Showing posts with label Afrika ya Kati. Show all posts
Showing posts with label Afrika ya Kati. Show all posts
Umoja wa Ulaya kutuma kikosi CAR

Umoja wa Ulaya kutuma kikosi CAR

Umoja wa Ulaya umekubali kutuma wanajeshi 500 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati katika juhudi za kusaidia kurejesha amani.
Uamuzi huo ulipitishwa baada ya wabunge katika jamhuri hiyo kumchagua meya wa mji mkuu, Bangui, Catherine Samba Pinza kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa na Michel Djotodia, kamanda wa wanamgambo wa Seleka aliyejiuzulu mwezi huu.
Mgogoro ulianza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya wanamgambo wa kiislamu kuchukua hatamu za uongozi wa nchi.
Ujumbe wa Umoja wa Ulaya utaungana na wanajeshi 1,600 wa Ufaransa na wengine wapatao 4000 kutoka mataifa ya kiafrika ambao tayari wamewasili nchini humo. 
Mkuu wa Sera wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amesema wanajeshi wao watafanya kazi katika mji mkuu Bangui kwa muda wa hadi miezi sita, wakisaidia  kulinda usalama wa watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.
CAR yapata Rais mpya wa mpito

CAR yapata Rais mpya wa mpito

Mamia walisherehekea wakati bwana Djotodia alipoondoka madarakani
Wabunge katika Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamemchagua Meya wa mji mkuu Bangui, Catherine Samba-Panza, kama Kaimu Rais .
Samba-Panza, ndie mwanamke wa kwanza kuwahi kushikili wadhifa huo.
Wagombea wanane waliwania wadhifa huo ambao ulikuwa unashikiliwa na Michael Djotodia, aliyeng'atuka mapema mwezi huu kufuatia shinikizo kutoka kwa viongozi wa mataifa jirani.
Panza alimpiku mshindani wake wa karibu Desire Kolingba katika duru ya pili ya kura hiyo.
Wakati huohuo mawaziri wa mambo ya nje wa Muungano wa Ulaya wamekubaliana kukutana Jumatatu kupeleka wanajeshi zaidi nchini CAR.
Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa takriban watu hamsini wameuawa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo mwishoni mwa wiki.
Mapigano yalianza wakati Djotodia alipochukua mamlaka mwaka jana kwa njia ya mapinduzi akiungwa mkono na waasi wa kiisilamu katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya waumini wa kikristo.
Waisilamu wawili waliteketezwa katika mji mkuu Bangui siku ya Jumapili.
Karibu watu milioni moja wameachwa bila makao kutokana na mgogoro huo.
Na BBCSwahili
UN yaonya juu ya mauaji ya halaiki CAR

UN yaonya juu ya mauaji ya halaiki CAR

Umoja wa Mataifa umeonya juu ya hatari ya kutokea mauaji ya halaiki katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Taifa hilo lilitumbukia katika vurugu za kidini baada ya waasi wa Seleka kuchukuwa madaraka mnamo mwezi wa Machi mwaka 2013.
 la mauaji na uporaji katika Jamhuri hiyo lilisababisha mapigano kati ya Waislamu na wanamgambo wa Kikristu. 
Zaidi ya watu milioni moja wamegeuzwa wakimbizi na mapigano hayo, na imeripotiwa kuwa zaidi ya alfu moja waliuawa katika mji mkuu Bangui pekee yake mwezi uliopita.
Afisa mwandamizi anaeshughulikia masuala ya kiutu katika Umoja wa Mataifa, John Ging, ambaye amerejea hivi karibuni kutoka Jamhuri ya Afrika ya Kati, amesema, hali inayoendelea huko ina dalili zote za mauji ya halaiki, kama zilizoshuhudiwa nchini Rwanda na Bosnia. 
Kumekuwepo taarifa za ukosefu wa usalama tangu rais Michel Djotodia alipojiuzulu wiki iliyopita.
Na Dw.DeSwahili
Rais wa mpito wa CAR ajiuzulu

