Showing posts with label Act. Show all posts
Showing posts with label Act. Show all posts
Mwalongo Mshinde kesi ya kupinga matokeo jimbo la Njombe kusini

Mwalongo Mshinde kesi ya kupinga matokeo jimbo la Njombe kusini


MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imemtangaza Edward Mwalongo Kuwa mbunge wa jimbo la Njombe kusini katika kesi iliyo kuwa ikimkabili ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyo funguliwa na aliye kuwa mgombea ubunge kupitia Chadema Emmanuel Masonga.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5 ya uchakuzi mwaka 2015 jaji wa mahakama hiyo Jaji Jacob Mwambegele alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi ulio tolewa mahakamani hapo unaonyesha kuwa mlalamikaji hakupeleka malalamiko yake katika kamati ya ya maadili ya uchaguzi ya jimbo.

Alisema kuwa mahakama yake haiwezi kutengua ushindi uliomtangaza mbunge wa jimbo la Njombe Kusini kwa kuwa mdai hakupeleka malalamiko yake katika kamati ya maadili kama sheria inavyo sema.

Jaji Mwambegele alisema kuwa licha ya mahakama yake kubaini kuwapo kwa kampeni zilizo kuwa zemekiuka misingi ya kimaadili na kuendeshwa kwa udhalilishaji lakini mlalamikaji hakufuata sheria ya uchaguzi.

Alisema kuwa kigezo cha kuto peleka malalamiko katika kamati ya maadili Masonga inamnyima haki ya kupinga matokeo hayo kwa kuwa kamati ya maadili ilikuwepo na kuunyima ushahidi wake nguvu ya kushinda.

Jaji Mwambegele alisema kuwa uchaguzi huo uliendeshwa kwa uhuru na haki na kuwa hawezi kumtegua mshinde aliye shinda katika uchaguzi huo.

Kesi hiyo ilisikilizwa mashahidhi zaidi ya 30 kutoka pande zote za walalamikaji na washitakiwa na kusikilizwa kwa zaidi ya miezi 3 huku baadhi ya wiki kuendeshwa mfurulizo bila kupumzika na kufanya kesi hiyo kuisha haraka.

Katika ukumbi wa mahakama wafuasi wa Chadema walionekana kuwa wengi kuliko wale wa Chama cha mapinduzi CCM ambao walifika kusikiliza hukumu hiyo.

Aidha mbunge Mwalongo alitoa shukrani zake kwa mahakama Kuu kwa kumtangaza mshinda katika kesi hiyo ya kupinga matokeo.


Octoba 25 mwaka huu kulifanyika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani ulimtangaza Edward Mwalongo kuwa mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Njombe Kusini ambako kulikuwa na wagombea wane ambao walisimamishw ana Vyamba vya CCM, Edward Mwalongo kura 27285, Chadema Emmanuel Masonga kura 23003, Act Wazalendo Emilian Msingwa kura 3888 na DP William Myegeta. kura 94 katika kata zake 13

KAULI YA ZITTO KABWE KUHUSU UKAWA KUTOKA NJE WAKATI RAIS MAGUFULI AKIHUTUBIA BUNGE HII HAPA


WAKATI Rais Magufuli akimpa heko Mbunge wa Kigoma Mjini Kupitia chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe kwa kitendo chake cha kutoungana na wabunge wanaowakilisha umoja wa katiba ya wananchi Ukawa kupiga kelele na kutolewa nnje ya Bunge na Spika Job Ndugai,Zitto ameibuka na kuwaunga mkono wabunge hao.
Akizungumza nnje ya bunge, muda mfupi mara baada ya bunge hilo kuhairishwa na Waziri Mkuu Mhe Kasimu Majaliwa,Zitto amesema kuwa hakuna haja ya kuwajadili wabunge hao kwa kuwa demokrasia inawapa haki ya kufanya hivyo.

Zitto ambaye alikuwa akizungumza na Shirika la Habari Tanzania’TBC’ amesema kuwa haoni sababua ya wabunge hao kuitwa wahuni au watoto kama walivyoitwa Bungeni kwa kuwa kufanya hivyo ilikuwa ni sehemu ya kuwasilisha hisia zao kwa walengwa.

Amesema kuwa binafsi hana muda wa kulijadili suala hilo kwa kuwa limeshapita na kinachotakiwa kwa sasa ni kufanya kazi iliyowapeleka bungeni.

