Showing posts with label 2017 at 02:44PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:44PM. Show all posts
Wabongo Noma Aisee..Wametengeneza Tanzanite Feki na Kuziuza Kama Njugu…!!!

Wabongo Noma Aisee..Wametengeneza Tanzanite Feki na Kuziuza Kama Njugu…!!!

BAADHI ya wauzaji wa madini ya Tanzanite mkoani Arusha, wamelalamikia uwepo wa madini bandia ya Tanzanite hali ambayo imekuwa ikikwamisha soko la madini hayo.
Akizungumza mmoja wa wahanga wa utapeli huo Gidion Lekasho alisema kuwa yeye alinunua madini bandia ya Tanzanite ya Sh. milioni 8.
Alisema kutokana na matukio hayo kuendelea kila siku sasa ni wakati muafaka kwa wizara ya madini kulifuatilia suala hilo hasa katika maonyesho ya madini ya vito yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni.
“Katika kipindi cha hivi karibuni kumekuwepo na tatizo la uwepo wa madini bandia ya Tanzanite hali mbayo inatajwa kutishia soko la madini hayo, huku baadhi ya wauzaji wakipata hasara,” alisema.
Mjiolojia kutoka Wizara ya Nishati na Madini Kanda ya Kaskazini, Salome Timanywa alisema madini yanapochimbwa yana umbo lake, hivyo wao kama wataalamu wanatambua kutokana na umbo la madini hayo.
Alisema wamejipanga vizuri ili waweze kukabiliana na hiyo changamoto na kuwataka wauzaji kufika wizarani ili kuweza kubaini madini feki na ambayo siyo feki.
Kaimu Kamishna wa Madini Kanda ya Kaskazini, Adam Jumaa alikiri kuwepo kwa tatizo hilo la madini bandia na kueleza kuwa katika maonyesho ya madini ya vito yatakayofanyika, tayari wana wataalamu wa kuyatambua madini hayo

from Blogger http://ift.tt/2o7djDM
via IFTTT


Auawa Baada ya Kuruka uzio na Kuingia Kwenye ikulu ya Kenya

Auawa Baada ya Kuruka uzio na Kuingia Kwenye ikulu ya Kenya

Walinzi wa Rauis walimpiga risasi na kumuua mtu aliyeingia kwenye ikulu ya Kenya, Jumapili ya majuzi wakati Rais Uhuru Kenyatta akihudhuria mashindano ya golf huko Muthaiga, kwa mujibu wa gazeti la Sunday Nation.
Katika tukio hilo ambalo limebaki kuwa siri kubwa wakati uchunguzi ukiendelea, mtu huyo asiyefahamika na mwenye umri wa makamo, alidaiwa kuingia bila ruhusa kwenye maeneo yanayolindwa vikali kabla ya saa 11 jioni na alikuwa kwenye eneo la maegesho, si mbali sana na jengo lenyewe na ndipo walinzi walipomuona.
Vyanzo vimeliambia gazeti hilo kuwa maafisa wa usalama wanaamini mtu huyo aliruka uzio wa ikulu hiyo sababu haiwezekani kuingia ndani bila kupita getini ambako nako hadi uruhusiwe.
Hii ni mara ya kwanza mtu yeyote kupigwa risasi na kuuawa ndani ya viwanja vya ikulu, lakini hilo ni tukio la tatu kwa mtu kuingia bila ruhusa tangu Rais Kenyatta ahamie humo mwaka 2013.
Chanzo kimoja kimesema mtu huyo alikuwa na kisu na kingine kudai hakuwa na silaha. Mwili wake ulipelekwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti jijini Nairobi na hadi Ijumaa hakukuwa na mtu aliyeenda kuulizia.

from Blogger http://ift.tt/2nvVDfG
via IFTTT


Kategori

Kategori