Rais wa mpito wa CAR ajiuzulu


 10A
Maelfu ya watu wamekimbia makwao kutokana na vurugu za kidini
Rais wa mpito wa Jamuhuri ya Afrika ya Kati, Michel Djotodia, amejiuzulu kufuatia shinikizo kali na kukosolewa kwa mwendo wake wa kujikokota katika kusuluhisha mgogoro wa kidini unaotokota nchini humo.
Hatma ya Djotodia ilikuwa swala kuu katika ajenda ya mkutano wa viongozi wa kikanda kuhusu mzozo unaoendelea nchini humo.
Mkutano huo ulifanyika nchini Chad huku maelfu wakiendelea kutoroka nchini humo kutokana na ghasia.
Maelfu ya watu waliandamana leo katika barabara za mji mkuu Bangui kumtaka Rais Djotodia, ajiuzulu.
Rais Djotodia amekosolewa vikali kwa kukosa kumaliza mapigano ya kidini kati ya wakristo na waliokuwa waasi waisilamu ambao walimsaidia kuingia mamlakani kwa njia ya mapinduzi mwaka jana.
Baraza lote la mpito katika Jamuhuri ya Afrika ya kati limekwenda nchini Chad ambako viongozi wa Afrika wanakutana kujadili mzozo unaoendelea nchini humo.
Mkutano huo wa viongozi wa kikanda, uliahirishwa, mapema asubuhi Ijumaa.
Lakini wajumbe kwenye mkutano huo wanasema walitakiwa kuendelea na mkutano usiku kucha ili kubuni mkakati kuhusu mustakabali wa Djotodia.
Viongozi wa kikanda wanasema wajumbe mia moja na thelathini na watano waliitwa kwa mkutano huo kwa sababu ni raia wa nchi hiyo pekee wanaoweza kuamua hatma ya taifa lao.
Ghasia baina ya wanamgambo wa kiisilamu na kikristo zimesababisha maelfu ya watu kuyahama makazi yao.
Djotodia aliingia mamlakani baada ya mapinduzi ya kijeshi mwezi Machi mwaka jana hali iliyotumbukiza taifa hilo katika viya vya wenyewe kwa kwenyewe.
Maelefu waandamana Bangui kupinga vikosi ya usalama