Zitto Kabwe Atoa Ushauri Muhimu Kwa Rais Magufuli Utakaosaidia Kuleta Mabadilko Kwa Watanzania

Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa ushauri wake kwa kiongozi mkuu wa nchi ili kuleta mabadiliko makubwa katika mfumo.

Zitto ameandika kupitia ukurasa wake wa Facebook, japo hakutaja jina lakini maelezo yake yanaonesha kuwa mwenye uwezo wa kufanya maamuzi hayo ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hivyo, ndiye mlengwa wa ujumbe huo.

Hivi ndivyo alivyoandika:
“Thomas Sankara once said “You cannot carry out fundamental change without a certain amount of madness”. Uwendawazimu

1) Weka mikataba yote ya Rasilimali za Nchi wazi – PSAs and MDAs 2) Futa posho za makalio katika mfumo mzima wa Serikali kama Mpango wa Maendeleo unavyotaka

3) Futa business class air tickets Kwa watendaji wa Serikali na wanasiasa isipokuwa Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu

 4)Futa matumizi ya mashangingi ( BoT wameonyesha mfano kwenye hili )

5 )Futa uagizaji wa sukari kutoka Nje na anzisha miradi ya miwa tuuze sukari Nje 

6 )Weka wazi taarifa ya Serikali kuhusu utoroshaji wa fedha na fungua mashtaka Kwa wahusika mara moja

7 )Wape takukuru mamlaka ya kukamata na kushtaki na kila mwenye Mali athibitishe yeye kaipataje (reverse burden of proof )

8 )Mali na Madeni ya Viongozi yawe wazi Kwa umma na wananchi waruhusiwe kuhoji

9 )Ruhusu mshindi wa uchaguzi Zanzibar atangazwe na ufanye naye kazi 

10)Acha mchakato wa Katiba Kwa kuanzia alipoishia Warioba, achana na Katiba Pendekezwa.”

Staa wa Bongo Movie kaamua kuingia ndani ya Daladala kupiga Kampeni za Ubunge Dar.. (Pichaz)

Staa wa Bongo Movie kaamua kuingia ndani ya Daladala kupiga Kampeni za Ubunge Dar.. (Pichaz)

Mkali wa Movie kwenye Kiwanda cha Bongo Movie Tanzania, Mohamed Mwikongiambaye wengi tunamfahamu kwa jina la Frank ni moja kati ya watu maarufu waliojitokeza kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika October 2015.
Frank ambaye ni mgombea Ubunge wa jimbo la Segerea kwa tiketi ya chama cha ACT Wazalendo October 12 2015 ameingia katika headlines baada ya kuonekana akitumia usafiri wa Daladala.
3X6A6898
Ripota wa millardayo.com alipata nafasi ya kupanda daladala moja na Frank na kushuhudia staa huyo wa filamu akiendeleza Kampeni zake humohumo ndani ya Daladala mdogomdogo..
Ikafanyika na exclusive interview na Frank ambapo alijibu pia sababu ya yeye kuonekana kwenye Daladala akifanya Kampeni zake…
DSC_0314
Unadhani huo ni usafiri wake wa kila siku au ndio mambo ya Kampeni? >>> “Huu ni utaratibu ambao ninao, hii ni daladala kwa daladala… ni fursa ya kukutana na watu wengi zaidi na kufahamu changamoto zao ambazo zinawakabili katika usafiri huu ikiwemo foleni, mimi daladala sijaanza kupanda wakati huu wa Uchaguzi, hata kabla ya Uchaguzi huwa naacha gari yangu nyumbani na kupanda daladala ili kupata idea za filamu”>>> Frank.
DSC_0313
Hii ni sauti ya Frank katika sehemu ya interview
U

Mgombea Ubunge ACT Wazalendo anusulika kupigwa na watu anaodai ni CCM










MGOMBEA wa ACT-Wazalendo jimbo la Njombe Kusini, Emilian Msigwa amenusulika kupigwa na watu wanao daiwa ni wafuasi wa chama cha mapinduzi akiwa katika mkunano wa kampeni za uchaguzi huku mfuasi mmoja wa chama hicho kukimbizwa Hospitalini.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Njombe Mgombea huyo alilalamika kuhusiana na vurugu hizo Juzi akisema kuwa zilitokea juzi katika mkutano wake uliokuwa ukifanyika katika kijiji cha Yakobi cha jimbo hilo mkoani Njombe.

