Showing posts with label 2017 at 02:15PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:15PM. Show all posts
MALINZI NA VIGOGO WENGINE WA TFF WAKWAMA TENA MAHAKAMANI

MALINZI NA VIGOGO WENGINE WA TFF WAKWAMA TENA MAHAKAMANI

Kesi inayowakabili Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wa shirikisho hilo Selestine Mwesigwa imeahirishwa hadi Julai 31 mwaka huu na watuhumiwa hao kurejeshwa rumande kwa kile mahakama ilichosema kuwa ni kutokamilika kwa upelelezi.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam imetoa uamuzi huo leo asubuhi baada ya watuhumiwa hao wanaokabiliwa na jumla ya mashtaka 28 yakiwemo ya kughushi nyaraka, uhujumu uchumi na matumizi mabaya ya ofisi.
Malinzi na vigogo wengine wa TFF walikamatwa mwezi Juni na kupandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza Juni 29 kujibu tuhuma hizo zinazowakabili.

from Blogger http://ift.tt/2uzR2kZ
via IFTTT


TAZAMA PICHA ZA MAPOKEZI YA KLABU YA EVERTON JIJINI DAR ES SALAAM

TAZAMA PICHA ZA MAPOKEZI YA KLABU YA EVERTON JIJINI DAR ES SALAAM

Klabu ya Liguu ya soka nchini Uingereza, Everton imewasili salama katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere saa nne asubuhi ya leo kwa ajili ya mchezo wao wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Barclays dhidi ya klabu ya Gor Mahia utakaopigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Klabu hiyo imetumia ndege binafsi kutoka Uingereza mpaka Dar es salaam ambapo wamepata mapokezo makubwa kutoka kwa mashabiki wa soka nchini, hasa wanaofatilia kwa karibu ligi kuu ya Uingereza na mchezaji mashuhuri aliyehamia klabu hiyo wiki iliyopita kutokea kwa Mashetani wa jijini Manchester, Wayne Rooney.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ameongoza umati mkubwa wa mashabki wa soka waliojitokeza uwanja wa ndege asubuhi hii kuilaki timu ya Everton, jambo lililowafurahisha sana timu nzima ya wakali hao wa Ligi Kuu ya Uingereza.
Katika tovuti ya klabu ya Everton, kikosi hicho kimeelezea kufurahishwa kwake na mapokezi makubwa waliyoyapata kutoka kwa ngoma za kabila la Kimasai na wananchi waliojitokeza kuwapokea na kwamba wachezaji wakikosi hicho wana hamasa kubwa ya kuona vivutio vya Tanzania kwa siku chache zijazo watakazokuwa hapa nchini.
Katika tovuti ya klabu hiyo, Everton wameandika:
“Tumepata mapokezi makubwa sana, ni jambo la kuvutia sana kwetu tulipopokewa na Wamasai. Ni jambo ambalo hatuwezi kabisa kuliona huko kwetu. Tumeshuka moja kwa moja kutoka kwenye ndege na sote tunafurahi sana kuwa hapa.””Tutafanya mazoezi leo usiku na tunausubiri kwa hamu mchezo wetu wa kesho. Lakini kwa sasa tutapimana ubavu tu kwakuwa tumerudi kutoka kambini wiki iliyopita tu. Itakuwa ni mchezo mzuri kwa kujipima nguvu na ni mategemeo yetu kwamba mashabiki wa hapa watajitokeza kwa wingi na wataufurahia mchezo huo.”Klabu hiyo itamenyena na Gor Mahia kesho Alhamis saa 11 jioni katika mchezo huo wa kirafiki. Gor Mahia imefanikiwa kupata nafasi hii baada ya Kampuni ya Bahati Nasibu za Michezo (SportPesa) kuendesha ligi ndogo iliyolenga kupata mshindani wa Everton. Klabu zote za Tanzania zilizoshiriki kwenye ligi hiyo zilitolewa na zote zitabaki kuwa watazamaji.
Tazama picha za mapokezi ya klabu ya Everton iliyowasili nchini leo hii:
Shabiki mnazi wa timu hiyo aliyetangulia kuja nchini siku chache zilizopita, Andrew Pemberton ameposti kwenye akaunti yake ya mtandao wa Twitter akiwaambiwa wenzake kwamba:
“Nimeipeperusha vyema bendera ya Everton nchini Tanzania kwahiyo natumai wenzangu mtanendelea pale nilipoishia mimi.”
Ujumbe huo ameuandika akiweka picha ambayo amepiga akiwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro. Mlima mrefu kuliko yote barani Afrika ambapo alipiga picha hito akiwa ameshika bendera ya klabu yake.
Kikosi cha Eveton chenye wachezaji 25 kilichowasili leo ni:
Maarten Stekelenburg, Mateusz Hewelt, Chris Renshaw, Tom Davies, Phil Jagielka, Ashley Williams, Callum Connolly, Jonjoe Kenny, Michael Keane, Muhamed Besic, Leighton Baines, Morgan Schneiderlin, James McCarthy, Davy Klaassen, Gareth Barry, Idrissa Gana Gueye, Joe Williams, Kieran Dowell, Kevin Mirallas, Wayne Rooney, Aaron Lennon, Dominic Calvert-Lewin, Ademola Lookman, Matthew Pennington, Yannick Bolasie.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2tdybXw
via IFTTT