Maelefu waandamana Bangui kupinga vikosi ya usalama


Maelfu ya waandamanaji wameendelea kuandamana mjini Bangui, huku vikosi vya Usalama vya Umoja wa Afrika vikiripotiwa kuwafyatulia risasi, na kusababisha kifo na kujeruhiwa.
Waandamanaji wapinga vikosi vya usalama. Waandamanaji wapinga vikosi vya usalama.
Waandamanaji hao walikusanyika katika geti la kuingilia uwanja wa ndege katika mji mkuu, Bangui, wakishinikiza kuondoka madarakani kwa rais wa serikali ya mpito inayoongozwa na Michel Djotodia, pia wakipinga kuendelea kuwepo kwa vikosi vya kulinda usalama vya Umoja wa Afrika.
Waandamanaji hao wa kikristu wanashinikiza kuondolewa kwa vikosi vya usalama kutoka Chad na kuwaacha askari wa Kifaransa, ambao wamekuwa wakifanya juhudi za kurejesha amani nchini humo.
Wanapinga utawala wa rais Michel Djotodia, rais wa kwanza wa kiislamu kuongoza taifa hilo, lenye idadi kubwa ya wakristu na hivyo kusababisha kuendelea kwa mapigano baina ya raia na waasi.
Wakati magari mawili ya vikosi vya usalama vya Umoja wa Afrika kutoka Chad yaliposogea karibu na eneo la waandamanaji hao hii leo , muda mfupi baadaye waandamanaji hao walianza kurusha mawe upande yalipoelekea magari hayo ndipo wanajeshi hao walipofyatua risasi za kutuliza ghasia na kujeruhi watu kadhaa na mtu mmoja kuuawa.
Askari wa Kifaransa watuliza ghasia
Mmoja auwa na wengine kadhaa kujeruhiwa. Mmoja auwa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Hata hivyo vikosi vya usalama kutoka Ufaransa viliingilia kati kuzima ghasia hizo na kuanza kuwaokoa majeruhi.
Pia maelfu wa waandamanaji wa kiislamu wanaounga mkono kundi la waasi la Seleka waliandamana jana katika mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Bangui.
Waandamanaji hao walipiga kelele wakidai kuwa rais Francois Hollande wa Ufaransa ni mtuhumiwa na kuvilalamikia vikosi vyake vya kulinda usalama kuwa vinaegemea zaidi kuwalinda wakristu.
Raia wengi wa Bangui wanailaumu Chad ambayo rais wake Idriss Deby Itno amekuwa anacheza karata ya nani aongoze Jamhuri ya Afrika ya kati na muasisi wa kikundi cha waasi cha Seleka.
Chad ni sehemu ya vikosi vya uslama vya kulinda amani Jamhuri ya Afrika ya kati ya wanajeshi 3,700 kutoka vikosi kutoka nchi za Afrika wanaolinda usalama.
Jumuiya za kimataifa zaonya
Jamahuri ya Afrika ya kati inakabiliwa na miezi ya mapigano, vitendo vya ubakaji na vurugu mbali mbali, jambo ambalo jumuiya za kimataifa zimetoa onyo juu ya kuendelea kuvunjika kwa haki za binaanadamu dhidi ya raia.
Mbali ya Ufaransa kupeleka askari 1,600 wa Kifaransa chini ya idhini ya Umoja wa Mataifa mapema mwezi huu kulisaidia kurejesha amani kwenye mji mkuu wa nchi hiyo, Bangui, ingawaje bado mashambulizi ya kulipiziana kisasi yanaendelea.
Askari wa Kifaransa wapingwa na waislamu wanaounga mkono waasi wa Seleka. Askari wa Kifaransa wapingwa na waislamu wanaounga mkono waasi wa Seleka.
Askari wa Kifaransa wanaungwa mkono na wakristu huku wakionekana kutofautiana na wasilamu wanaounga mkono waasi wa selekea, ambao maelefu waliandamana jana mjini Bangui kuwapinga askari hao na kusababisha mapigano yaliyopelekea kuuawa kwa waasi watatu wa kundi la Seleka.
Djotodia, aliwekwa kama rais wa muda chini ya mkataba maalumu ulioafikiwa na mataifa ya Afrika lakini kwa sasa anaonekana kuzidiwa nguvu na kushindwa kwake kuzuia umwagikaji damu ambao unaendelea.
Na dw.deswahili
Hali Inatisha Katika Jamhuri ya Afrika Kati

Hali Inatisha Katika Jamhuri ya Afrika Kati

Ufaransa imeelezea msimamo wake wa kutoelemea upande wowote katika mzozo wa Jamhuri ya Afrika kati,msimamo ambao wataalam wanahisi ni shida kuutekeleza katika wakati ambapo mshirika wake wa karibu Chad,haiufuati.
Maandamano ya wafuasi wa opereshini ya Ufaransa Sangaris katika Jamhuri ya Afrika kati
Mjini Bangui,wanajeshi wa Tchad wanaotumikia kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika wamewafyetulia risasi waandamanaji waliokuwa wakiwataka warejee makeao kwa tuhuma za kuwa karibu zaidi na waasi wa Seleka walionyakua madaraka mwezi Machi mwaka huu nchini humo.Mwanaharakati mmoja ameuwawa.
Serikali ya Chad imekanusha kuhusika na mashambulio hayo.
Mashambulio yameripotiwa pia kati ya wanajeshi wa Chad na wale wa Burundi wanaotumikia kikosi cha MISCA. Wanajeshi wa Chad wanasemekana waliwarushia guruneti wanajeshi wa Burundi walipokuwa wakiwapokonya silaha waasi wa zamani wa Seleka.
"Wanajeshi wa Chad wameondoka pamoja na waasi wote sita wa Seleka na kuanza kufyetua risasi kila upande,wamerejea baadae na kuanza kushambulia vituo vyetu" mkuu wa kikosi cha Burundi Luteni kanali Pontien Hakizimana amesema.
Ufaransa Yasema Haielemei Upande Wowote
Wanajeshi wa Ufaransa wanapiga doria mjini Bangui
Duru za kijeshi zinasema uhusiano kati ya wanajeshi wa Chad na wale wa Burundi katika kikosi cha MISCA,umezorota tangu wanajeshi wa Chad walipowekwa nje ya mji mkuu na wanajeshi wa Burundi kupewa jukumu la kulinda amani mjini Bangui.
Ikionyesha hamu ya kutaka kuendelea kuwa na mshirika wake katika eneo hilo,anayewasaidia pia katika vita dhidi ya ugaidi nchini Mali,Ufaransa imeelezea umuhimu wa kujulikana ukweli kuhusu kuuliwa mwanaharakati huyo.Ufaransa imeelezea pia "imani yake kamili kwa rais Idriss Deby wa Chad,mshirika mkubwa aliyetuma wanajeshi 850 katika kikosi cha kulinda amani cha MISCA katika Jamhuri ya Afrika kati.
Katika wakati ambapo wanajeshi wa Ufaransa wanalaumiwa na waandamanaji wanaowaunga mkono Seleka kufanya mapendeleo rais Francois Hollande amesisitiza kuhusu misingi ya kutoelemea upande wowote wanajeshi wa Ufaransa.
Maandamano dhidi ya Opereshini Sangaris
Ahmed Adam akisimama mbele ya msikiti mjini Bangui
Licha ya ahadi hizo maandamano yameripoitiwa tena dhidi ya opereshini za wanajeshi wa Ufaransa Sangaris katika Jamhuri ya Afrika Kati.
"Tunapinga ukoloni wa Ufaransa,hatuitaki Ufaransa na hatuitaki opereshini Sangaris" ni miongoni mwa madai ya waandamanaji huku wengine wakisema "hawataki vita vya kidini katika nchi yao."
Na dw.deswahili
Wananchi wa Afrika ya Kati hatarini

