Walinda amani wawili wa Umoja wa
Mataifa wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa katika shambulizi la bomu
dhidi ya benki inayofanya kazi peke yake mjini Kidal Kaskazini mwa
Mali.
Msemaji wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini
humo, alisema kuwa shambulizi hilo lilifanyika mapema asubuhi kabla ya
benki kufunguliwa.Shambulizi hilo linakuja kabla ya duru ya pili ya uchaguzi wabunge.
Hakuna aliyedai kuhusika na shambulizi hilo, lakini kundi la Azawad linalotaka kujitawala Kaskazini mwa Mali limesema kuwa linajiandaa kususia uchaguzi huo.
Mnamo mwezi Novemba, kundi la MNLA lilitupilia mbali mkataba wa Amani uliofikiwa kati yao na serikali miezi minne iliyopita na kuanza tena uasi.
Na BBCSwahili