China Wazindua Basi la Ajabu Linaloruhusu Magari Kupita Chini Yake..Linaweza Kupakia Abiria Zaidi ya 300 kwa Mkupuo..!!

China Wazindua Basi la Ajabu Linaloruhusu Magari Kupita Chini Yake..Linaweza Kupakia Abiria Zaidi ya 300 kwa Mkupuo..!!

CHINA inaendelea kufanya makubwa kwenye ulimwengu wa teknalojia na sasa inazindua basi kubwa la aina yake ambalo kwa chini litaruhusu magari mengine kupita kama ilivyo kwenye daraja.
Mfumo huu mpya wa usafiri ni sawa na mwendo kasi zinazohudumia wakazi wa Jiji la Dar es Salaam lakini huu ni wa kisasa zaidi.
Basi hilo lenye mita mbili kwenda juu linaitwa TEB na litaanza kuhudumia umma wa Wachina kuanzia Agosti mwaka huu.
Likitumia nguvu ya umeme, basi hilo linauwezo wa kubeba hadi abiria 300 kwa mara moja huku likiwa na urefu wa futi 72 na upana wa futi 25. Basi hili litaweza kupita hata sehemu yenye foleni kwa sababu ya upana wake na nafasi ya wazi iliyo kwa chini ikiyaacha magari mengine kwenye foleni
Video ya basi hilo la kwanza kutengenezwa, ilizua mjadala huku likiwashangaza wengi baada ya kuwekwa hadhari mwishoni mwa Mei.
Majaribio ya basi hilo tayari yameshafanyika katika mji wa Qinhuangdao ulioko kaskazini mashariki mwa China.
Basi hilo ambalo lina uwazi mkubwa chini yake kiasi cha kuruhusu magari mengine kupita, linaweza kukimbia hadi kufikia kilomita 60 kwa saa huku likivuka reli pamoja na kupita katika njia za barabara za kawaida.
“Faida moja kubwa ni kuwa basi hili litatumia nafasi ndogo wakati linapokuwa ya barabarani,” Injinia wa mradi huo Song Youzhou aliliambia shirika la habari la China Xinhua.
Basi la TEB linafanya kazi kama ambavyo Subway linafanya lakini gharama za utengenezaji ni nafuu zaidi ukulinganisha na Subway,” anaeleza injinia mwingine Bai Zhimini.
Basi hilo la TEB litaweza kufanya kazi inayofanywa na mabasi ya kawaida 40 kulingana na maelezo ya watengenezaji wake. Hata hivyo, bado haijafahamika ni lini litatumika kwa wingi katika miji mbalimbali nchini China.
Kwa mara ya kwanza, wazo la kuwa na basi la aina hii lilionekana kama mzaha hasa baada ya kampuni inayolitengeneza kuonyesha mchongo mdogo kwenye maonyesho ya kimataifa ya teknolojia za hali ya juu ya Beijing.