Wananchi wa Afrika ya Kati hatarini


Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa yuko Jamhuri ya Afrika ya Kati katika juhudi za kukomesha mkondo wa umwagaji damu ambapo mamia ya watu wameuwawa na asilimia 10ya wananchi wamepotezewa makaazi yao.
Watu waliopotezewa makaazi Jamhuri ya Afrika ya Kati. Watu waliopotezewa makaazi Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Balozi huyo wa Marekani kwa Umoja wa Mataifa Samantha Powers amesema wakati wa mkesha wa ziara yake hiyo kwamba yeye na Rais Barack Obama wa Marekani wana wasi wasi mkubwa na mauaji yanayofanywa na makundi ya wanamgambo yanayohasimiana tokea serikali ya nchi hiyo ilipopinduliwa hapo mwezi wa Machi. Amewaambia waandishi wa habari kwamba ghasia hizo zimekuwa za kikatili na kimsingi zimeelekezwa dhidi ya raia na kuzidi kuwa za madhehebu ambapo kunahitajika hatua ya dharura kuokowa maisha.
Akitahadharisha dhidi ya kulinganisha Jamhuri ya Afrika ya Kati na maafa mengine ya nchi za Kiafrika mfano Somalia na Rwanda amesema wananchi wa Afrika ya Kati wako hatarini.Katika ziara hiyo Powers atakutana na viongozi wa kidini na wa kijamii pamoja na Rais Michel Djotodia.
Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power. Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Samantha Power.
Mataifa ya Ulaya yametowa msaada kusaidia kukomesha umwagaji damu huo wakati juhudi za Ufaransa za kuwapokonya silaha wapiganaji zikionekana kuzaa matunda kufuatia umwagaji damu huo uliozuka mapema mwezi huu.
Mvutano umepunguwa
Generali Francisco Soriano ambaye anaongoza vikosi vya Ufaransa nchini humo amesema hali ya mvutano imepunguwa sana na kumekuwa na utulivu katika mji mkuu wa Bangui tokea Ijumaa isipokuwa hawezi kusema iwapo hali hiyo itaendelea kudumu au la.
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binaadamu la Amnesty International limesema leo hii katika repoti kwamba wapiganaji wa Kiislamu katika mji mkuu wa Bangui wamewauwa takriban watu 1,000 katika kipindi cha siku mbili kulipiza kisasi kwa mauaji yaliofanywa na makundi ya vijana wa kujitolea wa Kikristo kwa wanaume 60 wa Kiislamu hapo Disemba tano.
Mauaji ya kisasi
Vikosi vya Ufaransa vikipiga doria Bangui. Vikosi vya Ufaransa vikipiga doria Bangui.
Wahanga wa mauaji hayo ya kulipiza kisasi yaliofanywa na waasi waliokuwa wakiunga mkono serikali wa Seleka wengi wao walikuwa ni wanaume lakini pia walikuwemo wanawake na watoto na kwamba pia wanamgambo hao walifanya uporaji kwenye nyumba za raia. Mtaalamu wa Shirika la Amnesty kwa Afrika ya Kati Christian Mukosa amesema uhalifu umefanyika ukiwemo kunyongwa kwa watu, kukata viungo vya watu vipande vipande,uharibifu wa makusudi wa majengo ya kidini kama vile misikiti na kulazimisha mamia ya watu kuhama makaazi yao.
Kwa mujibu wa Amnesty licha ya kuwepo kwa vikosi vya Ufaransa na vile vya Afrika raia wameendelea kuuwawa kila siku ambapo takriban watu 90 wameuwawa tokea Disemba 8.Nayo ripoti ya shirika la Human Rights Watch imeonya kwamba vikosi hivyo vya Ufaransa vinapaswa kuimarishwa na vikosi kutoka nchi nyengine.
Mzozo huo wa Afrika ya Kati unatarajiwa kuwa juu katika agenda ya Mkutano wa Kilele wa Umoja wa Ulaya unaofanyika mjini Brussels leo hii na hapo kesho.
Walinda amani 2 wa UN wauwa Mali