Msigwa alisema kuwa katika kata ya yakobi amekuwa akipata shida ya kufanya kampeni katika vijiji vyake kutokana mgombea udiwani wa kata hiyo kupitia CCM kuweka vikwazo vya kuzuia mikutano ya chama hicho kwa kuweka naye ratiba zake na kufanya hujima na watendaji wa vijiji hivyo.

Alisema kuwa mgombea wa udiwani awali wlitakiwa kufanya mkutano katika kijiji hicho alicho letewa vurugu lakini alizuia gari ya matangazo na kusema kuwa katika kijiji hicho kuna kampeni za CCM kwa mujibu wa ratiba.

Alisema kuwa baada ya kufikishana katika Ofisi za kijiji cha Yakobi alibadilishiwa ratiba na kuwa mgombea huyo alikuwa  na ratiba ya siku nzima katika kijiji hicho hivyo siku ya Juzi baada ya kupangiwa ratiba kwa siku hiyo akiwa katikati ya mkutano aliona gari ya iliyo na bendela za CCM iliingia katika mkutano wake.

Akielezea mkasa huo alisema kuwa baada ya gali hiyo kuingia katika mkutano wake ilisimama kati kati ya jukwaa lake na upande walio simama wananchi na kuwa baada ya hapo uliwashwa muziki wa CCM na baada ya muda kuna watu walio na miili mikubwa (Mabaunsa) walishuka katika gali na kumfuata mfuasi wa chama hicho ambaye ni maarufu aliye toka chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema.

Alisema kuwa mfuasi hiyo Ally Mhagama maarufu Sagasaga alivamiwa na watu hao na kuanza kupigwa kasha kupelekwa katika gari ya CCM wakitaka kuondoka nae Wananchi wa liokuwepo kwenye mkutano hawakukubari waliamua kuaza kupambana nao.

Alisema wakati vurugu hizo zinatokea Polisi wa kulina uvunjifu wa amani katika mkutano wake hawakuwepo na kuwa yeye alikimbilia kweye gali akiwa anajiokoa.

Alisema kuwa wakati vurugu zinaendelea Mgombea Udiwani kata ya Yakobi alionekana eneo la tukio akiwa ameshika mawe mawaili akitaka kuwarushiwa wananchi na baada ya muda polisi walifika eneo la tukio.

Akizungumzia ulizi wa polisi katika mikutano yao alisema kuwa katika mikutano yao mingi ya vijiji huwa wanaenda bila ya kuwa na polisi kutokana na umbali wa maeneo na kuwa na imani ya kuwa na amani katika maeneo hayo na kusema kuwa mikutano ya mjini huwa wanakuwa na Polisi.


“Katika mikutano yetu yote wanayo ya vijiji huwa tunafanya bila ya kuwa na polisi kwa kuwa hawawezi kufika eneo la kampeni kutokan ana ubali wa baadhi ya maeneo na kuwapo na amani katika vijiji vingi lakini kwa maeneo ya mjini huwa tuna kuwa na askali na katika maeneo tunaona viashiria vya ukosefu wa amani huwa tuna waambia polisi wanakuwepo,” alisema Msigwa.

Msigwa aliongeza kuwa ameshiriki chaguzi nyingi lakini hajawahi kuona CCM wanafanya vurugu lakini vyama vingine lakini vyama vingine ni kawaida lakini mwaka huu ni tofauti na kuwa CCM wamebanwa.

"Chama cha mapinduzi mwaka huu kimebanwa na kinatumia mbinu mbalimbali kama zilivyonifanyia mimi mwaka huu," aliongeza Msigwa.

Akizungumza na Nipashe kamanda wa polisi mkoa wa Njombe, Wallboard Mtafungwa,   kwa njia ya simu alisema kuwa tukio hilo limewafikia na kuwa wanalifanyia uchunguzi huku akisema kuwa katika mkutano huo kulikuwepo na askari ambao haikuwa rahisi kufahamika.

Aliongeza kuwa jeshi hilo bado halijajua ni wakinanani wahusina kwa kuwa baada ya tukio walitokomea kusiko julikana.


ACT Wazalendo chaahidi kuweka nidhamu serikalini

ACT Wazalendo chaahidi kuweka nidhamu serikalini

Mgombea mwenza wa kiti cha Urais kupitia Chama cha ACT Wazalendo Hamad Yusufu amesema chama hicho kikiingia madarakani kazi ya kwanza itakuwa ni kuweka nidhamu serikalini ili kuhakikisha vitendo vya rushwa vinakwisha.

