Showing posts with label 2017 at 06:24PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 06:24PM. Show all posts
‘NDAMA MTOTO WA NG’OMBE’ AKIRI TENA KOSA LA UTAKATISHAJI FEDHA

‘NDAMA MTOTO WA NG’OMBE’ AKIRI TENA KOSA LA UTAKATISHAJI FEDHA

MFANYABIASHARA Ndama Shabani Hussein maarufu kama ‘Ndama Mtoto wa Ng’ombe,’ jana alikiri kwa mara ya tatu shtaka la kutakatisha fedha dola za Marekani 540,000 baada ya upande wa utetezi kuomba mshtakiwa kukumbushwa mashtaka yake.
Awali, Mei 23 mwaka huu, Ndama alikiri kosa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ilipanga kusikiliza maelezo ya awali Mei 29, lakini aliomba muda wa kujadiliana na mawakili wa utetezi hadi Mei, 30, mwaka huu alipokumbushwa mashtaka yake na kukana kutakatisha fedha hizo. Hata hivyo, hali ilikuwa tofauti jana katika mahakama hiyo iliyoketi jana chini ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Victoria Nongwa, baada ya Ndama kuomba kukumbushwa mashtaka yake na aliposomewa, alikiri kwa mara nyingine kutakatisha fedha hizo. Wakili wa Serikali, Esterzia Wilson, alimkumbusha Ndama mashitaka yanayomkabili baada ya wakili wa utetezi, Jeremiah Ntobesya, 
kuomba mteja wake kukumbushwa mashitaka hayo. Mahakama iliridhia ombi hilo na aliposomewa hati ya mashtaka sita, alikana mashtaka matano na kukiri shtaka la sita la kutakatisha fedha. Katika shitaka la kutakatisha fedha, Ndama anadaiwa kuwa kwa tarehe tofauti jijini Dar es Salaam, kati ya Februari 26 na Machi 31, 2014, akiwa Mwenyekiti na mtiaji saini pekee wa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited na akaunti ya benki ya kampuni hiyo iliyoko benki ya Stanbic, alijihusisha moja kwa moja katika uhamishaji fedha dola za Marekani 540,000. Ilidaiwa kuwa alizitoa fedha hizo taslim huku akijua au alipaswa kujua kuwa ni za kosa kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Hata hivyo, Ndama alikana mashitaka mengine ikiwamo la kudaiwa kuwa Februari 20, 2014, akiwa jijini Dar es Salaam, alighushi nyaraka ya kibali cha kusafirisha madini na sampuli za madini kwa kusudi la kuonesha kuwa kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited iliruhusiwa kusafirisha maboksi manne ya dhahabu ya kilogramu 207, yenye thamani ya Dola za Marekani 8,280,000 kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL DTYL Limited wakati akijua si kweli. Pia Ndama anadaiwa kuwa Machi 6, 2014, Dar es Salaam, alighushi kwa kutengeneza hati ya kibali cha Umoja wa Mataifa Ofisi ya Dar es Salaam, akijaribu kuonesha kuwa kilogramu 207 za dhahabu kutoka nchini Congo zinazotarajiwa kusafirishwa na kampuni ya Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya KUBWA Muru Platnum Tanzania Investment Company Limited kwenda Australia kwa kampuni ya Trade TJL PTYL Limited, zimesafirishwa bila jinai yoyote wakati akijua ni kosa kisheria. Aidha, anadaiwa kuwa Februari 20, 2014, alighushi fomu ya forodha yenye namba za usajili R.28092 akionesha kampuni ya Muru imeilipa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) dola za Marekani 331,200 kama kodi ya uingizaji wa bidhaa ambazo zina uzito wa kilogramu 207 za dhahabu zenye thamani ya dola za Marekani 8,280,000 kutoka Congo. Katika shitaka jingine, Ndama anadaiwa kuwa Februari 20, 2014, alighushi nyaraka ya bima kutoka Phoenix of Tanzania Assurance Company Ltd, akionesha kampuni ya Muru imeyawekea bima makasha manne yaliyokuwa na dhahabu hizo. Anadaiwa kuwa kati ya Februari 26 na Machi 3, 2014, akiwa Dar es Salaam, kwa njia ya udanganyifu alijipatia kutoka kwa kampuni ya nchini Australia ya Trade TJL DTYL Limited dola za Marekani 540,000 baada ya kudanganya atawapa na kusafirisha dhahabu hizo. Awali, Ndama aliposomewa maelezo ya awali, baada ya kukiri kosa hilo, alikana maelezo mengi ya msingi yanayounda shitaka hilo. Kutokana na hali hiyo, Hakimu Nongwa aliamuru kesi hiyo kuendelea kusikilizwa kwa kuwa nia ya Ndama ya kukiri kosa ilikuwa na shaka.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sHh8OH
via IFTTT


Breaking Newss..Nape Moses Nnauye Afyatuka Mazito Kuhusu Sakata la Kufutwa Uwaziri na Magufuli..Ataka Aliyemnyooshea Bastola Akamatwe Lasivo Atafichua Makubwa ya Utawala wa JPM..!!!

