Showing posts with label EAC NA KENYA. Show all posts
Showing posts with label EAC NA KENYA. Show all posts
Kikwete ahutubia bunge la Kenya

Kikwete ahutubia bunge la Kenya


Rais Kikwete waTanzania
Rais Kikwete waTanzania
Rais Jayaka Kikwete wa Tanzania amehutubia mabaraza mawili ya Bunge la Kenya mjini Nairobi Jumanne alasiri na kusema uhusiano kati ya Kenya na Tanzania utaendelea kuimarika zaidi na uongozi ujao wa Tanzania.
Rais Kikwete aliwasili katika majengo ya bunge Nairobi mwendo wa saa tisa na dakika 40 na kulakiwa na kundi kubwa la wabunge na wanachama wa Baraza la Senate waliokuwa na hamu ya kumsikiliza kiongozi huyo wa Tanzania anayetarajiwa kustaafu kwenye uongozi baada ya matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Tanzania tarehe 25 mwezi huu.

Kulikuwa na ulinzi mkali katika majengo ya bunge na wabunge wa chama tawala na wale wa upinzani walimiminika kwa wingi ndani ya majengo ya Bunge.
Baadaye Rais Kikwete aliwahutubia wabunge na kusema ni siku 19 kabla ya uchaguzi mkuu Tanzania na alialikwa na Rais Kenyatta kufika Kenya kuwaaga raia wa Kenya. Amesema Kenya ni rafiki na mshiriki mkubwa wa Tanzania. Amesema baada ya mkasa na ghasia za uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya alifika mara moja hapa Nairobi kutatua mzozo huo bila kualikwa isipokuwa kwa yeye mwenyewe kuomba kwenda Kenya kusaidia kupata ufumbuzi.
Ziara ya Rais Kikwete hapa Nairobi imekuwa na shughuli nyingi. Gavana wa jiji kuu la Nairobi Evans Kidero amemtunukia Rais Kikwete heshima kuu kwa kumkabidhi ufunguo maalum kama ishara ya mtu huru mjini Nairobi. Pia barabara mashuhuri ya Milimani imebadilishwa jina na kupewa jina la Jakaya Kikwete Road.

Idara ya Uhamiaji ya Kenya yalaumiwa

Idara ya Uhamiaji ya Kenya yalaumiwa


Wakenya wanatumia njia za mkato kupata stakabadhi wanazohitaji, na hilo ni hatari kwa usalama wa taifa.
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru KenyattaKwa kipindi kirefu wakenya hasa wakaazi wa eneo la Pwani wamelalamikia kunyanyaswa na idara za usajili wa watu na ile ya uhamiaji  wakati wa kutoa vitambulisho vya kitaifa, vyeti vya kuzaliwa au hati za kusafiria.
Kutokana na malalamiko  hayo tume ya utekelezaji haki  imefanya uchunguzi na kutoa ripoti kuhusu chanzo cha matatizo hayo na kutishia  usalama wa taifa hilo.
Taarifa zinasema kwenye ripoti hiyo ni asilimia 2.8 ya wakenya wanaridhika  na huduma zinazotolewa na idara ya kutoa vitambulisho na uhamiaji , idara ambazo zinawafanya  wakenya kukosa stakabadhi halisi za kujitambulisha.
Naibu mwenyekiti wa tume hiyo Regina Muatha amesema kuwa hatua hiyo imesababisha wakenya kutumia njia za mkato kupata stakabadhi hizo suala ambalo ni hatari kwa usalama wa taifa.
safari za KQ zarejeshwa

