Showing posts with label mauaji. Show all posts
Showing posts with label mauaji. Show all posts

MAMA NA MWANA WACHINJWA SHINYANGA


WATU wawili, Dilu Tungu (80) na mwanawe Bunya Mihangwa (45) wameuawa kikatili kwa kuchinjwa na watu wasiofahamika baada ya kuvamia nyumba hiyo katika kijiji cha Ihugi kata ya Lyamidati wilaya ya Shinyanga kwa kile kilichoelezwa kuwa ni imani za kishirikina.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha alisema kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14 mwaka huu saa mbili usiku katika kijiji cha Ihugi, kata ya Lyamidati tarafa ya Nindo wilaya ya Shinyanga.
Akielezea zaidi kuhusu tukio hilo alisema siku hiyo, Dilu na mtoto wake Mihangwa, wote wakazi wa Ihugi wakiwa nyumbani kwao wakijiandaa kwa chakula cha usiku na wanafamilia wenzao walivamiwa na watu watatu wasiofahamika wakiwa na mapanga.
Baada ya kuwavamia walianza kuwakata kwa panga sehemu mbalimbali za miili yao kisha kuwachinja shingo hadi wakapoteza maisha
alisema Kamanda Kamugisha.
Alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni imani za kishirikina kutokana na kile kilichodaiwa kuwa mwanamume aitwaye Bwanya Mlyashimba (40), mkazi wa Ihugi alikuwa akiwatuhumu Dilu na mwanawe Mihangwa kwamba walimroga yeye mwenyewe na kusababisha akose nguvu za kiume.
Alisema mbali na Mlyashimba kuwatuhumu kumroga, pia alikuwa anawatuhumu kumroga mama yake aitwaye Hollo Mahangwa aliyefariki dunia mwaka 2013.
Akasema Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa huyo kwa mahojiano zaidi huku likiendelea kuwasaka wahusika wengine wa mauaji hayo.

WAWILI WAFA MWAKA MPYA


WATU wawili wakazi wa Jijini Mbeya wamefariki katika matukio mawili tofati likiwemo la mtu kumfumania binamu yake na mpenzi wake nyumbani kwake katika maeneo ya Inyala jijini hapa.


Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi alisema, tukio la kwanza lilitokea siku ya mwaka Mpya (Juzi)  majira ya saa 10:00 katika maeneo ya Inyala halmashauri ya jiji la Mbeya.

Alisema kuwa katika tukio hilo, Huruma Laiton akufa wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Mbeya baada ya kupigwa mateke na Mme wake baada ya kufumaniwa akiwa chumbani na binamu wa mmumewe.

Alisema kuwa marehemu afumaniwa na mumewe, Mwakabenga Ezekiel mke wake akiwa ndani na Binadamu yake.

Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika huspitali ya rufaa jijini Mbeya.

Msangi alisema kuwa katika tukio la Pili lilitokea katika maeneo ya Itezi mashariki kata ya Itezi Jijini Mbeya Christopher Myamba, alifariki dunia baada ya kuchomwa kisu shingomi na Ndele baada ya kuzuka ugomvi.

Mgogoro huo ulitokea baada ya marehemu kukutana na kundi la vijana waliwa wa,elewa na kuzuga ugomvi ambao ulisababisha marehemu kuchomwa kisu.
Msangi alisema kuwa mara baada kifo cha marehemu mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chuma cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa Mbeya.

Alisema kuwa kufuatia tukio hilo linamtafuta mtuhumiwa na ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la Mbeya kuwa mwenye taarifa atoe taarifa ili kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.

Wafugaji vs Wakulima Kiteto: Mauaji ya kutisha!

Msomaji, habari hii inaambatana na picha ya maiti ya mtu aliyekatwa koromeo na kufariki, sijaianika wazi imefichwa hapa.


