Showing posts with label 2017 at 12:33PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:33PM. Show all posts
Hatarii..Ridhiwani Kikwete Atoa Povu kwa Serikali Juu ya Kukaa Kimya Sakata la Watu Kutekwa na Kupotezwa

Hatarii..Ridhiwani Kikwete Atoa Povu kwa Serikali Juu ya Kukaa Kimya Sakata la Watu Kutekwa na Kupotezwa

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete ameitaka Serikali kutokaa kimya na kutoa maelezo ya matukio yanayotokea nchini ili kuondoa wasiwasi na hali ya sintofahamu kwa wananchi.
Ridhiwani amesema hayo jana Bungeni, Mjini Dodoma wakati akichangia mapitio na mwelekeo wa kazi za Serikali na bajeti ya ofisi ya Waziri mkuu kwa mwaka 2017/2017.
Ameitaka Serikali akiwemo Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kutokalia kimya matukio ya utekaji yanayoendelea nchini.

from Blogger http://ift.tt/2oya72R
via IFTTT


NJIA SITA ZA KUTUMIA MAJI KUJIKINGA NA MAGONJWA MBALIMBALI

Watu wengi wamekuwa wavivu wa kunywa maji, hawajui kuwa maji ni muhimu sana katika mwili na yanahitajika kwa kiwango kikubwa. Wengi hawajui kuwa maji ni tiba ya maradhi mengi. Ili maji yawe tiba ya magonjwa, ni lazima ufuate kanuni ya namna ya kuyatumia.
Maji huwa na faida nyingi. Zifuatazo ni baadhi ya faida za kunywa maji kwa wingi.
Maji husafisha figo. Figo kuwa na uchafu ama vimawe vidogo vidogo husababishwa na kutokunywa maji ya kutosha. Maji huyeyusha takataka zote zonazojiunda kutengeneza vijimawe katika mkojo. Hivyo kunywa maji mengi kutasaidia kusafisha figo zako.
Maji huponya maambukizi ya njia ya mkojo. Kadiri unavyokunywa maji mengi, ndivyo unavyokojoa zaidi. Kunywa maji kwa wingi kutasaidia kuondoa bakteria katika kibofu chako cha mkojo.
Maji husaidia kutuliza homa. Homa ni kuongezeka kwa kiwango cha joto mwilini kinachosababishwa na sababu mbalimbali. Kunywa maji mengi kutakusaidia kupunguza joto hilo kupitia mkojo. Kama una homa kunywa maji mengi na utapata ahueni.
Maji husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kunywa glasi moja au mbili muda mchache kabla ya kula kutakufanya ule chakula kidogo. Kwa vile maji hayana kalori yoyote, itakupunguzia uwezekano wa kunenepa.
Maji huifanya ngozi yako kuwa laini na nyororo. Maji yatasaidia kuilainisha ngozi yako na kukufanya uwe na macho ang’avu kama tu utayanywa kwa wingi kila siku.
Ushauri wa kiafya wa namna nzuri ya kunywa maji
Kunywa maji punde tu unapoamka. Mwili wako hupoteza kiwango kikubwa cha maji unapokuwa umelala, hivyo jitahidi kunywa maji kabla ya kwenda kulala na baada ya kuamka. Unapokunywa maji asubuhi, husaidia kuondoa sumu zote zilizotengenezwa mwilini ulipokuwa umelala.
Jitahidi kunywa glass 8 mpaka 12 kwa siku. Kulingana na kliniki ya afya ya Mayo, mtu mwenye uzito wa kilo 55 anatakiwa kunywa maji glass 8 wakati mtu mwenye uzito wa kilo 87 anatakiwa kunywa maji glass 12 kwa siku. Inabidi kuhakikisha kuwa rangi ya mkojo inakuwa nyepesi. Unashauriwa kutokunywa zaidi ya glass 16 kwa siku.
Usisubiri mpaka kiu ikupate ndipo unyewe maji. Wakati unapohisi kiu, inawezekana umeshapunguza glass 2 katika kiwango cha maji kinachotakiwa mwilini. Wazee huwa hawapatwi na kiu mara kwa mara, kwahiyo wanahitajika kunywa maji hata pasipo kuhisi kiu.
Kunywa maji mengi unapokuwa mgonjwa. Hata kama hujisikii kunywa maji, kiukweli unahitaji kunywa maji zaidi ili kuusaidia mwili wako kupambana na maradhi. Maji yanapopungua mwilini mwako, ndivo ugonjwa unavopata nguvu ya kukutesa.
Kunywa maji mengi kama hali ya hewa ni ya joto. Watu wanaoishi katika maeneo yenye joto kama Dar es salaam, wanatakiwa kunywa maji kwa wingi. Watu hawa wako katika hatari ya kupata matatizo ya figo kama hawatakunywa maji kwa wingi ukilinganisga na watu wanaoishi katika maeneo yenye baridi kama vile Iringa na Mbeya.
Kunywa maji, na siyo vinywaji baridi, vileo ama kahawa. Baadhi ya wataalamu wanaamini kuwa chai, soda na kahawa vinaweza kuongeza kiwango cha maji mwilini. Ingawa vinywaji hivyo vina kiwango kikubwa cha kaboni na sukari ambayo inaweza kuongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari na mifupa. Utafiti unaonyesha kuwa watu wanaokunywa vikombe 6 vya kahawa kila siku, huongeza maji mwilini kwa kiwango kidogo sana. Pombe ndiyo mbaya zaidi kwani hukusababisha ukojoe sana na kupoteza kiwango kikubwa cha maji mwilini.
Kunywa maji kwa wingi kama unafanya mazoezi. ukiwa unafanya mazoezi, unatakiwa kunywa maji kwa wingi kwa kuwa unakuwa umepoteza kiwango kikubwa cha maji mwilini. Ongeza nusu lita zaidi kwa kila nusu saa mpaka saa moja ya kufanya mazoezi. Kula ndizi kutakusaidia kuongeza kiwango cha madini ya potassium mwilini.
Tazama video Mtoto amvua kofia
 Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nm5qoH
via IFTTT


