Madiwani 6 wa Chadema wilaya ya Arumeru mkoa wa Arusha wamejiuzulu na kujiunga na CCM
Katibu wa Chadema kanda ya Kaskazini Amani Gulugwa amesema wana ushahidi wa CCM kuwahonga madiwani hao na wameshachukua hatua za kisheria kudhibiti mwenendo huo
Diwani wa kata ya Majengo Emmanuel Kivondo anasema viongozi wa CCM wanatafuta mbinu ya kukaa naye wazungumze lakini wanashindwa
CCM Arumeru nao wamekanusha vikali tuhuma hizo wakisema madiwani hao wamehama kwa hiyari yao wenyewe na bado wengine wapo njiani kujiunga na CCM kwani wanaona hawapo sehemu salama VIDEO:
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Dk Leonard Masale, ameachia kazi rasmi baada ya kufikisha umri wa kustaafu kwa mujibu wa sheria za utumishi wa umma.
Masale aliyeteuliwa na Rais Dkt Magufuli Juni 26, 2016 amefikisha umri wa miaka 60 ambao kwa mujibu wa sheria anatakiwa kustaafu kwa lazima.
Kiongozi huyo mstaafu amethibitisha kuwa hayupo ofisini kuanzia Julai Mosi mwaka huu na kwamba nafasi yake inakaimiwa na Mkuu wa Wilaya ya Magu, Khadija Nyembo.
Aidha alisema kuwa tayari amepokea mafao yake ya kustaafu kutoka mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma, PSPF, baada ya kuwaandikia barua kuwajulisha kuhusiana na kustaafu kwake miezi sita iliyopita.
Pia Masale amesema kuwa bado anazo nguvu ana anaweza kulitumikia taifa katika nafadi yoyote atakayoteuliwa kuishika.
Mkuu wa Jeshi la polisi nchini (IGP), Simon Sirro amewataka makamanda wa polisi mikoa kuhakikisha wanatumia vizuri mafuta ya magari wanayowekewa ili kuepuka malalamiko ya wananchi kwa magari ya polisi kukosa mafuta.
Pia amesema hataki kusikia polisi hawajafika katika tukio kutokana na kisingizio cha kutokuwa na mafuta.
IGP Sirro alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jana mkoani Morogoro na kuongeza kuwa ni kosa kwa mwananchi kudaiwa fedha za mafuta ya gari la polisi.
IGP Sirro yupo katika ziara ya kuangalia hali ya uhalifu katika mikoa akitokea mkoani Dodoma.
Alisema mafuta ya gari yapo katika bajeti ya Jeshi la Polisi kwa kila mkoa hivyo kinachotakiwa ni makamanda wa mikoa kuhakikisha kuwa wanayatumia vizuri.
“Ni jambo la kusikitisha mwananchi kutakiwa kuchangia mafuta ya gari la polisi,hili hatuliruhusu kabisa,” alisema Sirro
Hivi karibuni, wakazi wa Malinyi walimlalamikia Mkuu wa Wilaya hiyo Jacob Kassema kwa kuwachangisha Sh800,000 za mafuta ya gari lake. Hata hivyo, Kassema alikanusha suala hilo.
Mbali ya suala la mafuta, IGP Sirro aliwatoa hofu wananchi na kusema Serikali inaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu mauaji yanayoendelea mkoani Pwani.
“Ni kweli kuna tatizo la mauaji Pwani lakini askari wetu wapo kazini mchana na usiku kutafuta suluhisho la tatizo,” alisema Sirro.
Kama Mtanzania niishie Dar es Salaam kuna mambo hupaswi yakupite. Wengi walikuwa wakitegemea mheshimiwa Rais kumtupilia mbali Makonda/Bashite ila haijawa kama mategemezi ya wengi kuwa hivyo.
Hii inatokana na sababu mbalimbali kama zifuatazo
i) Vita ya Dawa za Kulevya. Wengi tunajua vita hii ilivyo ngumu na hii ndo iliomfanya mpaka siri zake zikafichuka na raisi mwenyewe akaisapport hiyo vita na kutaka iendelee. Sasa leo hii akimtumbua kwa visa vilivyoibuka kutokana na madawa ya kulevya itakuwa ni usaliti na kutokuwa na maana.
ii) Kuna watu wanaopinga kila kitu afanyacho Rais, hapa nasemea Instagram pamoja sana sana pamoja na wanasiasa wanaopinga kila kitu kinachofanywa. Imagine mtu anapinga hadi kuletwa kwa ndege au flyover zinajengwa mtu anapinga (watanzania hatuko serious)
Kuna hadi wengine wanataka ufisadi urudi ili maisha yapungue ugumu. Wengine wakawa wanasema ni mpango wa ikulu kumtuma afanye hivyo ili wamtoe wafunike skendo na udhaifu wa serikali.