Ametoa kauli hiyo kwenye mkutano wake wa kampeni alioufanya mjini Babati mkoani Manyara.
Katika mkutano wake wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa kwaraa Babati, mgombea mwenza huyo wa urais kupitia ACT wazalendo amesema kwa kipindi cha miaka 50 chama cha Mapinduzi CCM hakijafanya lolote tofauti na kuendekeza rushwa iliyosabaisha umaskini.
Yusufu anasema kitu kingine kitakachopewa kipaumbele andapo chama hicho kitaingia madarakani ni kuboresha sekta ya elimu na kupitia mikataba yote ya wawekezaji.
Naye mgomea ubunge jimbo la Babati mjini kupitia ACT wazalando Biana Malya nasema kipaumbele chake ni kushughulikia afya.
Mgombea Mwenza wa chama cha ACT wazalendo Hamad Yusufu pia amewaombea kura wanaowania nafasi za udiwani kupitia chama hicho katika jimbo la Babati mjini.

TANZIA: Mgombea ubunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya ACT-Wazalendo afariki dunia



Mgombea ubunge wa Arusha mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo  Ndugu Estomih Malla amefariki dunia usiku wa leo saa saba katika hospitali ya KCMC Moshi.

Ndugu Malla alipelekwa KCMC jana mchana kutokea Hospitali ya St. Thomas iliyopo Arusha mjini baada ya kulazwa hapo kwa siku mbili kwa sababu ya kupata tatizo la shinikizo la juu la damu.

Hali hiyo ilimtokea siku ya tarehe 6/10/2015 mara baada ya kumalizika mkutano wa kampeni uliokuwa unafanyika Ngaramtoni,ambapo alilalamika kusikia kizunguzungu na baadae kukimbizwa hospital ya St Thomas ambapo madaktari wa pale walisema ndugu Malla anasumbuliwa na uchovu na hivyo anatakiwa kupumzika kwa muda mrefu.

Afisa Habari wa Chama Cha ACT Wazalendo, Abdallah Khamis, amethibitisha kutokea kwa kifo hicho. Amesema taarifa zaidi zitatolewa baadae baada ya uongozi wa chama hicho kufanya mawasiliano na viongozi waliopo mkoani Arusha.
Mpekuzi blog

MGOMBEA URAIS WA ACT-WAZALENDO AAHIDI KUMTEUA MAGUFULI KUWA WAZIRI WA UJENZI


Mgombea urais kupitia ACT-Wazalendo, Anna Mghwira amesema akipata ridhaa ya wananchi kuwa rais wa Tanzania, atamteua mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli kuwa Waziri wa Ujenzi.

Akizungumza kwenye mkutano wa kuhitimisha kampeni zake kwa Mkoa wa Arusha, mgombea huyo alisema Dk Magufuli ni mtendaji ndiyo maana anasisitiza kujenga madaraja na barabara kila anakokwenda.

“Kazi ya rais si kujenga barabara, sasa kwa kuwa yeye yuko vizuri katika suala la ujenzi nichagueni niwe rais wenu ili nije kumchagua aendelee kujenga barabara, kazi anayoifanya kwa ufanisi,” alisisitiza.

Awali, katika mikutano aliyofanya katika majimbo ya Arumeru Magharibi, Arumeru Mashariki na Arusha Mjini, mgombea huyo alisema Serikali yake ina sera mahsusi kwa ajili ya wananchi wa Arusha na Tanzania kwa ujumla.

Mkoa wa Arusha ni miongoni mwa mikoa yenye utajiri mkubwa nchini ukiwa umezungukwa na rasilimali mbalimbali.

Alisema mkoa huo pekee wenye madini ya Tanzanite nchini na duniani kwa ujumla, pia una mbuga mbalimbali za wanyama.

Kwa upande wa kilimo, alisema mazao kama kahawa, maua, vitunguu maji na mbogamboga ni vipaumbele vyake.

“Tunataka Watanzania wajiwekee akiba ili tutunishe mifuko ya hifadhi ya jamii. Katika utawala wetu tunataka watu milioni tano waingie kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kipindi cha mwezi mmoja,” alisema na kuongeza:

“Ukiweka Sh10,000 Serikali itakuongezea Sh20,000, hivyo kila mwezi utakuwa na uhakika wa kuingiza Sh30,000,” alisema.