Baada ya maonyesho hayo, kampuni mzalishaji ilitengeneza basi la kwanza ambalo lilifanyiwa majaribio na kuonyesha ufanisi mkubwa barabarani. Mamilioni ya watu walivutiwa na kushangazwa na basi hilo baada ya video yake kuwekwa mtandaoni.
Niliona picha za basi hili muda si mrefu uliopita lakini sasa naona zimegeuka kuwa basi kweli. Basi hili limejengwa kwa mwendo wa Kichina,” anasema mmoja wa watu waliolishuhudia basi hilo.
Likitazamwa kama mwarubaini wa foleni, TEB limeweza kuwa la aina yake kwa kuwa litaweza kutumia njia moja na magari mengine, pia halitalazimika kusimama wakati magari mengine yakisimama wakati wa foleni kali.
Barabara zetu bado zinakabiliwa na changamoto ya foleni,” anasema Wang Yimin mkazi wa mji ambao basi hilo lilifanyiwa majaribio ya kwanza.
Wazo la kutengeneza basi la aina hii lilikuwapo tangu mwaka 2010 wakati Jarida la Times lilipoandika makala ya kushawishi kampuni zenye uwezo kuwekeza kwenye usafiri ambao utasaidia kupunguza foleni barabarani.
Kampuni ya TEB Technology Development ilionekana kuvutiwa na wazo hilo na kuamua kulifanyia kazi. Mradi huo ambao kama utaweza kwenda kama unavyotarajia utasaidia tatizo la foleni na unaelezewa kuwa ni wa gharama nafuu ukilinganisha na aina nyingime za usafiri wa umma.
Vyombo vya habari vya Serikali ya China vilielezea kuwa uzinduzi wa huduma hiyo ulikuiwa wenye mafanikio makubwa huku tukio lake likivutia vyombo vya habari vya kimataifa kama shirika la habari la kimataifa la Reuters ambalo pia lilipewa nafasi ya kutembelea mradi huo pamoja na kufanya mahojiano ya kina.
Bila haka kama aina hii ya mabasi ingeletwa Tanzania na hususani Jiji la Dar es Salaam, pengine ingekuwa ni suluhisho la tatizo la kujazana kwenye mwendo kasi zetu ambazo zinaonekana kushindwa kuhudumia umma.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t8NIZb
via IFTTT


JPM- Kama Umefoji Cheti Kwenye Serikali Yangu Jiandae Kutumbuliwa..!!!

JPM- Kama Umefoji Cheti Kwenye Serikali Yangu Jiandae Kutumbuliwa..!!!