Mtu kama huyu utafata atakachokushauri na ina maana ukifata umempa kiburi aonekane yeye ndo yeye na atakaloamua nchi nzima inafata, liwe baya au zuri. Na mwenendo kama huo ungefanya serikali iwe dhaifu kupita kiasi
So ndo maaana Magufuli akaita hiyo call
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI
Bilionea Mmarekani anayefahamika pia kwa kutoa pesa za hisani kuwasaidia wasiojiweza David Rockefeller amefariki dunia akiwa usingizini nyumbani kwake Poncantico Hills, New York.
Alikuwa na umri wa miaka 101.
Bw Rockefeller alikuwa wa mwisho wa kizazi chake cha familia hiyo maarufu nchini Marekani.
Alikuwa mjukuu wa mwanzilishi wa kampuni ya Standard Oil John D Rockefeller.
Mzee huyo ndiye aliyekuwa anasimamia mali na biashara za familia hiyo, pamoja na miradi yake ya kusaidia jamii.Alikuwa kijana wa kiume mdogo zaidi kati ya wana watano wa kiume wa John D Rockefeller Jr.
Ingawa hakuwahi kutafuta wadhifa wowote wa kisiasa, kaka zake wawili walihudumu serikali.
Nelson Rockefeller alihudumu kama gavana wa New York na kwa muda kama Makamu wa Rais wa Marekani.
Winthrop Rockefeller naye alikuwa gavana wa Arkansas.Haki miliki ya pichaGEORGE HW BUSHImage captionRais wa zamani wa Marekani George HW Bush amesema amehuzunishwa sana kwa kumpoteza rafiki yake mzuri sana
David Rockefeller alihitimu kutoka chuo kikuu cha Harvard mwaka 1936 na akapokea shahada ya uzamifu katika uchumi kutoka Chuo Kikuu cha Chicago mwaka 1940.
Alitumikia jeshi wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia na baadaye akafanya kazi katika benki ya Chase Bank, ambayo baadaye ilikuwa benki ya JP Morgan Chase.
Bw Rockefeller alimiliki kazi za sanaa za thamani ya $500m (£404m).
Alipokuwa anasherehekea kutimiza miaka 100 mwaka 2015, alitoa ardhi ya ekari 1,000 kwa mbuga ya taifa katika jimbo la Maine.
Juhudi zake za kusaidia jamii zilimfanya kutunukiwa Nishani ya Uhuru ya Rais mwaka 1998.
Alikuwa na watoto wanne – David Jr, Richard, Abby, Neva, Margaret na Eileen.
Mkewe Margaret (jina lake la kuzaliwa McGrath) alifariki 1996
Upelelezi wa kesi ya
kutumia dawa za
kulevya inayomkabili
Msanii Agnes Gerald maarufu kama Masogange (28) katika Mahakama ya Kisutu bado haujakamilika na
imeahirishwa,
huku akishindwa kufika mahakamani hapo kutokana na kukwama kwenye foleni.
Wakili wa Serikali, Adolf Mkini aliyaeleza hayo leo wakati kesi ilipotajwa kwa Hakimu Mkazi Mkuu,
Wilbroad Mashauri.
Mkini alidai kuwa upelelezi bado haujakamilika na mshtakiwa hayupo mahakamani hapo.
Baada ya kueleza hayo, wakili wa Masogange,
Nictogen Itege ameiarifu Mahakama kuwa mteja wako hiyo
alikuwa njiani kuelekea mahakamani lakini alikwama katika foleni eneo la Jangwani.
Kesi imeahirishwa hadi Aprili 20, 2017 kwa ajili ya kutajwa ili kuangalia kama upelelezi utakuwa
umekamilika ama la.
Masogange anakabiliwa na mashtaka mawili ya kutumia dawa za kulevya aina ya Heroin na Oxazepam.
KAMA ULIMIS VIDEO YA MCHEZAJI WA Ghana ALIE JIKANYAGA KWA KUWASHUKURU MUKE NA MCHEPUKO WAKE TAZAMA HAPA