safari za KQ zarejeshwa


Marufuku juu ya safariza anga za shirika la ndege la KQ yafutwa .
Hatimaye marais Uhuru Kenyetta wa Kenya na Jakaya Kikwete wa Tanzania wamekubaliana kufutilia mbali maagizo ya Mamlaka ya anga nchini Tanzania kupunguza idadi ya ndege za Kenya zinazotua nchini Tanzania na agizo la Wizara ya maliasili ya Kenya kupiga marufuku magari ya Tanzania kuingia katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Katika makubaliano hayo ndege za Kenya Airways sasa zitafanya safari zake kama kawaida nchini Tanzania na magari ya Tanzania yataruhusiwa kuchukua watalii na abiria katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta.
Kutoka Dar es Salaam Arnold Kayanda na taarifa ifuatayo.
Akizungumza na waandishi wa habari waziri wa mambo ya nje wa Tanzania Bernald Membe amesema uamuzi huo umefikiwa baada ya viongozi hao wakuu wa nchi hizo mbili kukutana nchini Namibia walikokwenda kuhudhuria maadhimisho ya miaka 25 ya uhuru wa Namibia na kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo.
Awali kabla ya uamuzi wa marais hao, magari ya Tanzania yaliyokuwa yakichukua watalii katika uwanja wa ndege wa Jomo Kenyatta, yalipigwa marufuku na serikali ya kenya katika agizo lililotangazwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Biashara na Utalii Phyllis Kandie, ambapo baadae Tanzania nayo kupitia mamlaka ya Anga ya nchi hiyo ikaagiza ndege za shirika la ndege la Kenya, Kenya airways zinazoingia Tanzania kupunguza safari kutoka 42 kwa wiki hadi 14 pekee.
Makubaliano ya marais hao yanakuja siku chache baada ya mzungumzo ya mawaziri wa utalii wa Tanzania na Kenya kuvunjika mwishoni mwa wiki kufuatia pande hizo mbili kushindwa kufikia muafaka kuhusu magari ya Tanzania yaliyopigwa marufuku uwanja wa Jomo Kenyatta. Huku pia mamlaka ya anga ya Tanzania na ile ya Kenya nazo zikishindwa kufikia muafaka kuhusu kupunguza safari za ndege za kenya zinazoingia Tanzania.
 Wabunge wa Afrika Mashariki wataka kuimarishwa kwa jumuiya yao

Wabunge wa Afrika Mashariki wataka kuimarishwa kwa jumuiya yao


Viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa  Kenya .
Viongozi wa nchi wanachama wa jumuiya ya Afrika Mashariki Paul Kagame wa Rwanda, Yoweri Museveni wa Uganda na Uhuru Kenyatta wa Kenya .
Bunge la Afrika Mashariki limeanza vikao vyake vya nne nchini Uganda na kuanza kwa  kuzitolea mwito  nchi zote wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki kutia bidii kwenye mchakato wa kuhakikisha kuwa wanaijenga na kuiboresha jumuiya. Bunge la Afrika mashariki   linafanya vikao vyake vya wiki moja nchini Uganda. 

Phillis Kandie Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri amesema kuwa mazungumzo ya kujadili upya muundo wa muungano wa kisiasa wa Afrika Mashariki na mpango wa utekelezaji utazingatiwa mwezi wa April mwaka huu.

Miongoni mwa mambo ambayo muungano wa jumuiya ya Afrika mashariki unaweza kujivunia ni pamoja na kuweko na forodha moja ambayo ilitekelezwa tarehe moja mwezi huu. Pia,  jumuiya iliweza  kutia saini itifaki ya kuanzisha sarafu moja ya jumuiya.

Phillis Kandie Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri na ambaye pia ni  waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki nchini Kenya ametoa mwito kwa wabunge wazishinikize serikali zao zihakikishe kuhakikisha kuwa kutekelezwa kwa itifaki ya sarafu moja kunaanza tarehe moja mwezi wa Julai mwaka huu kama viongozi wa jumuiya walivyokubaliana walipokutana mara ya mwisho mwezi wa novemba mwaka uliopita.

Wakati huo huo  Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Margaret Zziwa katika mkutano ya wanahabari alitangaza kwamba wataituma timu ya ukaguzi Sudan Kusini  kukagua kama nchi hiyo iko tayari kujiungana jumuiya. Hii ni baada ya Sudan Kusini kuwasilisha rasmi ombi  lao  la kutaka kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki.

 Timu hii itakuwa ikiangalia kama Sudan Kusini inatimiza misingi bora ya utawala kama vile demokrasia, utawala wa sheria, utunzaji wa haki za binadamu na haki za kijamii.

Waziri wa Mambo ya Afrika Mashariki  kutoka Kenya  Bi Kandie amewatakia heri raia wa Sudan Kusini na akasema kama majirani hawatawetekeleza haswa wakati huu wanapohitaji usaidizi.
 Wala Mbwa kutokana na Ukame Kenya