Walinda amani 2 wa UN wauwa Mali



Waasi wa Azawad wamerejea vitani baada ya kutupilia mbali mkataba waliofikia na serikali miezi minne iliyopita

Walinda amani wawili wa Umoja wa Mataifa wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi la bomu dhidi ya benki inayofanya kazi peke yake mjini Kidal Kaskazini mwa Mali.
Msemaji wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo, alisema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mapema asubuhi kabla ya benki kufunguliwa.
Walinzi hao walikuwa wanalinda benki pekee inayomilikiwa na serikali mjini Kidal ambako waasi wa Tuareg wanataka kujitenga na Mali. Waasi hao walianza uasi wao miaka miwili iliyopita.
Shambulizi hilo linakuja kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wabunge.
Hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo, lakini kundi la Azawad linalotaka kujitawala Kaskazini mwa Mali limesema kuwa linajiandaa kususia uchaguzi huo.
Mnamo mwezi Novemba, kundi la MNLA lilitupilia mbali mkataba wa Amani uliofikiwa kati yao na serikali miezi minne iliyopita na kuanza tena uasi.
Na BBCSwahili

Jeshi la Ufaransa lashambuliwa

Vikosi  vya  jeshi  la  Ufaransa  limeshambuliana  na  waasi wa  zamani  katika  jamhuri  ya  Afrika  ya  kati  katika  mji mkuu  Bangui  leo  wakati  wakijaribu  kuwanyang'anya silaha  wapiganaji  baada  ya  ghasia  ambamo  mamia  ya watu  wameuwawa.  
Jeshi  la  Ufaransa  limeanza operesheni  ya  kuwanyang'anya  silaha  waasi , kwa nguvu  ikiwezekana , hususan  kundi  ambalo  linaundwa kwa  kiasi  kikubwa  na  Waislamu  la  Seleka  na  kundi hasimu  la  Wakristo. 
Wanajeshi  hao  wameweka  vizuwizi katika  barabara  kuu mjini  Bangui  na  wanapekua  kila gari  wakitafuta  silaha.
Mashambuliano  ya  silaha  yalizuka  karibu  na  uwanja wa  ndege  baada  ya  waasi  wa  Seleka  kukataa kukabidhi  silaha  zao. 
Msemaji  wa  jeshi  la  kimataifa  la kulinda  amani  katika  jamhuri  ya  Afrika  ya  kati  FOMAC Celestin Christ Leon  amesema  kuwa  waasi  wa  Seleka hawakutaka  kunyang'anywa  silaha  na  kukatokea mapambano  ya  silaha  kwa  muda. Mjini  
Wanajeshi wawapokonya waasi silaha CAR