Wanafamilia Mbeya wakataa kumzika ndugu aliyefariki Sumbawanga

Familia ya marehemu Cleva Mlawizi (32), yenye makazi katika kijiji cha Ikolomela, wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, imegoma kuuzika mwili wa ndugu yao huyo kwa madai kuwepo kwa utata katika kifo chake.
Mwanamke huyo aliyekuwa akiishi Sumbawanga na mumewe alifariki usiku wa Machi 15. Mume wa marehemu alieleza kuwa baada ya chakula cha usiku alimuaga mkewe na kwenda kuangalia mpira kupitia runinga, lakini aliporudi alimkuta mkewe huyo akiwa amefariki tayari.
Ripoti ya daktari aliyefanyia uchunguzi maiti hiyo ilisema kuwa sababu ya kifo cha marehemu ilikuwa ni njaa.
Lakini msemaji wa familia alisema kuwa, baada ya mwili kusafirishwa kupelekwa Ikolomela, walikuta maiti ikiwa imevimba na inatokwa na damu kiashiria kuwa marehemu alipigwa na kitu kizito kichwani kabla ya kukutwa na umauti.
Kamanda wa Poilisi Mkoa wa Songwe, Mathias Nyange, alithibitisha kupokea malalamiko ya wanafamilia hao na kusema kwamba, baada ya kufika kituoni, polisi waliwaeleza kuwa kama hawakuridhishwa na maelezo ya uchunguzi wa daktari wa awali basi waupeleke mwili huo katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya ili ufanyiwe uchunguzi wa kina.

from Blogger http://ift.tt/2ny54QC
via IFTTT


Njia 5 za Kudumisha Mahusiano ya Kimapenzi…!!!