Wala Mbwa kutokana na Ukame Kenya


Kitoweo cha nyama ya Mbwa ni nadra sana Afrika Mashariki
Kisa cha kusikitisha kimeripotiwa kutokea katika jimbo la Turkana ambapo mwanamke mmoja mkongwe alilazimika kupikia familia yake nyama ya Mbwa kutokana na uhaba wa chakula unaokumba eneo hilo.
Hali mbaya ya ukame imesababisha uhaba wa chakula na kuwalazimu baadhi ya wakaazi ambao ni wafugaji wa kuhamahama kula nyama ya Mbwa.
Tukio hilo limeripotiwa katika eneo la Kakuma ambapo akina mama wawili walipatikana wakikaanga kitoweo cha nyama ya Mbwa.
Chifu wa eneo hilo Cosmus Nakaya amethibitishia BBC tukio hilo ambapo, wanawake wawili walikamatwa katika eneo hilo ambalo ni hifadhi kwa maelfu ya wakimbizi kutoka Somalia,wakikaanga kitoweo cha nyama hiyo tayari kuwalisha watoto.
Mama Akaran Aparo, mwenye umri wa miaka 73, aliambia maafisa kuwa alilazimika kupikia familia yake nyama hiyo kwani hakutaka kuiba Mbuzi au Kuku wa mtu kisha akamatwe na kufikishwa mahakamani.
Aidha Mama Aparo aliwaambia waandishi wa habari kwamba yeye hulazimika kusafiri umbali wa kilomita 3 kutafuta chakula katika kambi ya Kakuma ingawa hurejea na kidogo sana au wakati mwingine kukosa hata hicho kidogo.
Mama huyo alisema kuwa yeye hutegemea chakula cha msaada kwani anaishi na wajukuu wake watano ambao wazazi wao walifariki.
Anasema yeye hupokea chakula cha msaada lakini hajapokea chochote tangu mwezi Septemba mwaka jana.
Jimbo la Turkana ni kame sana ingawa hivi karibuni kumekuwa na habari njema kutoka katika jimbo hilo kwani visima vya mafuta vimepatikana pamoja na visima vya maji vilivyo chini ya ardhi.
Utajiri huu unatarajiwa kuboresha maisha ya wenyeji ingawa hadi mavuno yatakapoanza kupatikana ndipo faida zitakapoanza kudhihirika kwa wenyeji wa jimbo hilo.
Efforts to get the government to send food have been futile,” she said.
I didn’t want my grandchildren to keep suffering
She said that on her way to Kakuma, she spotted a dog which had made a shelter and given birth to five puppies. “I picked two for our meal as I didn’t want my grandchildren to keep suffering.”
Ms Aparo said she hit the puppies on the head and roasted them traditionally without removing the skin.
Her friend and age-mate, Ms Eregae, said she was too weak to go round begging for food from hotels.
“My friend called me and said she had prepared a meal which we shared,” she said.
Eyewitness Peter Lomiyana said he saw two roasted dogs in the house and called the police.
“They asked me why the police were arresting them for the roasted dogs in the house when they had already eaten two.” Said area District Officer Samuel Osodo while appealing for relief: “Vulnerable children and women urgently need relief aid.”
Na BBCSwahili
SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

SERIKALI YA TANZANIA KUENDELEA KUIMARISHA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

IMG_9491Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta (katikati) akifafanua kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Serikali ya Tanzania ilivyodhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi wanachama wa Jumuiya hiyo. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole na wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Msaidizi  Idara ya Habari Maelezo Bi Zamaradi Kawawa.
IMG_9566Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akisisitiza kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam kuhusu Tanzania itakavyonufaika na mfumo wa himaya moja ya forodha katika kuimarisha biashara kati ya nchi wanachama wa Jumuiya hiyo.
IMG_9572
aziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Samuel Sitta akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es salaam juu ya  Shirikika la ndege la Tanzania (ATCL) kupanua huduma zake na kufika Bujumbura nchini Burundi, ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama moja ya hatua za kuimarisha usafiri wa anga kati ya nchi wanachama. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Amantius Msole.
…………………………….
Na Frank Mvungi
Serikali ya Tanzania imedhamiria kuimarisha ushirikiano baina yake na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Nyanja za miundombinu.
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh. Samuel Sitta wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
Mh.Sitta alibainisha kuwa mwishoni mwa mwaka 2013 Mawaziri wa Tanzania, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) walikutana kujadili namna ya kuimarisha miundo mbinu ya barabara, reli, anga, anga na maji.
Mh.Sitta aliongeza kuwa katika kikao hicho ilikubaliwa kuwa Shirikika la ndege la Tanzania (ATCL) lipanue huduma zake na kufika Bujumbura nchini Burundi ambapo ATCL ilianza kufanya safari zake kati ya Tanzania na Burundi Desemba16, 2013 mara tatu kwa wiki kama hatua za awali za utekelezaji.
Mh. Sitta alisisitiza kuwa katika mkutano wa 8 wa Baraza la la Mawaziri la Jumuiya hiyo umeridhia mfumo wa himaya moja ya Forodha na mpangokazi unaoainisha masuala ya utekelezaji katika kipindi cha miezi sita ili kuwezesha kuanzishwa kwa himaya hiyo ifikapo Juni 2014.
Mh. Sitta akifafanua zaidi alisema mfumo wa himaya moja ya forodha unaainisha utaratibu wa mzunguko wa biashara, usimamizi wa mapato na mfumo wa kisheria.
Katika mfumo huo Sitta alisema kuwa ilikubalika kuwa nchi wanachama zitakusanya mapato yake ya kodi.
Aidha, kwa bidhaa zinazopitia nchi moja kuelekea nchi nyingine wanachama za Jumuiya hiyo zimekubaliana kuwa nchi husika itakusanya mapato yake na kuifahamisha mamlaka ya forodha mizigo ilipoingilia katika Jumuiya kwa kwa ajili ya kuruhusu bidhaa kuondoshwa.
Mkutano wa 15 wa Kawida wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya Afrika Mashariki Uliofanyika Jijini Kampala, Uganda Novemba 30, 2013 na kuamua masula muhimu ya maendeleo ya Mkutano wa Jumuiya Afrika Mashariki.
Baadhi ya masuala yaliyojadiliwa na kutolewa uamuzi ni pamoja na kutiwa saini kwa Itifaki ya Umoja wa Fedha, kuidhinishwa uundwaji wa Himaya ya Umoja wa Forodha (Single Customs Territory).
Na mapukio na vijana
 Museveni akataa kuidhinisha mswada tata

