Mahakama ya kimataifa ya uhalifu
wa kivita, ICC, imemruhusu Naibu Rais wa Kenya William Ruto
kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi dhidi yake katika mahakama hiyo.
Ruto alishitakiwa kwa kosa la uhalifu dhidi ya
binadamu baada ya kusemekana kuwa baadhi ya washukiwa wakuu wa ghasia za
baada ya uchaguzi zilizokumba Kenya mwaka 2007/08.Ruto amekanusha madai ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi wa mwaka 2007 na 2008.
Takriban watu 1,200 waliuawa katika ghasia hizo za kikabila na wengine laki sita kuachwa bila makao.
Mwaka jana mahakama hiyo pia ilimruhusu Rais Uhuru Kenyatta kutohudhuria vikao vyote vya kesi yake.
Kenyatta na Ruto walishitakiwa kama washukiwa wakuu wa ghasia zilizozuka baada ya kuibuka utata kuhusu matokeo ya uchaguzi mkuu wakati huo kati ya Rais mstaafu Mwai Kibaki na aliyekuwa waziri mkuu Raila Odinga.
Na BBCSwahili