from Blogger http://ift.tt/2opvgZw
via IFTTT
Showing posts with label 2017 at 06:28PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 06:28PM. Show all posts
Askofu Gwajima Aposti Ujumbe Huu Tata ..!!!
Mtu akichukua mateka atachukuliwa mateka, mtu akiua kwa upanga, atauawa kwa upanga, hapa ndipo penye subira na imani ya watakatifu
Ufunuo 13:10
NA HILI NDILO NENO LA MUNGU.
from Blogger http://ift.tt/2oTuZ2z
via IFTTT
Katuni 5 Bora Leo:SIASA, ELIMU & MICHEZO
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
from Blogger http://ift.tt/2ob1BI2
via IFTTT
Asasi 30 Afrika zalaani uvamizi Clouds
Dar es Salaam. Asasi za kiraia 33 barani Afrika zimelaani kitendo cha kuvamiwa kwa studio za televisheni ya Clouds na kulazimisha maudhui yasiyostahili yarushwe hewani.
Tamko la asasi hizo limetolewa ikiwa ni siku chache baada ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, (THBUB), Jukwaa la Wahariri (TEF) na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kulaani kitendo hicho kinachodaiwa kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.
Asasi hizo zinazohusika na utawala bora, demokrasia, haki za binadamu na uhuru wa habari zilikutana hivi karibuni mjini Kampala nchini Uganda katika mkutano uliokuwa ukizungumzia uhuru wa kujieleza na kupata habari.
Tanzania kwenye mkutano huo iliwakilishwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) , miongoni mwa mijadala iliyotawala ni kukemea vitisho na vitendo vya kunyanyasa waandishi.
Pia, wajumbe katika mkutano huo waligusia mabadiliko madogo ya baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais John Magufuli kwa kumtoa Nape Nnauye kwenye nafasi ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
Asasi hizo zilimpongeza Nape ambaye kabla ya kuondolewa kwenye nafasi hiyo aliunda kamati iliyochunguza tukio la uvamizi wa studio za Clouds, wakisema uamuzi huo ulionyesha ujasiri wa kusimamia uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na asasi hizo, ilidai kwa siku za karibuni Tanzania imekuwa na matukio zaidi ya 40 yanayolenga kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari.
“Waandishi wamekuwa wakizuiwa au wakati mwingine kubughudhiwa ili wasifanye kazi yao. Vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa hasa na wakuu wa wilaya na polisi,” ilibainisha taarifa hiyo.
Wajumbe walikumbusha kifungu cha pili cha Azimio la kanuni za uhuru wa kujieleza Afrika la mwaka 2002, kinachoelekeza Serikali ihakikishe inachukua hatua stahiki kuzuia uvamizi kwenye vyombo vya habari.
Kifungu hicho kinaelezea endapo uvamizi huo utatokea, Serikali ina wajibu wa kuchunguza na kuwaadhibu wahusika kwa mujibu wa kosa lao.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
from Blogger http://ift.tt/2nIdZhp
via IFTTT
BREAKING: Maalim Avuliwa Ukatibu Mkuu CUF
Baraza Kuu la Uongozi Taifa la Chama cha Wananchi(CUF) leo limemvua Maalim Seif nafasi ya Ukatibu Mkuu na kumpa Magdalena Sakaya.
Taarifa ya hatua hiyo imetangazwa Mapema leo na Prof Ibrahim Lipumba
Habari zaidi itakujia hivi punde…
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
from Blogger http://ift.tt/2nf8ovV
via IFTTT
Bunge Liko Kwenye Majaribu Makubwa- Lema
Kimenukaa..Nape Nnauye Aaanza Kuichana Serikali ..Amtaja Magufuli na Mwakyembe..!!!
Aliyekuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye kupitia ukurasa wake wa twitter amempongeza Rais Magufuli kwa kutumia busara kumwachia msanii Nay wa mitego huku akienda mbali na kudai kuwa matumizi ya nguvu kubwa hayana faida yoyote.
“Matumizi ya nguvu sana hayalipi! Kurekebisha kwa upendo hulipa! Hongera Rais, Hongera Mwakyembe kwa uamuzi wa Busara dhidi ya muziki wa Ney!”
Nay wa Mitego alikamatwa usiku wa kuamkia juzi ambapo alipelekwa katika Kituo cha Polisi Mvomero na baadae alisafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kati jijini Dar es Salaam.Alikuwa anatuhumiwa kwa kutoa wimbo ambao unaikashifu serikali.
Hata hivyo, Rais Magufuli kupitia kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Harrison Mwakyembe, jana mchana alitoa agizo kwa Jeshi la Polisi kumuchia huru msanii huyo na kutaka wimbo wake ‘Wapo’ uendelee kuchezwa kwenye vyombo mbalimbali,
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA
from Blogger http://ift.tt/2neXJBE
via IFTTT
Lissu Azidi Kumcharukia Magufuli, Akerwa Mtuhumiwa wa Range Rover Zilizofichwa Kwenye Makontena ya Mitumba Kusota Mahabusu Siku 23..!!!