Alisema mfumo wa maisha ya Watanzania unahitaji kufanyiwa mabadiliko na wao ndio wanaopaswa kusimamia suala hilo

ZOMEA ZOMEA ACT NJOMBE NGOME YA CHADEMA

 MGOMBEA wa chama cha ACT-Wazalendo jimbo la Njombe kusini amekunana na somea zomea wakati akimnadi mgombea Urais kupitia chama chache Anna Mgwila na kuonekana kumkandia mgombea wa ubunge wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema baada ya kusema mgombea huyo hataweza kuiondoa CCM.

Akizungumza katika kampeni zake katika kata ya Njombe mjini mgombea wa Ubunge jimbo la Njombe kusini Emilian Msigwa alikutana na zomea zomea baada ya kuanza kujinadi katika Ngome ya chama cha Chadema ambapo katika jimbo hilo anakubalika na vijana ambao walikuwepo katika mkutano huo.

“Ndugu zangu wana Njombe nataka niwaambia kuwa katika kipindi hiki wote tunataka mabadiuliko katika jumbo hili naombeni mnipekura mimi na za Urais mumpe mama Anna Mgwila na udiwani mumpe diwani wa kata yenu hasa wa Chadema kwa sababu sisi hatuma madiwani na nipo tayari kufanya kazi na diwani yoyote,” alisema Msigwa na ndipo zomea ilipo  anza.

Wananchi walio kuwepo katika mkutano howa walionekana kukelwa na kusemwa kwa mgombea ubunge wa Chadema Emmanuel Masonga na kulkisikia jina la Mgwila.
Msigwa akisema wamchague yeye na kuwa ataiondoa CCM alikutana na sauti ya Ooooooh! Na akisema wamchague Mgwila zilisikika sauti za Rais Lowassa bila mafanikoa na badayalake kuwaomba wananchi kuuliza mashwali kitu kilicho ongeza zomeazomea kutokana na maswali aliyo kuwa akiulizwa na watu alio dai kuwa wapo Chadema.

Kadri zomea zomea ilipo kuwa ikiongezeka vijana walizidi kuongezeka ili kuona kinacho endelea katika mkutano huo, ambapo maswali yaliyo kuwa yakiuliwa yalikuwa kakikazania kumchafua na kumfanya azidi kuzomewa.

Moja ya swali lililoulizwa katika mkutano huo ni pamoja na kwanini anasema kuna wagombea anawaunga mkono wa Chadema alipokuwa Chadema lakini aligombea nao mpaka alishindwa na kuhamia chama alichopo.

Akijibu swali hilo alisema kuwa wakati anagombea katika kura za maoni za Chadema alisema kuwa ilionekana kuwa hata likiwekwa jiwe Chadema kinaweza kushinda ndio maana na yeye aliingia kushindana licha ya kuwepo watu anao wakubali.

Aidha Nestory Mkinga aliulizwa kuwa vyama vyote vya upinzani lengo lake ni kukiondoa chama cha CCM lakini kwanini wanachama wa ACT wasiungane Ukawa kuiondoa CCM.


Akijibu shwala hilo alisema kuwa vyama vyama vyote vinakatiba yake na kuwa chama chake Katiba yake hairuhusu kujiunga na Ukawa.

ACT-Wazalendo Njombe na kuelekea Dodoma katika Picha

Picha zifuatazo ni picha zinazo kampeni ya ACT-Wazalendo Njombe mjini leo zikiwa na mgombea wa Ubunge wa jombo la Njombe Kusini  kupitia chama hicho karibu na fuatilia.......

 
 Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Njombe wakisikiliza sera za mgombea wa Chama cha ACT- Wazalendo, jombo la Njombe Kusini Emiliani Msigwa.



 Emiliani Msigwa Mgombea wa Ubunge wa jimbo la Njombe Kusioni kupitia chama cha ACT-Wazalendo 

Baadhi Wakazi wa njombe wakiwa katika Mkutano wa ACT-Wazalendo

Polisi Yathibitisha Mgombea Ubunge wa ACT-Wazalendo Kutekwa


Jeshi la Polisi mkoani Simiyu limethibitisha kutekwa kwa mgombea ubunge Jimbo la Bariadi, kupitia chama cha ACT Wazalendo Masunga Ng’hozo na watu wasiojulikana.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Gemini Mushy amesema kuwa tangu kutoweka kwa mgombea huyo, simu yake imekuwa ikitumika kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa wazazi wake.

