lymo akiwajibika kwa kuakama taswira za warembo.






Baada ya hapo warembo na viongozi walishirikki chakula cha mchana nyumbani kwa Naibu Kamanda wa UVCCM Moshi Vijijini, Innocent Shirima Melleck.

Misaada yaanza kuwafikia waathiriwa Ufilipino

Misaada ya dharura iliyokuwa imesubiriwa kwa hamu imeanza kupelekwa katika eneo lililoathirika zaidi na kimbunga Haiyan nchini Ufilipino  na kuwafikia waathiriwa ambao wamekuwa wakiteseka kwa wiki sasa. Umoja wa Mataifa umekadiria kuwa watu waliowachwa bila makaazi imefikia takriban milioni mbili. 
Juhudi hizo za kusambaza misaada bado zimevurugika huku maafisa wakisema manusura wa kimbunga hicho wanaendelea kuhangaika na kusubiri chakula na maji . 
Ikiwa ni zaidi ya wiki moja baada ya Kimbunga Haiyan kuwauwa watu 3,633, mamia ya wafanyakazi wa kimataifa wa misaada wameweka hospitali za muda na kupeleka misaada. Mataifa kadhaa yakiongozwa na Marekani yanaendelea kuwasilisha misaada yao kwa wahanga wa janga hilo.

Kategori

Kategori