WILAYA ya Kiteto imeingia kwenye orodha ya maeneo yanayotisha kwa mauaji ya kinyama baada ya wakulima kuuawa mara kwa mara na wafugaji kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo za kugombea ardhi  Miongoni mwa waliouawa kinyama Dec 20 kwa kuchinjwa shingo yake ni Juma Mlagwa (49) wa Kitongoji cha Kalikala Kata ya  Njoro (Kiteto) ambaye alivamiwa nyumbani kwake usiku na kundi la vijana wa kifugaji masai (makorianga)  Imeelezwa kuwa wakati anavamiwa zilisikika Risasi zikipigwa juu Kitongojini hapo na baada ya watu kuendelea kujificha ndani vijana hao walianza kunyinyizia nyumba zao mafuta aina ya petrol  kisha kuwasha moto  Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara Ally Mussa Mwenyekiti wa Kitongoji hicho alisema siku hiyo haitasahaulika mashani mwake kwa yaliyotokea kutokana na vitendo hivyo akisema ilikuwa mara ya kwanza kuona mtu anachinjwa hadharani  “Nilichomewa Pikipiki zangu mbili pamoja na vitu mbalimbali vya ndani zikiwemo nguo vyakula, lakini nilichonusuri ni roho yangu ambayo hadi leo nasema najivunia uhai nilio nao”alisema Mwenyekiti huyo  Alisema chanzo cha mauaji hayo ni jamii ya kifugaji wamasai kuingiza mifugo yao kwenye shamba la mmoja wa wakulima Kitongojini hapo na baada ya kukatazwa walimpiga kisha nae kupigwa ndipo wakakusanyana kupanga uvamizi huo  Hata hivyo baada ya kufikishwa taarifa kwa viongozi wa Serikali walidaiwa kulifika Kitongojini lakini walikataa kwenda kuongea nao km chache kwa madai kuwa ni uongo kwamba hakuna watu waliokusanyana  Akielezea hayo Mwenyekiti huyo alisema tatizo ni uongozi dhaifu kuanzia ngazi ya Kitongoji hadi Wilaya ambapo alidai kuwa ukabila umeshamiri kwa viongozi kujiona kuwa wanahaki ya kutfanya utetezi katika upande mmoja  Kwa upande wake Lairumbe Mollel Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya akizungumzia sakata hilo alimzodoa mwenyekiti huyo wa Kitongonji kuwa ni muongo kwani baada ya wao kufika kabla ya tukio alikataa kuwataja wahusika  Hata hivyo kauli hiyo ilionekana kutokuwa na mashiko baada ya mwenyekiti huyo wa Kitongoji kuonyesha udhaifu wa viongozi hao akisema baada tu ya kufika hawakuweza hata kukubali kupelekwa walikoweka kambi vijana hao wa kimasai  “Baada ya kufika walitaka nisema majina ya walioleta fujo na nilipowataka twende eneo la tukio wakakata nakuona kuwa hawakuwa na njia njema kisha wakarejea Kiteto ambapo usiku vijana hao wakatekeleza azima yao ya kuchinja mtu mmoja na kumpiga mwingine risasi kisha kuwajeruhi watu saba”alisema Mwenyekiti huyo wa kitongoji  Waliofariki katika uvamizi huo ni pamoja na Juma Malagwa (49) ambaye alichinjwa shingo, Yohana Ivo (33) ambaye alipigwa sehemu mbalimbali za mwili na kusababisha kifo pamoja na watu wengine saba kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa kujeruhiwa kwa fimbo na mapanga  Waliolazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto ni Hoti Daniel (38) Emanuel matias (21) Juma Bahati (13) Mwajuma Hamisi (20) Habiba Ally (16) Mwajuma Martin pamoja na Musa Juma (16) aliyepelekwa Dodoma kwaajili ya matibabu  Hata hivyo mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara Elaston Mbwillo akiwa katika kitongoji hicho aliwapa siku 30 viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuweka utaratibu wa kuwatambua wananchi hao ili kuondoa tofauti zao waweze kufanya kazi bila bughdha  “Ninyi wananchi mwende kujisajili Kijijijini ili Serikali iwatambue kwani maisha bora kwa wananchi yatapatikana kwa kufahamika mlipo ili mpatiwe huduma za jamiiambazo kwa sasa hamna hata moja,” alisema Mbwill  
Na Wavuti

MCHUNGAJI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI HUKO RORYA...!SOMA ZAIDI HAPA...

MCHUNGAJI wa Kanisa la Apostolic lililoko mji mdogo wa Shirati wilayani Rorya, Mkoa wa Mara, ameuawa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kwa kupigwa risasi usiku wa kuamkia jana. Hata hivyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Justus Kamugisha licha ya kukiri kutokea kwa tukio hilo, alisema polisi wanaendelea na uchunguzi.
Habari zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio, zinasema mchungaji huyo, Owiti Ariri aliuawa muda mfupi baada ya kukabidhiwa sanduku la fedha za kikundi chao cha kuweka na kukopa alichokuwa akikifanyia kama mweka hazina. Habari zilizothibitishwa na mchungaji mwenzake, Christopher Nyaitega, zinasema tukio hilo lilitokea juzi katika moja ya hoteli iliyoko katika mji huo.Mchungaji Nyaitega ambaye hata hivyo hakuweza kujua kiasi cha fedha kilichokuwemo ndani ya sanduku hilo kwa kuwa yeye siyo mmoja wa wanakikundi, alisema wanakikundi waliamua kumkabidhi fedha hizo ili azipeleke benki kesho yake.
Alisema akiwa nyumbani kwake, alifikiwa na mmoja

wa wanakikundi wenzake aliyeanza kudadisi kuhusu fedha hizo, ambapo marehemu alimhakikishia kuwa ziko salama hali iliyomfanya mgeni wake huyo aondoke.

Alisema muda mfupi baada ya mgeni huyo kuondoka, ghafla majambazi walifika nyumbani hapo na kumtaka marehemu awape fedha hizo kabla ya kumuua.

Alisema jeshi hilo linamshikilia mwanakikundi huyo kwa mahojiano zaidi, huku akiahidi kutoa taarifa zaidi kuhusiana na tukio hilo leo.

Na The choice

Kategori

Kategori