RAIS wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Tundu Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Singida Mashariki, amesikitishwa na hatua ya Jeshi la Polisi – kitengo cha Bandari kuendelea kumshikilia Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju, bila kumfikisha mahakamani ama kumwachia kwa dhamana.
Ramadhani ndiye anayehusishwa na tukio la kusafirisha magari matatu ya kifahari aina ya Range Rover katika makontena ambayo taarifa zake zilionyesha mzigo huo ni nguo za mitumba, tukio lililofichuliwa na Rais Dk. John Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar e s Salaam takriban wiki moja iliyopita.
Lissu ambaye pia ni Mwanasheria Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na pia Mnadhimu Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni, aliweka bayana hayo jana, Machi 27, 2017. Kwa mujibu wa taarifa ya Lissu ambayo ‘tovuti’ hii imeinasa, Ramadhani amekuwa mahabusu kwa wiki kadhaa sasa.
“Nimetoka Polisi Bandari muda huu. Nilikwenda kumwona mtu aitwaye Ramadhani Mussa Hamisi Ukwaju ambaye yuko mahabusu ya Polisi Bandari tangu tarehe 4 ya mwezi huu. Ukwaju anatuhumiwa kuhusika na mzigo wa magari ya kifahari yaliyokamatwa na Bwana Mkubwa Rais siku chache zilizopita. Leo ni siku ya 23 yuko mahabusu. Hajapelekwa kwenye mahakama yoyote na hajashtakiwa kwa kosa lolote lile,” anaeleza Lissu
Anaendelea; “Suala lake limeshafika kwa DPP (Mwendesha Mashitaka) na kwa RPC Simon Sirro tangu siku kadhaa zilizopita lakini kila mkubwa anayehusika anaogopa kutoa maamuzi ya kumpeleka mahakamani au hata kumwachia kwa dhamana ya polisi.”
Kwa mujibu wa Lissu, hayo ndiyo madhara ya rais kuingilia majukumu ya kisheria yasiyomhusu. Anasisitiza; “Rais wetu anaweza kuwa Amiri Jeshi Mkuu lakini yeye sio askari polisi mwenye jukumu la kukamata wahalifu au kupeleleza makosa wanayotuhumiwa nayo.”
Anasema japokuwa ni Rais ndiye anayemteua DPP, lakini yeye si DPP na hana mamlaka ya kuamua nani apelekwe mahakamani na nani asipelekwe.
“Sasa inapotokea Rais anakwenda kwenye matukio ya uhalifu, kama ilivyokuwa kwenye suala la Ukwaju, anawafanya watendaji wanaohusika nayo washindwe kufanya kazi zao kwa mujibu wa sheria.
“Katika mazingira ya sasa ya ‘utumbuaji majipu’, watumishi wa umma wanaogopa kufanya maamuzi kwa hofu ya kutumbuliwa majipu, hasa kwa masuala ambayo yameshafikishwa kwa Rais kwa njia extra-legal kama hili la Ukwaju. Matokeo yake haki za wananchi za kuwa huru zinakiukwa bila sababu za msingi.”
“Haya ni masuala ambayo TLS chini ya uongozi wangu inatakiwa kuyashughulikia. Hii ni sehemu ya agenda tutakayompelekea Rais na IGP (Mkuu wa Jeshi la Polisi) na AG (Mwanasheria Mkuu wa Serikali) pamoja na Waziri mpya wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi tutakapoenda kuonana nao kama tulivyokwishawaomba. Kila mmoja wetu, mawakili na wasiokuwa mawakili tuyapigie kelele matumizi mabaya ya mamlaka ya kiupelelezi na ya kipolisi yanayopelekea haki za wananchi wetu kuvunjwa namna hii,” anasema Lissu na kuongeza kuwa kelele zitasaidia, ukimya ni sawa na kuyaunga mkono matendo hayo aliyoyaita mabaya.
from Blogger http://ift.tt/2nIi4lC
via IFTTT
Ukweli Mchungu…Rais Magufuli Kaitia Aibu Basata…!!!
MSANII Emanuel Elibariki ‘Nay Wa Mitego’ ameibua gumzo kubwa kufuatia kukamatwa kwake na kusafirishwa kutoka Turiani mkoani Morogoro hadi Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, kwa kile kinachodaiwa kuwa maelekezo ‘kutoka juu’ kuhusiana na wimbo wake mpya, Wapo.
Jana asubuhi, Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) chini ya Katibu wake Mkuu, Godfrey Mngereza, limetoa taarifa ya kuufungia wimbo huo, wakiukataza kutumika kwa namna yoyote hadi hapo maelezo mengine yatakapotolewa.
Basata ilitoa vifungu kadhaa vinavyoipa mamlaka ya kuchukua uamuzi huo, wakisema wimbo huo ulikosa maadili.
Mchana wa jana, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma, amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameliagiza Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kumuachia huru Rapa Emmanue Elibariki ‘Nay wa Mitego’!
Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Rais Magufuli ametaka Nay aachiwe huru na wimbo wake uendelee kupigwa kama ulivyo katika vyombo vyote vya habari, lakini kuna baadhi ya maneno ametaka yaongezwe endapo atataka, kama wauza madawa ya kulevya na wakwepa kodi.
