Showing posts with label 2017 at 12:40PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:40PM. Show all posts
JEFF BEZOS ATANGAZWA TAJIRI NAMBA 1 DUNIANI BAADA YA KUMPITA BILL GATES JANA

JEFF BEZOS ATANGAZWA TAJIRI NAMBA 1 DUNIANI BAADA YA KUMPITA BILL GATES JANA

Mwanzilishi wa Kampuni ya Amazon, Jeff Bezos amempita Bill Gates na kuwa tajiri namba moja duniani akimiliki utaji wa dola za kimarekani 90.6 bilioni (Tsh 203 trilioni).
Kupanda wa hisa za Amazon kwa asilimia 1.5 leo Alhamisi Julai 27 kulimaanisha kuwa tajiri huyo amempita mwanzilishi mwenza wa Microsoft, kwa mujibu wa taarifa za jarida la Forbes la nchini Marekani.
Forbes wameeleza kuwa Bezos ana utajiri wa $90.6 bilioni akimzidi Bill Gates aliyekuwa anashikilia nafasi hiyo akiwa na utajiri wa $90 billioni sawa na Tsh 201.5 trilioni.
Bezos ananakadiriwa kumilikia hisa milioni 80 za Amazon akiwa ni mwenye hisa nyingi zaidi ya mwingine yeyote.
Kwa miaka ya hivi karibuni amekuwa akijikita zaidi katika mradi wake wa Blue Origin unaohusika na urushaji wa rocket kwenda angani pamoja na Washington Post ambazo zote anazimiliki.
Bezos ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu (CEO) wa Amazon alizaliwa mwaka 1964 Albuquerque Jimbo laNew Mexico na alisoma Sayansi ya Kompyuta na Uhandisi wa Umeme katika Chuo Kikuu cha Princeton.
Alipohitimu alikwenda kufanya kazi na Wall Street lakini mwaka 1994 aliacha kazi na kwenda kuanzisha Amazon ambapo kwa mara ya kwanza Amazon ilianzishiwa katika karakana ya kutengenezea magari. Baada ya kampuni hiyo kuanza kufanikiwa na kujipanua katika nchi mbalimbali, mwaka 2000 alianzisha kampuni ya Blue Origin inayojishughulisha na masuala ya anga.
Mwaka 2013 akiendelea kujipanua, aliinunua Kampuni ya Washington Post kwa $250 milioni na ilipofika Mei 2017 alitajwa kuwa na utajiri wa $ 84.8 bilioni, lakini leo Julai 27, 2017 amefikisha utajiri wa $90.6 bilioni na kushikilia usukani wa mtu tajiri zaidi duniani.
Kwa mujibu wa Forbes, hawa ndio matajiri 10 wanaoongoza duniani;
  1. Jeff Bezos (53)- Amazon.com
  2. Bill Gates (61)- Microsoft
  3. Amancio Ortega (81)- Zara
  4. Warren Buffett (86)- Berkshire Hathaway
  5. Mack Zuckerberg (33)- Facebook
  6. Carlos Helu (77)- telecom
  7. Larry Ellison (72)- software
  8. Michael Bloomberg (75)- Bloomberg LP
  9. Bernard Arnault (68)- LVMH
  10. Charles Koch (81)- diversified

from Blogger http://ift.tt/2w61FZg
via IFTTT


Billnass afunguka sababu ya wasanii kuringa

Billnass afunguka sababu ya wasanii kuringa

Mzungu Mzee ‘Billnass’ anayesumbua na ngoma ya ‘Mazoea’ ameweka wazi kinachowafanya wasanii wengi waonekane wanaringa na kusema wengi wao hukumbuka mateso na manyanyaso ambayo huwa wanapitia kabla ya kutoboa lakini pia ni mbinu za kibiashara.
Billnass amefunguka hayo na kusema kuwa wasanii wengi siyo kwamba wanaringa bali huamua kukaa maisha ya mbali na wale watu kipindi walipokuwa wanatafuta misaada halafu wakawa wanawanyima, hivyo wanapotusua na wao wanakuwa hawataki mazoea.
“Mimi ni social sana ndo maana hata maneno mengi yananipata, wasanii wanaonekana wanaringa kwa sababu hawataki zile kujuana sana ndiyo kuharibiana CV so usinijue kama hauna plan B’ ndo mazoea hawataki. Unajua visasi siyo vizuri lakini kuna watu wakiwa wana ‘hustle’ huwa wanawakariri nani na nani walinipa msaada nani alinikazia kwa hiyo akifanikiwa anaamua kuishi maisha yake binafsi ya kukaa mbali na watu wanafiki” Amesema Billnass.
Hata hivyo msanii huyo ambaye ni mwanafunzi wa chuo cha CBE amedai licha ya kuwa anachukua kozi ya manunuzi (Procurement) anampango wa kuwa mfanyabiashara mkubwa na kabla ya kujiajiri atataka kuajiriwa na kufanyia kazi elimu yake.
“Nina ndoto za kuwa mfanyabiashara mkubwa, lakini elimu yangu ambayo naichukua lazima niifanyie kazi hata nikajiriwa miaka miwili inatosha kabisa ili niweze kwenda kujiajiri peke yangu kwenye biashara ninazoplan kuzifanya”, alimalizia Billnass.

from Blogger http://ift.tt/2oWUkM4
via IFTTT


Kategori

Kategori