Amesema kuwa ujumbe huo umekuwa ukiwataka wazazi wake kutoa kiasi cha fedha shilingi milioni mbili na nusu ndipo waweze kumwachia huru vinginevyo wajiandae kupokea maiti ya mwili wa mtoto wao.

Kamanda Mushy ameeleza kuwa mgombea ubunge huyo ambaye ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, (SAUT) kampasi ya Mbeya alitoweka Septemba 27 mchana akitokea ofisi ya chama hicho mkoa.

Amesema kuwa jeshi la polisi liliweza kupata taarifa rasmi ya kutekwa mgombea huyo tarehe 29 Septemba mwaka huu, ambapo ameeleza kuwa mpaka sasa siku ya nne hajulikani alipo na yuko katika mazingira ya usalama kiasi gani.

“ Ni kweli tumepata taarifa za mgombea ubunge huyo kutekwa na mpaka sasa ni siku ya nne hatujafahamu yuko sehemu gani na katika mazingira gani lakini jeshi la polisi kwa kushirikiana na wazazi wake na watu wake wa karibu tunaendelea kufanya uchunguzi ili tubaini mahali alipo na wahusika wa tukio hilo” amesema Kamanda Mushy.

Aidha Kamanda Mushy amesema kuwa kabla ya mgombea huyo kutekwa aliondoka katika ofisi ya chama hicho Mkoa, alikiwa amebeba begi lake huku akiwa anaongea na simu huku akimtaka dereva wa gari lake pamoja na fundi mitambo kumsubiri ofisini hapo.

Kufuatia tukio hilo Kamanda Mushy ameeleza kuwa jeshi lake linaendelea kufanya uchunguzi kwa njia ya mitandao ili kubaini ujumbe wa vitisho unatokea maeneo gani ikiwa pamoja na kuwakamata wahusika wanaoendelea kutumia simu ya mgombea huyo.

Kwa upande wake Katibu wa ACT-Wazalendo, Simiyu, Matondo Maduhu amesikitishwa na kulaani kitendo hicho, hivyo wanaliomba jeshi la polisi kufanya uchunguzi mapema ili kubaini mahali na kunusuru maisha ya mgombea huyo.

Mpekuzi blog
ACT Wazalendo: Tutamaliza tatizo la maji Tabora.

ACT Wazalendo: Tutamaliza tatizo la maji Tabora.

KIONGOZI wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema kama chama hicho kitashinda katika Uchaguzi Mkuu ujao, kitamaliza tatizo kubwa la maji lililopo mkoani Tabora.

 
Kabwe aliyasem,a hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Mjini Tabora akiwataka wananchi kuhakikisha wanawachagua wagombea wa chama hicho kuanzia rais, wabunge na madiwani.
 
Alisema Ilani ya ACT, imeeleza wazi juu ya mpango wa chama hicho kuanzisha mfuko wa maji vijijini ambao utatumika kuendeleza, kulinda vyanzo vya maji na kukarabati miundombinu yake.
 
“Wakazi wa Tabora msiwe na wasi, jitokezeni kwa wingi kwenye vituovya kupigia kura mkaichague ACT ili tufanye kazi ya kuondoa kerokubwa ya maji,” alisema.
 
Aliwaomba wamchague Nicholaus Kayoka kuwa mbunge wa Jimbo la Ulyankulu, Amir Kirungi (Kaliua), Abraham Rupia (Sikonge), Kansa Mbaruku (Tabora Kaskazini) na Mapalala Kuziwa (Tabora Mjini).
ACT designates Zitto to be Prime Minister

ACT designates Zitto to be Prime Minister


By PETI SIYAME

ACT-Wazalendo Union Presidential candidate, Ms Anna Mghwira, pledged that if elected she will appoint Mr Zitto Kabwe to be the prime minister.

ACT-Wazalendo leader Mr Zitto Kabwe
ACT-Wazalendo leader Mr Zitto Kabwe

Ms Mghwira said this while addressing campaign rally held on Thursday at Kizwite area and that she had already beseeched ‘wananchi’ from Kigoma to vote for Mr Kabwe so that she would be able to appoint him the prime minister of the Fifth Phase government.

Mr Kabwe who is the chief leader of ACT- Wazalendo is contesting for parliamentary seat for Kigoma Urban Constituency.

During the campaign rally, Ms Mghwira was accompanied by her running mate, Mr Hamad Yusuph Musa. “When I was in Kigoma I implored ‘wananchi’ from Kigoma Urban Constituency to vote for Mr Kabwe,” she added.

