Mwalongo Mshinde kesi ya kupinga matokeo jimbo la Njombe kusini


MAHAKAMA kuu kanda ya Iringa imemtangaza Edward Mwalongo Kuwa mbunge wa jimbo la Njombe kusini katika kesi iliyo kuwa ikimkabili ya kupinga matokeo ya uchaguzi iliyo funguliwa na aliye kuwa mgombea ubunge kupitia Chadema Emmanuel Masonga.

Akisoma hukumu hiyo ya kesi namba 5 ya uchakuzi mwaka 2015 jaji wa mahakama hiyo Jaji Jacob Mwambegele alisema kuwa baada ya kupitia ushahidi ulio tolewa mahakamani hapo unaonyesha kuwa mlalamikaji hakupeleka malalamiko yake katika kamati ya ya maadili ya uchaguzi ya jimbo.

Alisema kuwa mahakama yake haiwezi kutengua ushindi uliomtangaza mbunge wa jimbo la Njombe Kusini kwa kuwa mdai hakupeleka malalamiko yake katika kamati ya maadili kama sheria inavyo sema.

Jaji Mwambegele alisema kuwa licha ya mahakama yake kubaini kuwapo kwa kampeni zilizo kuwa zemekiuka misingi ya kimaadili na kuendeshwa kwa udhalilishaji lakini mlalamikaji hakufuata sheria ya uchaguzi.

Alisema kuwa kigezo cha kuto peleka malalamiko katika kamati ya maadili Masonga inamnyima haki ya kupinga matokeo hayo kwa kuwa kamati ya maadili ilikuwepo na kuunyima ushahidi wake nguvu ya kushinda.

Jaji Mwambegele alisema kuwa uchaguzi huo uliendeshwa kwa uhuru na haki na kuwa hawezi kumtegua mshinde aliye shinda katika uchaguzi huo.

Kesi hiyo ilisikilizwa mashahidhi zaidi ya 30 kutoka pande zote za walalamikaji na washitakiwa na kusikilizwa kwa zaidi ya miezi 3 huku baadhi ya wiki kuendeshwa mfurulizo bila kupumzika na kufanya kesi hiyo kuisha haraka.

Katika ukumbi wa mahakama wafuasi wa Chadema walionekana kuwa wengi kuliko wale wa Chama cha mapinduzi CCM ambao walifika kusikiliza hukumu hiyo.

Aidha mbunge Mwalongo alitoa shukrani zake kwa mahakama Kuu kwa kumtangaza mshinda katika kesi hiyo ya kupinga matokeo.


Octoba 25 mwaka huu kulifanyika uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani ulimtangaza Edward Mwalongo kuwa mshindi wa kiti cha ubunge katika jimbo la Njombe Kusini ambako kulikuwa na wagombea wane ambao walisimamishw ana Vyamba vya CCM, Edward Mwalongo kura 27285, Chadema Emmanuel Masonga kura 23003, Act Wazalendo Emilian Msingwa kura 3888 na DP William Myegeta. kura 94 katika kata zake 13