Breaking Newss..Nape Moses Nnauye Afyatuka Mazito Kuhusu Sakata la Kufutwa Uwaziri na Magufuli..Ataka Aliyemnyooshea Bastola Akamatwe Lasivo Atafichua Makubwa ya Utawala wa JPM..!!!

Dar es Salaam. Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amezungumza na wapiga kura wake leo katika kijiji cha Chihuta huku akieleza kuwa yeye ndiye aliyemtafutia kura Rais John Magufuli katika kampeni za uchaguzi wa mwaka 2015.
Kadhalika Nape alizungumzia tukio la kutolewa bastola alipotaka kuzungumza na waandishi wa habari hivi karibuni na kuvitaka vyombo vya ulinzi na usalama vichukue hatua.
“Shida niliyonayo wapiga kura wangu huyu jambazi aliyetoa silaha vyombo vya ulinzi nausalama vinafanya nini,” alisema
Alisema kutokana na tukio lile, alihitaji busara zaidi na kutulia kwani kifua chake kina mambo mengi.

from Blogger http://ift.tt/2pdWOC3
via IFTTT


Vita vya Madawa ya Kulevya Vyaamia kwa Mawakili wa Serikali ya Rais Magufuli,Huu Ndio Mchezo Wanaoufanya Kupiga Pesa Ndefu Kupitia Madawa ya Kulevya ..!!!

MAWAKILI wawili wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), wanashikiliwa na kuhojiwa na Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya yenye kifupisho cha lugha ya Kiingereza cha DCEA, kwa tuhuma za kuharibu kesi za ‘unga’ siku za nyuma.
Kukamatwa kwa Mawakili wa Serikali hao ni matokeo ya ahadi ya mapema mwezi uliopita ya Kamishana Mkuu wa DCEA, Rogers Sianga.
Akikabidhiwa majina ya watuhumiwa 97 wa biashara ya dawa za kulevya na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Februari 13, Sianga alisema kuna majaji, mahakimu na Mawakili wa Serikali ambao walivuruga kesi zinazohusiana na dawa za kulevya kwa makusudi siku za nyuma.
Alisema kutokana na kuwapo kwa hali hiyo, DCEA ingepitia kesi zote za nyuma ambazo Serikali ilishindwa licha ya kuwa na vidhibiti, ili kuwabaini na kuwachukulia hatua, ikiwamo kwa kupeleka orodha kwa mamlaka husika.
Akizungumza na Nipashe jana iliyotaka kujua idadi ya watuhumiwa wanasheria hao na jinsi walivyohusika kupindisha kesi hizo, Sianga alisema:
“Hili jambo ni lazima ukae vizuri kwa kuweka ushahidi vizuri, (lakini) wanasheria wawili kutoka Ofisi ya Mwansheria Mkuu wa Serikali (tayari) tumeshawakamata.
“Hatua inayofuata ni kukamata mahakimu na majaji.
“Tunakwenda hatua kwa hatua kuhakikisha taratibu za kisheria zinafuatwa.
Kamishna Sianga ambaye aliiambia Nipashe kuwa alizungumza wakati akiwa safarini, aliahidi kutoa ufafanuzi zaidi wa hatua hiyo baadaye.
“Lakini kimsingi majina tunayo tayari na kuna mwanasheria atakayesimamia zoezi hilo anayejua namna ya kuchukua hatua kwenye suala hilo.”
Kamishna Sianga aliteuliwa Februari 12, na siku iliyofuata alikabidhiwa ripoti yeye majina ya watu 97 ambao ilidaiwa na Makonda kuwa wafanyabiashara, vigogo wa serikali ya awamu ya kwanza hadi ya tano, watoto vigogo na wananchi wengine.
Kamishna huyo alisema watapitia kesi zote za madawa ya kulevya zilizowahi kuamuliwa miaka ya nyuma, ili kuweka wazi zilizoharibiwa kwa makusudi.
Akitolea mfano wa kesi ambazo amedai zilivurugwa na mahakimu, alisema ni kesi iliyokuwa na ushahidi uliokuwa wazi kuwa mtuhumiwa amemeza dawa za kulevya, lakini hakimu akasema kuwa mtuhumiwa huyo alikuwa na matatizo ya vidonda vya tumbo.
Aidha, Machi 6, wakati Sianga akikabidhiwa ripoti ya dawa za kulevya kidunia iliyoonyesha robo tatu ya waathirika ni wanawake na watoto, alisema DCEA inawahoji vigogo watano.
Tangu hapo, iligundulika, mtoto wa Rais mstaafu wa awamu ya nne Jakaya Kikwete, ambaye ni Mbunge wa Chalinze (CCM), Ridhiwani Kikwete, ni mmoja kati ya watu waliohojiwa na mamlaka hiyo.
MSUKUMO MPYA
Vita dhidi ya dawa za kulevya nchini imepata msukumo mpya tangu Makonda ataje orodha ya watu 65 ambao alitaka waisaidie polisi kuhusiana na biashara ya madawa ya kulevya Februari 8.
Kabla ya kutaja orodha hiyo iliyokuwa na viongozi wa dini, wafanyabiashara na wanasiasa, Makonda alikuwa ametoa orodha ya Polisi 12 na wasanii kadhaa ambao walitakiwa pia kufika Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam kwa mahojiano.
Lakini harakati za kuwakamata watumiaji, wauzaji na watu wenye taarifa kuhusu biashara ya dawa za kulevya katika jiji la Dar es Salaam na nchini kwa ujumla zilipata msukumo mkubwa siku nne baadaye, baada ya Rais Magufuli kutaka zisiache mtu yeyote.
“Hakuna mtu maarufu, mwanasiasa, waziri au kiongozi yoyote au mtoto wa fulani, askari ambaye anajihusisha na dawa za kulenya aachwe, hata awe mke wangu Janeth… kamata wote weka ndani,” alisema Rais Magufuli.
Alisema biashara ya dawa za kulevya nchini imefikia katika hali mbaya na kwamba zinauzwa kama njugu nchini.
Alitaka vyombo vyote vya ulinzi vinavyoendelea kupambana na dawa za kulevya viendelee na mapambano.
Alisema biashara ya dawa za kulenya inapoteza nguvu kazi za Watanzania wengi haswa vijana, na kwamba vyombo vyote vya ulinzi vinapaswa kushirikiana ili kuwakamata hao.
Rais Magufuli aliwataka wahusika kuuwinda mtandao wote unaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
“Haiwezekani wauzaji wapo mtaani wanatanua tu, hawakamatwi,” alisema Rais Magufuli.
“Kwa mfano kuna muuzaji mkubwa yupo mkoani Lindi, alishikwa na dawa za kulevya lakini sijasikia hata siku moja akitangulizwa Mahakamani.
“Ninajua kuna viongozi wanamtetea.”
Rais Magufuli alikuwa akimzungumzia mtu anayeaminika kuwa ‘mzungu wa unga’ aliyekuwa akitafutwa zaidi nchini na Marekani pia.
Ali Khatibu Haji (50), maarufu kwa jina la Shikuba, alikamtwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Machi, 2014 baada ya kuwindwa kwa miaka miwili kabla ya kuhamishiwa mkoani Lindi.
Anatuhumiwa kuwa kiongozi wa genge lenye makao yake Afrika Mashariki lakini likiwa na uhusiano wa kibiashara mpaka China, Brazil, Canada, Japan, Marekani na Uingereza.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2njvzoY
via IFTTT