Museveni akataa kuidhinisha mswada tata


Moses raia wa Uganda anayeshiriki mapenzi ya jinsia moja akitafuta hifadhi nchini Marekani
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni amekataa kuidhinisha mswada ambao ikiwa utaidhinishwa utatoa adhabu kali kwa watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja.
Museveni amemuandikia spika wa bunge barua na kumkosoa kwa hatua ya kupitisha mswada huo Disemba mwaka jana bila ya kuwa na idadi ya kutosha ya wabunge.
Aidha Rais amesema kuwa Watu wanaoshiriki mapenzi ya jinsia moja ni watu wenye akili timamu na wanaweza kuokolewa kutokana na tabia hiyo.
Mswada huo unatoa adhabu kali kwa watu watakaopatikana na hatia ya kushiriki mapenzi ya jinsia moja ikiwemo kufungwa jela na pia ni uhalifu kwa mtu yeyote kukosa kuripoti visa vya mapenzi ya jinsia moja.
Mwandisi wa BBC mjini Kampala Cathrene Byaruhanga anasema kuwa mswada huo pia unapendekeza kuadhibiwa kwa watu wanaozungumzia maisha ya wapenzi wa jinsia moja bila ya kuwakashifu kwani wanaweza kufungwa jela.
Kwa mujibu wa gazeti la Monitor, Rais Museveni amesema kwamba mswada huo ulishinikizwa zaidi kupitishwa na wabunge licha ya kuwashauri kusubiri hadi serikali itakapoutathmini.
Rais anaelewa kwamba ikiwa atauidhinisha mswada huo na kuufanya sheria kutakua na ukosoaji mkubwa kutoka kote hali inatakayochangia baadhi ya nchi za kigeni kusitisha msaada kwa Uganda.
Na BBCSwahili
Jeshi la UG vitani na waasi S.Kusini

Jeshi la UG vitani na waasi S.Kusini

Mkutano wa kupatanisha makundi yanayozozana Sudan Kusini unaendelea nchini Ethiopia
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesema kuwa jeshi la Uganda linashirikiana na wanajeshi wa Sudan kupambana na waasi nchi Sudan Kusini.
Mapigano hayo ambayo yalizuka mwezi uliopita yanaendelea katika maeneo kadhaa ya Sudan kusini, licha ya kufufuliwa kwa mazungumzo ya amani katika nchi jirani ya Ethiopia.
Baada ya wiki kadhaa za tetesi za wanajeshi wa Uganda kuwa nchini Sudan Kusini, jeshi la Uganda sasa limekiri rasmi kuwa liko katika vita na waasi wa Sudan Kusini.
Kwa mujibu wa msemaji wa jeshi, Luteni Kanali Paddy Ankunda, Uganda ina takriban wanajeshi elfu moja na mia sita nchini humo.
Serikali ya Uganda imekiri kukabiliana na waasi hao tangu mwanzoni mwa wiki hii,wakati wanajeshi hao waliposhambuliwa na waasi wanaoongozwa na makamu wa zamani wa Rais Riek Machar.
Akisimulia kuhusu tukio hilo kwenye mkutano wa kikanda nchini Angola mnamo Jumatano, Rais Yoweri Museveni, alisema kwamba baadhi ya wanajeshi wake waliuawa au kujeruhiwa.
Jeshi la Uganda hata hivyo halijaeleza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa.
Luteni Kanali Paddy Ankunda ametetea hatua ya Uganda kupeleka wanajeshi wake Sudan Kusini ikisema lengo lake ni kulinda raia na kufungua njia kwa misaada kuingizwa nchini humo .
Na BBCSwahili
Uganda yakiri kulisaidia jeshi la Sudan Kusini vitani

