MCHUNGAJI
wa Kanisa la Apostolic lililoko mji mdogo wa Shirati wilayani Rorya,
Mkoa wa Mara, ameuawa na watu wanaosadikiwa kuwa majambazi kwa kupigwa
risasi usiku wa kuamkia jana. Hata hivyo, Kamanda wa Jeshi la Polisi
Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya, Justus Kamugisha licha ya kukiri kutokea
kwa tukio hilo, alisema polisi wanaendelea na uchunguzi.
Habari
zilizopatikana kutoka katika eneo la tukio, zinasema mchungaji huyo,
Owiti Ariri aliuawa muda mfupi baada ya kukabidhiwa sanduku la fedha za
kikundi chao cha kuweka na kukopa alichokuwa akikifanyia kama mweka
hazina.
Habari zilizothibitishwa na mchungaji mwenzake,
Christopher Nyaitega, zinasema tukio hilo lilitokea juzi katika moja ya
hoteli iliyoko katika mji huo.Mchungaji Nyaitega ambaye hata
hivyo hakuweza kujua kiasi cha fedha kilichokuwemo ndani ya sanduku hilo
kwa kuwa yeye siyo mmoja wa wanakikundi, alisema wanakikundi waliamua
kumkabidhi fedha hizo ili azipeleke benki kesho yake.
Alisema akiwa nyumbani kwake, alifikiwa na mmoja
wa
wanakikundi wenzake aliyeanza kudadisi kuhusu fedha hizo, ambapo
marehemu alimhakikishia kuwa ziko salama hali iliyomfanya mgeni wake
huyo aondoke.
Alisema muda mfupi baada ya mgeni huyo kuondoka,
ghafla majambazi walifika nyumbani hapo na kumtaka marehemu awape fedha
hizo kabla ya kumuua.
Alisema jeshi hilo linamshikilia
mwanakikundi huyo kwa mahojiano zaidi, huku akiahidi kutoa taarifa zaidi
kuhusiana na tukio hilo leo.
Na The choice
Subscribe to:
Post Comments (Atom)