Rais Magufuli leo wakati akizindua majengo ya Hostel za Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM) amefunguka na kusema sasa anasubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wanatumia vyeti vya kufoji.
Rais Magufuli amesema kumekuwa na changamoto kubwa katika kila sekta hivyo sasa anasubiri hiyo ripoti ili aweze kuifanyika kazi na kutenda haki katika jambo hilo.
“Naisubiri ripoti ya wafanyakazi wa Serikali zaidi ya elfu tisa ambao wana vyeti vya kufoji ili niifanyie kazi” alisema Rais Magufuli 
Mbali na hilo Rais Magufuli ameitaka Taasisi ya TCU kuacha kuwapangia wanafunzi vyuo bali wanafunzi wanapaswa kuwa huru kuchagua aina ya vyuo ambavyo wao wanataka kwenda na kusema kwa kufanya hivyo itatoa nafasi kila chuo kuwa na wanafunzi wa kutosha huku wanafunzi pia wakienda kusoma sehemu ambazo wao wanahitaji kwenda kusoma na si kuwapangia. 
“Mtu amefaulu ana sifa zake anataka kuja kusoma Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam afaidi mabweni ya Magufuli analazimishwa kupelekwa kwenye ka chuo ambako wala hakana jina hata ukitafuta kwenye mtandao hakaonekani, akasome pale wakati hawana hata mabweni na saa zingine hata walimu hawana, tunawatesa watoto hawa na saa zingine wakuu wa vyo vile wamekuwa na tabia ya kwenda kwenye uongozi wa TCU ingawa sina ushahidi wapangiwe idadi wa wanafunzi wanaowataka kwenye vyo hivyo, sifahamu wanapangiwa kwa rushwa lakini wapo pia kuna ushahidi na baadhi ya viongozi wa vyuo fulani fulani waliofunga safari kwenda TCU kwa ajili ya kuomba wapangiwe wanafunzi au kutoa shukrani, au hata kwenda kuwasalimu tu” alisema Rais Magufuli

from Blogger http://ift.tt/2plQysA
via IFTTT


Walioua Askari 8 Wilayani Kibiti Nao Wauawa..!!

Walioua Askari 8 Wilayani Kibiti Nao Wauawa..!!

Jeshi la Polisi Tanzania limesema limewaua majambazi wanne ambao walikuwa ni sehemu ya kundi la majambazi lililowashambulia na kuwaua askari 8 wilayani Kibiti mkoani Pwana jana usiku.
Akizungumza na wanahabari leo, Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa jeshi hilo, Nsato Marijani amesema kuwa mara baada ya kundi hilo kuwashambulia askari, kikosi kingine cha askari kilifanya msako na kubaini maficho ya majambazi hao.
Amesema baada ya kuwabaini, yalifanyika mashambulizi ya kurushiana risasi, ambapo majambazi wanne waliuawa pamoja na kukamata bunduki 4 zikiwemo SMG mbili zilibainika kuwa kati ya zile zilizoporwa na majambazi hao.
Akielezea tukio hilo lilivyokuwa, Kamishna Marijani amesema kundi la waharifu walikuwa na silaha za moto na ambao idadi yao haikujulikana liliweka mtego na kufanikiwa kuishambulia kwa risasi gari iliyokuwa na askari 9 waliokuwa wakitoka katika malindo kurudi kambini, na kuwaua askari 8 kati yao huku mmoja akijeruhiwa mkononi.
Amewataja askari waliuawa kuwa ni pamoja na Mkaguzi Msaidizi Peter Kiguu, Koplo Francis, PC Haruna, PC Jackson, PC Zakaria, PC Siwale, PC Maswi na PC Ayoub, ambapo pia walipora bunduki 7 zikiwemo SMG 4.
Kufuatia tukio hilo, Kamishna Marijani ametangaza vita na waharifu wote katika maeneo hayo, ambapo amesema vyombo vya ulinzi na usalama vinaanza oparesheni maalum katika mkoa wa Pwani, kuhakikisha vinawasaka na kukomesha mauaji hayo ikiwa ni pamoja na kuwachukulia hatua.
Mpaka sasa jeshi limekwisha poteza skari zaidi ya 10, inatosha…. Tunakwenda kweny oparesheni maalum, hatutakuwa na mzaha, tutawasaka popote walipo na kuwashughulikia kikamilifu, ,,, watajua tofauti ya moto na maji… mpaka jana idadi ilikuwa ni 8 kwa nne, lakini nawahakikishia kuwa ndani ya wiki moja idadi hiyo itakuwa imebadilika, na tutakuwa na hesabu tofati” amesema Marijani
Kuhusu hofu ya ugaidi, Kamishna Marijani amesema tukio hilo siyo la kigaidi bali ni uhalifu wa kawaida, huku akibainisha kuwa Tanzania hakuna ugaidi
Katika hatua nyingine, jeshi hilo limepiga marufuku uendeshaji wa pikipiki katika maeneo yote ya Kibiti, Mkuranga na Rufiji zaidi ya saa 12:00 jioni. Amesema usafiri wa boda boda utaruhusiwa kati ya saa 12:00 asubuhi hadi saa 12:00 jioni