Uganda yakiri kulisaidia jeshi la Sudan Kusini vitani

Jeshi  la  Uganda  limesema  kuwa  majeshi  yake yamejiunga  na  jeshi  la  serikali  ya  Sudan  kusini  katika vita  dhidi  ya  uasi  kwenye taifa  hilo  changa  duniani.
Msemaji  wa  jeshi  la  Uganda  luteni  kanali Paddy Ankunda  amesema  leo kuwa  majeshi  ya  uganda yanasaidiana na vikosi vya serikali ya Juba  kuwaondoa waasi  katika  mji  wa  Bor, mji  muhimu  karibu  na  mji mkuu juba ambao  umeshuhudia  mapigano  makali  tangu kuanza  kwa  mzozo  huo  katikati  ya  mwezi  uliopita nchini  Sudan  kusini. 
Maafisa  wa  Uganda  wamekuwa wakikana   kuwa  majeshi  ya  nchi  hiyo  yamejiunga  na mapigano, wakisema  majeshi  ya  Uganda  wamewekwa Sudan  kusini  kwa  ajili  ya  kufanikisha  zoezi  la kuwaondoa  raia.
Rais Yoweri  Museveni  wa  Uganda  amesema  jana  kuwa wanajeshi  wa  Uganda  wameuwawa  katika  mapigano nchini  Sudan  kusini. 
Akizungumza  katika  mkutano  mjini Angola  jana, Museveni  amesema  majeshi  ya  nchi  yake yamekuwa  yakipigana  kulisaidia  jeshi  la  serikali nchini Sudan  kusini.
Nao  wabunge  wa  Marekani  wameeleza  kufadhaishwa kwao  jana kuhusiana  na  wimbi  la  ghasia   nchini  Sudan kusini ,na kuwekea alama ya kuuliza hatua ya  marekani kuendelea  kutuma  mamilioni  ya  dola  kuisaidia  nchi hiyo.
na DW.DESwahili
Msani wa Kenya ang'ara Hollywood

Msani wa Kenya ang'ara Hollywood

kutoka kushoto Lupita Nyong'o, Chiwetel Ejiofor, Steve McQueen, Sarah Paulson, na Michael Fassbender katika picha kwenye tuzo za Golden Globe.
Kutoka kushoto Lupita Nyong'o, Chiwetel Ejiofor, Steve McQueen, Sarah Paulson, na Michael Fassbender katika picha kwenye tuzo za Golden Globe.

Mcheza sinema Lupita Nyong’o kutoka Kenya alikuwa mmoja wa wanawake waliong’ara katika sherehe za tuzo za Golden Globe kwa wacheza sinema huko Hollywood, California. Lupita alishiriki katika sinema ya “12 Years a Slave” ambayo ilikuwa moja ya sinema zilizojizolea tuzo nyingi katika sherehe za Jumapili usiku, ikiwa ni pamoja na sinema bora katika aina ya drama.

Lupita ambaye alianza kujulikana zaidi Afrika katika mfululizo wa tamthiliya ya MTV Shuga, Kenya, alicheza kama msichana mtumwa katika sinema ya “12 Years a Slave.”

Jumapili alitokeza akiwa amevalia gauni refu jekundu na kutajwa kama miongoni mwa wanawake waliopendeza sana katika sherehe hizo.

Sinema ya “ 12 Years a Slave” iliyoongozwa na mkurugenzi Steve McQueen inaelezea jinsi mwanaume mmoja mweusi alivyotekwa na kuuzwa kama mtumwa kabla ya vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Marekani.

Pia mtengenezaji wa filamu kutoka Mexico, Alfonso Cuaron alitajwa kama mwongozaji mahiri katika utengenezaji wa sinema za drama.

Wengine waliotamba katika tuzo za Golden Globe ni pamoja na mcheza sinema Mathew McConaughey aliyepata tuzo yake kwa kuwa muigizaji bora katika mitindo ya drama za hisia kwenye filamu ya “Dallas Buyers Club” na Leonardo DiCaprio alipata tuzo bora akijulikana sana katika drama kwenye muziki au uchekeshaji, filamu iliyompa chati ni “ The Wolf of Wall Street”.

Tuzo za Golden Globe ni mfululizo wa kipindi cha tuzo za Hollywood ambazo kilele chake kitakuwa tuzo maarufu zinazojulikana sana kama Oscars Machi  mbili. 