Wanajeshi wawapokonya waasi silaha CAR



Waasi wa Seleka mjini Bangui
Wanajeshi wa Ufaransa wameanza kuwapokonya silaha waasi katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Leo asubuhi makabiliano yalitokea kati ya wanajeshi hao na wapiganaji wa serikali mjini Bangui, wakati shughuli hiyo ilipoanza.
Masemaji wa jeshi la Ufaransa, alisema kuwa wanajeshi waliwakamata wapiganaji kadhaa na kunasa silaha walizokuwa wanatumia.
Kikosi cha wanajeshi 1,600, kimepelekwa nchini CAR baada ya siku kadhaa za mapigano yaliyosababisha vifo vya watu 400.
Kiongozi wa waasi, Michel Djotodia, aliingia mamlakani mwezi Machi kwa usaidizi wa wapigajani wake ambao wengi wao ni waasi wa zamani. Djotodia amechukua mamlaka baada ya kumpindua aliyekuwa Rais Francois Bozize.
Wanajeshi wa Ufaransa, sasa wanashika doria katika barabara na mitaa ya mji mkuu Bangui.
Walikwenda Bangui siku ya Ijumaa baada ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa kuunga mkono azimio la kurejesha utulivu nchini humo kwa kutumia njia yoyote itakayofaa, hata kama ni kwa nguvu.
Nyumba zimeharibiwa kwa maguruneti kufuatia makabiliano makali kati ya waasi hao na wanajeshi na pia kutokana na vita vya kidini ambavyo vimetokana na vurugu hizo.
Wakati wa mapigano, mamia ya waumini wa kiisilamu walikimbilia katika nyumba ya Imamu mmoja ambako walikwenda kutafuta hifadhi.
NA BBCSWAHILI
80 wauawa kwenye mapigano A.Kati

80 wauawa kwenye mapigano A.Kati


Machafuko katika mji wa Bangui Afrika ya Kati
Baraza la Usalama la umoja wa mataifa limeidhinisha kutumwa maelfu ya majeshi ya Afrika na wa Ufaransa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Hali imeendelea kuwa mbaya nchini humo huku mapigano yakichacha usiku kucha na leo mchama mzima. Takriban watu 80 wameripotiwa kuuawa kwenye mapigano makali mjini Bangui Alhamisi.
Mji huo ulivamiwa na wafuasi wa Francois Bozize aliyeng'olewa mamlakani na waasi mwezi Machi hali iliyotumbukiza nchi hiyo katika mgogoro wa kisiasa.
Mapigano makali ya kurushiana risasi na silaha nzito nzito yalishuhudiwa mapema leo katika mji wa Bangui kabla Baraza kuu la Umoja wa Mataifa kupitisha azimio la kupeleka majeshi ya kutoka Afrika na Ufaransa.
Mwandishi wa habari wa BBC aliyepo katika mji wa Bangui anasema aliona magari ya kivita yakiendeshwa kupita katika mitaa na kwamba watu wengi bado wamejifungia majumbani mwao.
Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Gerald Araud ameiambia BBC kuwa kuongezwa majeshi ya kimataifa utasaidia hali ya usalama ndani ya wiki chache.
Bwana Araud amesema Majeshi ya Umoja wa Afrika na yale ya Umoja wa Mataifa yanapaswa kusimamia sheria na utulivu katika mji wa Bangui kabla ya kuangalia usalama katika miji mingine nchini Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
 Ufaransa yaongeza majeshi A. Kati

Ufaransa yaongeza majeshi A. Kati


Majeshi ya Ufaransa yakiwa ndani ya Kifaru cha kijeshi
Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imethibitisha kuwa imetuma mamia ya wanajeshi wa ziada kwenda kusaidia kuimairisha hali ya usalama Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Maafisa ya Umoja wa Mataifa umesema hali ya usalama nchini humo ni ya wasi wasi huku ikionya huenda mauaji ya halaiki yanaweza kuendelea.
Ufaransa imekuwa ikitoa msukumo kwa azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa ambalo linazungumzia namna ya kuyasaidia majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema raia katika eneo la Jamuhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakikumbana na matatizo yaliyozidi uwezo wao ikiwa ni pamoja na unyanyasi wa kijinsia, utesaji, mauaji na fujo kati ya wakristo na waislamu.
Majeshi ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakijaribu kuimarisha hali ya usalama nchini Afrika ya Kati tangu Rais Francois Bozize apinduliwa mwezi Marchi.

Kategori

Kategori