from Blogger http://ift.tt/2pij4y3
via IFTTT


Mwakyembe Amtaka Makonda Ajibu Maswali 9

Mwakyembe Amtaka Makonda Ajibu Maswali 9

Waziri wa Habari, michezo na utamaduni Dr Harrison Mwakyembe amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Daresalaam ajibu maswali tisa ambayo yalipelekea kuvamia kituo cha habari cha Clouds televisheni, Mh Mwakyembe ameeleza kwamba kitendo cha Makonda kuvamia kituo cha luninga cha Clouds kitendo hicho hakikubaliki, hivyo anapaswa kujibu maswali kadhaa katika kuhoji upande wa pili maana kitendo hicho kimelaaniwa sana na jukwaa la wanahabari Tanzania na wadau wengine wa habari ndani na nje ya nchi.
Nipashe.

from Blogger http://ift.tt/2od5oUg
via IFTTT


Tabia Hizi 5 Zitakufanya Uwe na Maisha Mafupi Sana Hapa Duniani..!!!

Kwa kawaida maisha ya kibinadamu mwisho wake huwa ni kufa, hivyo kila mwenye pumzi hii leo mwisho wa maisha yake huishia kaburini.
Hata hivyo, kumekuwepo na viashiria fulani fulani ambavyo huweza kuashiria baadhi ya makundi fulani ya watu huenda wanaweza kuwa na muda mfupi wa kuishi duniani kutokana na sababu tofauti tofauti.
Miongoni mwa dalili ambazo huweza kuashiria mhusika anaweza kuwa na maisha mafupi duniani ni pamoja na hizi zifuatazo.
1. Watu wenye kupenda maisha ya anasa na starehe
Watu wa aina hii huwa katika hatari ya kupoteza maisha haraka hata kabla ya siku zao kutokana na kuwa na hatari kubwa ya kupatwa na magonjwa mbalimbali yakiwemo ya zinaa.
2. Wavutaji wa sigara.
Watu wanaovuta sigara huwa katika hatari ya kuishi maisha mafupi zaidi kuliko wale ambao hawatumii sigara kwani watu wa aina hii huwa katika hatari ya kukumbwa na saratani ambayo huweza kukatisha uhai wa mhusika hata kabla ya siku zake.
3. Kushinda umekaa siku nzima
Wale ambao huwa miili yao haina mazoezi kabisa nao huwa katika hatari ya kupoteza maisha mapema kutokana na kushambuliwa na magonjwa yasiyoambukiza kama vile shinikizo la damu, kisukari nk.
4. Unywaji wa pombe
Watumiaji wa vileo na huwa katika hatari ya kupoteza maisha yao mapema kutokana na mambo mawili makuu
a) Kupata ajali kutokana na kutumia vyombo vya moto wakati wakiwa wamelewa na baadaye kujikuta wanapoteza maisha.
b) Ugomvi ambao huweza kuibuka kutokana na mihemko ya vilevi wanavyokuwa wamekunywa na kuweza kusababisha ugomvi mkubwa. Mfano kupigana na chupa na baadaye kupoteza uhai.
5. Ulaji wa vyakula vya viwandani
Kuna wale ambao mara nyingi wamekuwa wakila vyakula vya makopo ambavyo vinapotumiwa mara kwa kwa mara huweza kuwa na madhara kadhaa likiwemo tatizo la saratani. Hivyo kundi hili nalo linaweza kuwa katika hatari ya kupoteza maisha kabla ya siku zao.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2nT5Nvh
via IFTTT


Kategori

Kategori