Na VOASwahili. 
 Kesi ya ugaidi ya Westgate yaanza Kenya

Kesi ya ugaidi ya Westgate yaanza Kenya


Washukiwa wa ugaidi walioshitakiwa kuhusiana na shambulizi la Westgate
Kesi ya washukiwa wanne wa shambulizi la kigaidi la Westgate lililofanyika nchini Kenya mwaka jana, imeanza rasmi nchini humo.
Mashahidi wa wawili wa kwanza walifika mahakamani kabla ya kesi kuahirishwa hadi Alhamisi.
Washukiwa hao wanne wameshitakiwa kwa kusaidia magaidi waliofanya shambulizi hilo ambapo watu 67 waliuawa na wengine 200 kujeruhiwa.
Wamekanusha mashitaka.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu al-Shabab lilikiri kufanya shambulizi hilo.
Maafisa wakuu nchini Kenya wanaamini kuwa washambuliaji wote wanne walifariki wakiwa ndani ya jengo hilo.
na BBCSwahili
 ICC: Ahueni kwa William Ruto

ICC: Ahueni kwa William Ruto


Naibu Rais Ruto amepata ahueni ya kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi yake
Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita, ICC, imemruhusu Naibu Rais wa Kenya William Ruto kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi dhidi yake katika mahakama hiyo.
Ruto alishitakiwa kwa kosa la uhalifu dhidi ya binadamu baada ya kusemekana kuwa baadhi ya washukiwa wakuu wa ghasia za baada ya uchaguzi zilizokumba Kenya mwaka 2007/08.

Jaji mkuu katika kesi yake hata hivyo amesema kuwa sharti Ruto ahudhurie vikao muhimu wakati kesi yake ikiendelea, ikiwemo nyakati mashahidi wanapotoa ushahidi.
Ruto amekanusha madai ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na 2008.
Takriban watu 1,200 waliuawa katika ghasia hizo za kikabila na wengine laki sita kuachwa bila makao.
Mwaka jana mahakama hiyo pia ilimruhusu Rais Uhuru Kenyatta kutohudhuria vikao vyote vya kesi yake.
Kenyatta na Ruto walishitakiwa kama washukiwa wakuu wa ghasia zilizozuka baada ya kuibuka utata kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu wakati huo kati ya Rais mstaafu Mwai Kibaki na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga.
Na BBCSwahili
Dhahabu' nyeusi yazizima Kenya

Dhahabu' nyeusi yazizima Kenya


Kupatikana kwa mafuta Kenya kunaimarisha matumaini ya uchumi kunawiri
Kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow imetangaza kupata visima vipya vya mafuta katika jimbo la Turkana, Kaskazini mwa Kenya na kuinua matumaini ya uchumi wa Kenya kuimarika zaidi.
Kampuni hiyo ya Uingereza ambayo huendesha shughuli zake nyingi Afrika, imesema kuwa visima vyote vya mafuta vilivyogunduliwa katika eneo hilo lote tangu mwaka jana, vina uwezo wa kuzalisha mapipa milioni 600 .
Lakini imeongeza kuwa inaamini uwezo wa visima hivyo ambao utatathminiwa zaidi katika miaka miwili ijayo, unaweza kuwa zaidi ya mapipa bilioni moja.
Ugunduzi huu unafikisha saba visima vya mafuta vilivyogunduliwa na kampuni ya Tullow Kaskazini mwa Kenya.
Tullow inasema kuwa imekubaliana na serikali ya Kenya kuanza utafiti zaidi na kuona njia za kuweza kutengeza mabomba ya kusafirisha nje mafuta hayo.
Serikali ya Kenya inatarajia kuwa ifikapo mwaka 2015/16 itaanza rasmi kuuza mafuta yake.
Uganda na Kenya zimetangaza kufanya miradi ya pamoja ya kuwa na bomba la mafuta kuelekea bahari hindi.
Kampuni ya Tullow ilikuja kujulikana wakati ilipogundua mafuta nchini Ghana na Uganda.
Ugunduzi wa mafuta katika jimbo la Turkana umewachangamsha watu wengi nchini Kenya, lakini hata ikiwa mafuta hayo yatakuwa na thamani bado changamoto nyingi zinaisubiri Kenya.
Na BBCSwahili
KAGAME: ITAKULA SAHANI MOJA NA WANAO HATARISHA AMANI YANGU

KAGAME: ITAKULA SAHANI MOJA NA WANAO HATARISHA AMANI YANGU

Rais wa Rwanda alipokuwa akipiga kura.
Rais wa Rwanda alipokuwa akipiga kura.