She further said that if elected, she will ensure that every senior officer must declare his or her wealth and debts in public as an effort to ensure transparency and commitment.

Ms Mghwira also said that it was important to establish special modern agriculture zone in three regions of Rukwa , Kigoma and Katavi which are famous for food crops.


“Once established these zones will be able to feed the whole country as well as create jobs,” she explained.

Earlier on, in his welcoming note, the running mate, Mr Musa said that there is need for a special dialogue that will involve all union presidential candidates and the public a chance to ask them different questions.

Source: Tanzania Daily News

ACT-Wazalendo wazindua kampeni zao Mbagala Zakhem Dar es Salaam

 Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira (kushoto), akihutubia katika uzinduzi wa kampeni ya chama hizo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala jijini Dar es Salaam leo.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto akihutubia katika uzinduzi huo.
 Mshauri wa Chama cha ACT-Wazalendo, Profesa Kitila Mkumbo akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto (kushoto), akiteta jambo na  Mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mghwira.
 Viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiimba wimbo wa taifa.
 Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akiwatambulisha wagombea ubunge wa majimbo yote ya Dar es Salaam.
  Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Kabwe Zitto, akigawa ilani ya chama hicho kwa mgombea urais na mwenza wake.
 Mgombea Mwenza, Hamad Mussa Yusuph akihutubia kwenye uzinduzi huo.
 Mwana muziki Bwana misosi, akitoa burudani katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Mbagala Dar es Salaam leo.
Umati wa Wananchi ukiwa katika uzinduzi wa kampeni wa Chama cha ACT-Wazalendo uliofanyika viwanja vya Zakhem Magala Dar es Salaam leo.

MGOMBEA URAIS WA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO KUJULIKANA LEO



MGOMBEA urais kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, anatarajiwa kujulikana leo baada ya Kamati Kuu ya chama hicho kupendekeza jina la mgombea atakayepeperusha bendera ya chama hicho.


Jana Kamati Kuu ya chama hicho ilikutana jijini Dar es Salaam, kujadili majina ya wagombea wa nafasi ya urais na ubunge. 

Akizungumza na waandishi wa habari, Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba alisema kamati hiyo imekutana kwa ajili ya kujadili ajenda tatu ikiwemo ya kujadili majina ya wagombea.


Alisema kujadiliwa kwa majina hayo ni baada ya kumalizika kwa kura za maoni zilizofanyika katika mikoa mbalimbali nchini.

Vurugu kubwa mkutano wa ACT shinyanga,zomea zomea yatawala,story nzima iko hapa





Mkutano wa hadhara wa Chama Cha ACT-Wazalendo uliokuwa ukiongozwa na mwenyekiti wa taifa Anna Mugwira leo jioni katika Viwanja vya Shycom Mjini Shinyanga umegubikwa na vituko na zomea zomea za hapa na pale baada ya viongozi wa Chama hicho kupanda jukwaani kuwahutubia wakazi wa Shinyanga.

Vurugu hizo zimeanza baada ya katibu mwenezi wa ACT Wazalendo taifa Sabini Richard kupanda jukwaani na kuwatangazia wananchi kuwa kiongozi wa taifa wa Chama Hicho Zitto Kabwe hatahudhuria mkutano kutokana na kuwa na kazi zingine za kichama.


Kufuatia taarifa hizo wananchi walianza kupiga kelele na kuondoka kwenye mkutano huo huku wakilalamika kuwa kwanini chama hicho kiliwatangazia kuwa Zitto atakuwepo kwenye mkutano huo.

Hata hivyo hali ilikuwa mbaya zaidi baada ya mwenyekiti wa chama hicho taifa Anna Mugwira kupanda jukwaani na kuwakaribisha baadhi ya madiwani waliokuwa wa Chadema katika manispaa ya Shinyanga Nyangaki Shilungushela na Siri Yasin ambapo wananchi walianza kunyosha vidole vya ishara ya Chadema na kuimba Yuda Yuda Yuda!!

Wananchi hao walisikika wakisema kuwa madiwani waliohamia ACT Wazalendo ni wasaliti wa Chadema na hawajafanya lolote katika kata zao wakati wa uongozi wao.


