Kesi ya ugaidi ya Westgate yaanza Kenya


Washukiwa wa ugaidi walioshitakiwa kuhusiana na shambulizi la Westgate
Kesi ya washukiwa wanne wa shambulizi la kigaidi la Westgate lililofanyika nchini Kenya mwaka jana, imeanza rasmi nchini humo.
Mashahidi wa wawili wa kwanza walifika mahakamani kabla ya kesi kuahirishwa hadi Alhamisi.
Washukiwa hao wanne wameshitakiwa kwa kusaidia magaidi waliofanya shambulizi hilo ambapo watu 67 waliuawa na wengine 200 kujeruhiwa.
Wamekanusha mashitaka.
Kundi la wapiganaji wa kiisilamu al-Shabab lilikiri kufanya shambulizi hilo.
Maafisa wakuu nchini Kenya wanaamini kuwa washambuliaji wote wanne walifariki wakiwa ndani ya jengo hilo.
na BBCSwahili