Rais Paul Kagame wa Rwanda ameonya wale wote wanaokula njama za kuhatarisha serikali yake na taifa kwa ujumla yatawageuka wenyewe kabla ya kufikia azma yao. Kauli ya Rais Paul Kagame imekuja huku kukiendelea shutuma kutoka kwa wapinzani kwamba serikali yake ikawa ilihusika na mauaji ya mkuu wa zamani wa ujasusi nchini Rwanda Kanali Patrick Karegeya aliyeuwawa  nchini Afrika Kusini. Serikali ya Rwanda ilikanusha madai hayo.

Rais Kagame alitoa kauli hiyo mjini Kigali kwenye kongamano la viongozi wa serikali na madhehebu mbalimbali katika maombi ya kuliombea taifa na kumshukuru Mungu kwa mwaka uliopita. Rais Kagame ambaye alikuwa mzungumzaji wa mwisho kwenye kongamano hilo la siku moja amesema kamwe hatakuwa salama mtu yeyote atakayethubutu kuisaliti Rwanda kwa lengo la kuangamiza maisha ya wanyarwanda wasio na hatia kwa maslahi binafsi.

Amesema nchi hiyo imetoka kwenye dimbwi la mauaji na mateso ya kila aina na kujijenga kufikia hatua ilikofikia leo, huku akiongeza yeyote mwenye dhamira ya kubomoa mafanikio hayo yatamgeuka mwenyewe kabla ya kufikia azma yake.
Alisema “Huwezi kulisaliti taifa na ukadhani utakaa salama,yeyote atakayejaribu atakabiliwa na nguvu tulizopewa na Mungu kuilinda nchi yetu.Yeyote atakayejaribu atakiona hata wale ambao bado wako hai wasubiri - ni suala tu la muda”.

Bila kutaja majina Rais Kagame amesema viongozi wa Rwanda wamekuwa wakitumia muda wao kukanusha shutuma dhidi ya Rwanda kuhusu kifo cha mtu fulani akasema hata kama Rwanda haijahusika lakini kwa nini watu hao waachwe ili waendelee na hujuma zao dhidi ya wananchi wasio na hatia? Na wengi ni wale aliowataja kama waliosahau kilicho watoa utumwani na sasa wanaigeukia nchi yao.
 
Kagame aliongeza na kusema  "wale wanaosahau kilichowatoa utumwani, ni lazima wakabiliwe na athari ikiwa ni pamoja na hao mnaowasema, wamesahau wameshiba na kuvimbiwa kisha kusahau kilichowapa umaarufu huo, lakini kumbe wakasahau kwamba nchi yao Rwanda na Mungu aliyewaumba viko juu zaidi yao."

Rais Kagame ametoa tamko hili huku kukiendelea wimbi la lawama kupitia vyombo vya habari kwamba serikali ilikuwa na mkono kwenye mauaji ya mkuu wa zamani wa ujasusi nchini Rwanda Kanali Patrick Karegeya. Rais na serikali ya Rwanda imekuwa ikikanusha vikali kuhusika na mauaji hayo. Hata hivyo katika  kuonyesha ukali wa shutuma zake dhidi ya wapinzani alitoa mfano.
 
Akisema "watu wanaokuja hapa na kurusha mabomu na kuua watoto wadogo wasio na hatia, polisi walioko wanafahamu vipande vya miili ya watu wanavyookota baada kuuawa na mabomu kisha uniambie niombe radhi?kamwe ."

Hii imekuwa mara ya kwanza kwa Rais Paul Kagame kutoa matamshi makali baada ya kuwepo na shutuma dhidi ya serikali kuhusu masaibu yanayowakabili wapinzani wa serikali katika nchi za kigeni.
 