TAMKO LA WAZIRI DKT MWANYEKEMBE KUHUSU MADAI YA RC MAKONDA KUVAMIA CLOUDS

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe, leo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es salaam, amekiri kuwa anafahamu kuhusu tukio la uvamizi lililofanyika katika ofisi za Clouds Media Group.
Akizungumza na waandishi wa habari, Waziri Mwakyembe aliyechukua nafasi ya aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye alisema kuwa yeye kwa sasa hawezi kulizungumzia tukio hilo wala kutoa uamuzi wowote kwa kuwa hajapata ushahidi unaojitegemea.
“Ninachokijua kuhusu hilo tukio kinatokana na taarifa za vyombo vya habari, taarifa za magazeti, za redio, za televisheni, na sidhani kama taarifa hizo zinatosha kwa mimi kutoa uamuzi wowote.”
Ameongeza kuwa bado suala hilo ni la kuchunguzwa zaidi kwani picha inayotolewa ni ya upande mmoja.
“Mlalamikaji hapa ni Clouds, anayetupa taarifa kuhusu suala hili zima ni Clouds na wenzake. Kwa hivyo naipata picha hii kwa upande mmoja…”
Aidha kwa mujibu wa ripoti iliyokuwa imetolewa na kamati iliyoundwa na aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ilisema kuwa wamesikiliza upande wa mlalamikaji (Clouds Media Group).
Lakini walipokwenda kwa ajili ya kuusikiliza upande wa mlalamikiwa (RC Paul Makonda) hawakufanikiwa kumpata. Hii ni baada ya wao kusubirishwa kwa muda mrefu nje ya ofisi yake na baadae kuambiwa kuwa Makonda ameondoka na hatoweza kurudi kwa siku hiyo. Jambo hili liliwafanya wajumbe hao kujiaminisha kuwa Makonda hakuwa tayari kulizungumzia suala hilo na aliamua kuwatoroka.
Hata hivyo ripoti hiyo ilikabidhiwa kwa aliyekuwa Waziri, Nape Nnauye ili aifikishe katika mamlaka husika kwa ajili ya kuchukuliwa hatua zaidi.
TAZAMA JAMAA HUYU ALIVYOKOSWA KOSWA NA KIFO KWA AJARI MTONI

from Blogger http://ift.tt/2nQ51Qg
via IFTTT


Kategori

Kategori