Rais Magufuli ameusikiliza wimbo ule kama walivyousikiliza maofisa wa Basata na mamlaka zingine. Ameona jinsi Nay wa Mitego alivyojitosa kufikisha ujumbe wake kwa namna alivyofanya.
Kuagiza kuwa wimbo huo uendelee kupigwa na kujaribu kushauri kuongeza baadhi ya mada, ni wazi Rais Magufuli hakuona popote penye ukosefu wa maadili.
Katika hali ya kawaida, hili si jambo zuri hata kidogo, hasa kwa mamlaka kama Basata, ambao wanapaswa kuona kilichoonwa na rais tokea awali.
Ukilitazama jambo hili kwa macho mawili, unabaini kuwa mamlaka zetu hazifanyi kazi zao kwa weledi, isipokuwa kwa hisia, tena za uoga. Na huenda kuna mtu anatumia ukali wa Rais Magufuli kupenyeza ajenda kwa masilahi yake, huku akiwajengea wenzake hofu.
Jeshi la Polisi lilimkamata Ney juzi saa nane usiku na baada ya kulala ‘sentro’ kwa siku moja, Basata likaupiga marufuku wimbo wake asubuhi ya Jumatatu.
Kinachotokea ni watu, hawa walio katika mamlaka, kutekeleza majukumu yao kwa uoga na kujaribu kumtafsiri kiongozi mkuu wa nchi, badala ya kuangalia sheria walizoapa kuzisimamia zinasema nini.
Hii ni hatari, Nay amefanikiwa kutoka mikononi mwa dola kwa sababu habari zake zimemfikia rais kupitia mitandao, vipi kuhusu makumi kwa mamia ya watu wasio na umaarufu wanaotupwa selo kwa staili hii Tanzania nzima?
from Blogger http://ift.tt/2neJFYU
via IFTTT
Iyobo ..Siachi Kunengua Ng’oo..!!!
MNENGUAJI wa kundi la Wasafi Classic (WCB), Moses Iyobo, amesema hajawahi kufikiria kuwa mwimbaji kwakuwa ni kazi inayohitaji kutumia akili nyingi tofauti na unenguaji.
Iyobo ambaye amejizolea umaarufu mkubwa kutokana na aina yake ya uchezaji, amesema ataendelea kubaki kuwa mnenguaji katika maisha yake yote sambamba na kuwa mwalimu kwa wenzake.
Alisema kazi ya kuimba inahitaji akili nyingi ili kufikia malengo hivyo ataendelea kubaki na kazi yake ya unenguaji.
“Nitabaki kuwa dansa maisha yangu yote, labda nitakachoongeza hapo ni kuwa mwalimu na kuwafundisha wengine, unajua kuimba kunahitaji akili nyingi ili ufanikiwe. Sasa kwa upande wangu sitaweza ni bora nibaki huku huku ndio pananifaa zaidi,” alisema Iyobo ambaye ni mpenzi wa msanii Aunt Ezekiel.
from Blogger http://ift.tt/2nIgu3u
via IFTTT
Rasmi..Okwi Athibitiha Kuwa Anatua Simba Msimu Ujao,Atoa Kauli Hii kwa Yanga..!!!
AMA kweli Emmanuel Okwi amenogewa na Simba, kwani licha ya uongozi wa Wekundu hao wa Msimbazi kuweka wazi kuwa atarejea msimu ujao, taarifa kutoka Uganda zinadai kuwa, hata yeye mwenyewe ameonyesha mapenzi ya kurejea kwenye timu yake hiyo ya zamani.
Okwi, ambaye alikuwa akikipiga nchini Denmark katika Klabu ya SonderjyskE, kwa sasa anaichezea SC Villa ya nchini kwao Uganda na anafanya mambo makubwa, hali iliyomfanya kuitwa kwa mara nyingine katika kikosi cha timu ya Taifa ya nchi hiyo.
Miongoni mwa marafiki wa Okwi kutoka nchini Uganda, amesema kuwa, mchezaji huyo anasubiri tu kumalizika msimu huu arejee Tanzania kujiunga na Simba, baada ya viongozi wa timu hiyo kuonyesha nia ya kumhitaji.
“Hata yeye mwenyewe anaipenda Simba, kwa sasa baada ya kusikia kuwa viongozi pamoja na mashabiki wanataka arejee, anajiandaa kumalizia msimu huu na kuna kila dalili wakamalizana mapema,” alisema rafiki huyo wa karibu.
Kwa upande wake, Kocha wa zamani wa Simba, ambaye kwa sasa ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Uganda, Mosses Basena, alisema kuwa, Okwi amekuwa akionyesha kiwango kizuri kila siku, hivyo kama Simba atamrejesha watakuwa wamelamba dume.
Mapema Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, aliliambia gazeti hili kuwa, suala la Okwi wala halina mjadala mkubwa, kwani yeye kwa klabu hiyo ni kama nyumbani, hivyo anakaribishwa muda wowote.
from Blogger http://ift.tt/2nf453W
via IFTTT
Subscribe to:
Posts (Atom)