Akizungumza katika mkutano huo huku akizomewa na wananchi Aliyekuwa diwani wa viti maalum kata ya Chamaguha Siri Yasin amesema lengo la ACT wazalendo ni kuwakomboa wananchi na kwamba watakijenga chama hicho kama walivyofanya kazi ya Kujenga Chadema na kuifanya ikue katika manispaa ya Shinyanga.

Yasin amesema waliofanya vurugu hizo wameowaonea wivu madiwani hao wa Chadema waliohamia ACT Wazalendo.

Naye aliyekuwa diwani wa kata ya Kambarage Nyangaki Shilungushela akizungumza katika mkutano huo amewataka wananchi kuwapuuza wanaobeza ACT Wazalendo na kudai kuwa hata wakati wanaianzisha CHADEMA walionekana kupuuzwa na baadaye wananchi kuona chama kinafaa.


Kwa upande wake mwenyekiti wa ACT Wazalendo Jimbo la Shinyanga mjini Godwin Makomba amewataka wananchi kuacha kufanya vurugu na kuunga mkono chama hicho.

Awali wakati mkutano unaanza kijana mmoja ambaye hakujulikana jina wala makazi yake anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 hadi 25 alinusurika kuuawa na wananchi waliohudhuria mkutano huo kwa madai kuwa alikuwa anaiba pesa za mmoja wa wananchi waliohudhuria mkutano huo.

Hata hivyo walinzi wa ACT Wazalendo wakishirikiana na askari wa jeshi la polisi walifanikiwa kunusuru maisha ya kijana huyo kisha mkutano kuendelea huku zomea zomea kwa kila kiongozi aliyepanda jukwaani zikitawala hadi mkutano ulipomalizika .

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa zomea zome hizo zimefanywa na watu wanaodaiwa kuwa wafuasi wa CHADEMA,huku ikidaiwa kuwa hata huyo kijana aliyenusurika kuuawa ni mpango wa watu hao kuharibu mkutano wa ACT Wazalendo.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde,alikuwepo eneo la tukio,ametuletea picha kutoka eneo la tukio,TAZAMA HAPA CHINI


Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Jimbo la Shinyanga mjini Godwin Makomba alifungua mkutano wa hadhara katika viwanja vya Shycom mjini Shinyanga
Viongozi wa ACT Wazalendo wakiwasukuma wananchi waliokuwa na hasira,waliokuwa wanamshushia kipigo kijana(yupo hapo chini) aliyedaiwa kuwa alikuwa anaiba pesa kwenye mfuko wa suruali ya mmoja wa wananchi walikuwa kwenye mkutano huo
Kijana aliyenusurika kuuawa baada ya kudaiwa kuiba pesa kwenye mkutano
Wafuasi wa ACT Wazalendo wakimwokoa kijana huyo,yuko chini
Baunsa wa ACT Wazalendo akimwokoa kijana huyo kabla ya askari hawajafika eneo la tukio
Askari polisi akimwokoa kijana huyo
Kijana akiondolewa eneo la tukio na wasamaria wema na askari polisi
Askari polisi wakiwa na kijana aliyenusurika kifo na wananchi wenye hasira
Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo taifa Sabin  Richard akizungumza kwenye mkutano huo na baada ya kusema Zitto Kabwe wananchi wakaanza kupiga kelele(kuzomea) kisha kuanza kutawanyika
Wananchi wakiondoka kwenye mkutano

Katibu mwenezi wa ACT Wazalendo Sabin Richard akiwahutubia baadhi ya wananchi waliobaki kwenye mkutano
Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Anna Mugwira,akimtambulisha aliyekuwa diwani wa CHADEMA kata ya Kambarage katika manispaa ya Shinyanga Nyangaki Shilungushela,aliyeambulia kuzomewa na wananchi


Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Anna Mugwira,akimtambulisha aliyekuwa diwani wa viti maalum CHADEMA kata ya Chamaguha katika manispaa ya Shinyanga,ambaye pia alizomewa

Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Anna Mugwira,akiwahutubia wakazi wa Shinyanga katika wakati mgumu kwani zomea zomea zilitawala
Nyangaki Shilungushela akizungumza katika mkutano huo,huku akieleza kutokereka na zomea zomea hizo akidai kuwa hata wakati wanaianzisha CHADEMA walipuuzwa sana

Baadhi ya wananchi waliokuwa wanazomea wakiwa wamenyoosha vidole viwili wakiimba YUDA YUDA YUDA!!
Siri Yasin akizungumza katika mkutano huo


Zomea zomea na vidole viwili ikiendelea

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga

Kategori

Kategori