Japo inasemwa kuwa mapenzi hayana njia moja ya kufuatwa lakini kuna vitu ambavyo vinajulikana kuchangia katika kuboresha mahusiano baina ya wapenzi.
Mahusiano ya mapenzi yenye kudumu ni sharti yapandwe katika udongo wenye rutuba kama ulivyo mmea,yatahitaji maji ya kumwagilia na mbolea ya kukuzia. Na zaidi ya yote yanahitaji muda wa kukua kabla matunda kuonekana.
Uaminifu
Kumwamini mwenza wako ni jambo la msingi sana katika kudumisha mahusiano. Usimshuku mpenzi wako kuwa si muaminifu bila ushahidi wowote.
Kushukiwa kukosa uaminifu pasipo ukweli inasononesha sana na kumkosesha raha mpenzi wako.
Imesemwa na wanafalsafa wa mawazo ya binadamu kuwa “Unachofikiri na kuamini kinatokea” hivyo unashauriwa kutofikiri vibaya juu ya mpenzi wako kwani haileti afya katika mahusiano.
Hali kadhalika na wewe uwe mwaminifu na mwenye kusema kweli mara zote. Ongeeni juu ya mipango na mawazo yenu bila kufichana.
Watambulishe kwa mpenzi wako ndugu ,jamaa na marafiki wakaribu ili kumpa mwenza wako amani.
Weka muda kwajili ya Mwenza wako.
Mahusiano mazuri kati ya wapenzi yanahitaji muda wa wapenzi hao kukaa pamoja. Wapenzi wasio na muda wa kukaa wana hatari ya kupoteza mvuto wa mahusiano yao na hivyo kuhatarisha uhai wa mapenzi kati yao.
Kama wapenzi wapo mbali mbali basi wanahitaji kuweka muda wa kuongea kila inapowezekana.
Tafuta muda wa kutoka pamoja,hata kama mtaenda mkahawani kunywa chai au juisi tu,inatosha sana na inawaweka karibu zaidi.
Mawasiliano
Mawasiliano ni muhimu sana baina ya wapenzi.
Hata kama umebanwa na kazi pata dakika chache za kuongea na mpezi wako na kumtaka hali. 
Andika hata ujumbe wa maneno au barua pepe. Mwambie mpenzi wako ulipo kila mara inapobidi ili kumjengea imani na wewe na kumpa amani moyoni. Tuma ramani ya mahali ulipo kama unatumia simu ya “Smart” (Tuma location kwenye whatsapp)
Mawasiliano ni ufunguo wa kudumisha upendo.
Wakati kuwasiliana na mpendwa wako, kumbuka kwamba upendo ni muhimu. Ongea toka moyoni na si kwa ajili ya kutimiza wajibu tu,kwani mpezi wako atajua tu kama hakuna mahaba katika mawasiliano yenu hivyo kutoleta faida ile inayotegemewa.
Mawasiliano mengine ni yale ya kuelezana yaliyo moyoni. Mweleze mwenza wako linalokusibu ili kupata ufumbuzi wa pamoja. Wapenzi wanaoongea kwa utulivu siku zote watakuwa pamoja.
Zawadi
Tafuta kitu cha kumpa mpenzi wako. Si lazima kiwe na thamani kubwa.Inaweza ikawa pipi au matunda tu.
Mnunulie zawadi kila inapowezekana hasa unaposafiri au katika siku yake ya kuzaliwa.
Onyesha Upendo wako
Kila mtu anajinsi yake tofauti ya kuonyesha upendo, lakini vyovyote itavyokuwa ni jambo la muhimu sana kuonyesha hisia zako kwa mpenzi wako.
Mara nyingi wapenzi wa muda mrefu wanasahau juu ya hili.
Maneno kama “Nakupenda”au majina ya mahaba kama “Mpenzi” au ”La-azizi” yanachangia sana kuonyesha mapenzi na kumfanya mwenza wako kujisikia vizuri.
Maneno haya yanaposemwa kwa hisia halisi na toka moyoni yana mchango mkubwa katika kuboresha mahusiano.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://ift.tt/2ms2574
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


from Blogger http://ift.tt/2m3QXC4
via IFTTT


Kategori

Kategori