Na Voaswahili.
KENYA YAIUNGA MKONO TZ A.MASHARIKI

KENYA YAIUNGA MKONO TZ A.MASHARIKI



Amina Mohamed,waziri wa mambo ya nje wa Kenya

Kenya imekuwa nchi ya kwanza kutoka Jumuia ya Afrika Mashariki kuipongeza Tanzania kwa hatua yake ya kutangaza bayana kwamba haiko tayari kutoka katika jumuiya hiyo kama ilivyodhaniwa.
Wasiwasi kuwa Tanzania ingejitoa kutoka jumuia ya Afrika Mashariki ulitokana na hali iliyojitokeza kwa baadhi ya nchi za jumuia hiyo kuendesha mikutano yao bila kuishirikisha Tanzania na Burundi.
Baadhi ya wanasiasa na wananchi nchini Tanzania walitaka nchi yao iachane na jumuia hiyo wakizishutumu Kenya, Rwanda na Uganda kuitenga Tanzania hata katika mikutano ya masuala yaliyohitaji maamuzi ya jumuia.
Kufuatia mfarakano huo, ulionekana kutishia uhai wa Jumuia ya Afrika Mashariki, Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania, wiki hii alilihutubia bunge la Muungano wa Tanzania mjini Dodoma, katikati ya nchi na kutangaza bayana kuwa Tanzania haitatoka katika jumuiya ya Afrika Mashariki, kwani imefanya kazi kubwa kuifufua na kuiunda upya baada ya kusambaratika mwaka 1977.
Kwa upande wake, Kenya moja ya nchi waanzilishi wa Jumuia ya Afrika Mashariki na ambayo ilishutumiwa kushiriki kuibagua Tanzania, imemtuma waziri wake wa mambo ya nje, Amina Mohammed kwenda Tanzania na kuwa na mazungumzo na waziri mwenzie wa mambo ya nje Bernard Membe kuhusu mfarakano huo na nia ya kuimarisha zaidi uhusiano wa nchi mbili hizo.
Katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Jumapili, waziri Amina Mohammed, amesema Kenya inaunga mkono hotuba ya Rais Jakaya Kikwete, kuhusu uamuzi wake wa kutojitoa katika Jumuia ya Afrika Mashariki, huku akisisitiza kuwa bila Tanzania hakuna Afrika Mashariki na bila Afrika Mashariki hakuna Tanzania.
"Kama unavyojua Kenya na Tanzania tumekuwa tukiijenga jumuiya ya Afrika Mashariki kwa muda mrefu sana, tuko na mafanikio mengi sana, kuna mambo mengi tumeyafanya, kuna njia ndefu imebakia kuna mambo mengi yasiyoweza kupimwa kati ya nchi hizi. Na tuna tumaini kwamba tutaendelea kuijenga Afrika Mashriki kwa nguvu zote na tutawasiliana na watu wetu kwa sababu tunataka watu wetu waishi vema na wawe majirani wazuri na waendelee . Kwa Tunataka uchumi wetu uende vizuri. Kwa hiyo tutaendelea kushirikiana, sisi ni wale wa kwanza tuliokuwa pale kwa hiyo tunataka tufanye kile tunachoweza kuendeleza Afrika Mashariki..... Lakini tumefurahia sana sana hotuba ya Rais aliyotoa pale bungeni na tunawashukuru pia Watanzania kumuunga mkono."

Uhusiano wa Kenya na Tanzania ni wa kindugu

Pia waziri Amina amesisitiza kuwa hakuna namna ambavyo Tanzania na Kenya zitatenganishwa, kwa namna ambavyo zimejenga maingiliano makubwa ya kijamii na kiuchumi, huku akiomba Tanzania kusaidia kusukuma ombi la Kenya la kutaka kesi ianyomkabili Rais wake, Uhuru Kenyatta iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi ili kumpa fursa ya kutekeleza majukumu yake ya kitaifa.

Benard Membe,waziri wa mambo ya nje wa Tanzania
Kwa upande wake waziri wa mambo ya nje wa Tanzania, Benard Membe amesema serikali yake imefurahi kuona Kenya imekuwa nchi ya kwanza kuipongeza Tanzania kwa kuinusuru jumuia ya Afrika Mashariki kama ilivyokuwa mwanzoni na kujenga jumuiya ya watu na si ya viongozi, na kuahidi kushirikiana na Kenya katika masuala mbalimbali likiwemo la kutaka kesi inayomkabili Rais Uhuru Kenyatta katika mahakama ya ICC iahirishwe kwa mwaka mmoja zaidi.
Waziri Membe amesema waziri mwenzake Amina kutoka Kenya amesema hotuba ya Rais Kikwete imewazindua kwani hawakujua kuwa baadhi ya yale waliyokuwa wakiyafanya yalikuwa ni kukiuka taratibu za Jumuia ya Afrika Mashariki na kuahidi kuwa Kenya itashirikiana kikamilifu na nchi waanzilishi halisi wa Jumuia ya Afrika Mashariki.
Katika kuonyesha nia thabiti ya kutotoka katika Jumuia ya Afrika Mashariki, Rais Kikwete katika hotuba yake aliyoitoa bungeni, alisema "Tanzania ni mwanachama mvumilivu, mtiifu na mwaminifu na tunatimiza wajibu wetu kwa jumuia na kuhusika kikamilifu katika ujenzi wake."alisema.
Rais Kikwete alitumia muda mrefu katika hotuba hiyo kuchambua masuala mbalimbali ya msingi ya uhai wa jumuia hiyo huku akisema ameshangazwa na nchi za Kenya, Uganda na Rwanda kuzitenga Tanzania na Burundi.

Kategori

Kategori