Showing posts with label 2017 at 12:27PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:27PM. Show all posts
Hali ya Mchezaji wa Simba Jonas Mkude Baada ya Kupata Ajali iliyoua Shabiki wa Simba

Hali ya Mchezaji wa Simba Jonas Mkude Baada ya Kupata Ajali iliyoua Shabiki wa Simba

Nahodha wa Simba, Jonas Mkude anaendelea vizuri katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam ambako amefanyiwa vipimo na kupata matibabu kwa ujumla.
Mkude alikuwa kati ya watu sita waliopata ajali iliyotokea jana na shabiki mmoja wa Simba, Shose Fidelis amepoteza maisha.
Ajali hiyo ilitokea siku moja tu baada ya Mkude kuingoza Simba kubeba ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma.
Kiungo huyo alifikishwa Muhimbili kwa matibabu zaidi ili kupata uhakika.
Lakini hali yake inaonekana kuimarika na imeelezwa jana alikuwa akilalama sana maumivu lakini sasa ana nafuu.
“Anaendelea vizuri, labda tuangalie kidogo kujua zaidi,” alisema mmoja wa viongozi wa Simba.

from Blogger http://ift.tt/2sddcUy
via IFTTT


wana FA. – East Coast Team Haitarudi Tena .!!!

wana FA. – East Coast Team Haitarudi Tena .!!!

Msanii wa ‘HipHop’ Bongo Mwana FA amefunguka na kusema kundi la East Coast Team halitaweza kurudi tena katika mambo ya muziki tofauti na taarifa za awali za kurejea upya kwa kundi hilo.
FA ameuweka wazi ukweli huo akiwa kwenye kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio kwa kusema itakuwa vigumu kurudisha kundi hilo tena katika ulingo wa muziki lakini wanachoweza kipindi hiki ni kufanya ‘collabo’ ambayo itakuwa inawakutanisha pamoja yeye GK na AY.
“Tulifanya ngoma mbili tatu ila hatukukubaliana kuziachia pia East Coast haiwezi kurudi kwa pamoja lakini mimi, GK na AY tunaweza kufanya kazi kwa pamoja kwani ni jambo rahisi”. Alisema FA
Pamoja na hayo msanii huyo amesema tayari amesharekodi kazi nyingi amezihifadhi maktaba kwake kwa kuwa anaogopa kuzitoa katika kipindi hiki.
Nina kazi nyingi katika maktaba nasubiria ‘timing’ tu niachie maana sasa hivi kuna mambo mengi yanaendelea unaweza ukatoa wimbo hamna mtu anayesikiliza, watu wanaweka bando kufuatilia ubuyu tu, kwahiyo acha patulie kidogo tutaangusha” Alisema FA

from Blogger http://ift.tt/2o48HcM
via IFTTT


JINSI YA KU-UPDATE TECNO C8 KWENDA KATIKA TOLEO JIPYA LA ANDROID MARSHMALLOW

Tecno C8 imekuwa simu ya pili kutoka katika kampuni ya Tecno kupokea toleo jipya la Android Marshmallow na HiOS baada ya ile Boom J8.
Tecno Camon C8, sasa rasmi imeboreshwa kwa Marshmallow ili kuweza ku-update simu yako ya Tecno Camon C8 kuna njia mbili kuu za kutumia, njia ya SD Card na njia ya flashtool. Njia inayoshauriwa na ya rahisi zaidi ni ya SD Card.
Tafadhali soma kwa makini hatua zote, kabla ya kuanza ku-update simu yako, kwani ukikosea unaweza ukaharibu simu yako (Usiwe na shaka ila kuwa makini na fuata hatua zote kama zilivyoelekezwa) . Kama itakushinda, unaweza wasiliana nasi katika sehemu ya maoni au kwa kututumia message katika ukurasa wetu wa Facebook.
NAMNA YA KU-UPGRADE TECNO CAMON C8 KWENDA MARSHMALLOW UKITUMIA NJIA YA SD CARD
1. Download Tcard_update_20160425 kutoka kwenye linki hii, hii ni kutoka katika mtandao wa tecnospot
(Unapaswa kuwa umesajiliwa ili linki hii ifanye kazi, jisajili katika sehemu ya usajili), Faili utakalo-download lina zaidi ya MB800, itakubidi uwe na internet yenye kasi na kifurushi cha kutosha.
2. Ingiza Tcard_update_20160415 kwenye SD Card yako usiingize ndani ya folder lolote, kwa maana nyingine weka katika root.
3.Fanya ‘BACKUP’ ya data zako kisha zima simu yako ya Tecno Camon C8.
4. Shikilia Batani ya kuwashia na Batani ya kuongezea sauti. Hapo nembo (logo) ya ‘startup’ ikitokea, achia Batani moja ya Kuwashia tu. Kisha utaona nembo (logo) ya android kama inavyoonekana hapo chini. Hapo Achia Batani ya kuongezea sauti.
5. Shikilia tena Batani ya Kuwashia kwa sekunde 2, kisha Bonyeza Batani ya Kuongezea sauti.
6. Tumia Batani ya Kupunguzia Sauti kwenda kutumia update kutoka kwenye SD Card kisha CHAGUA kwa kubonyeza Batani ya Kuwashia. Fanya hivyo bila kuachia batani ya kuwashia utaona uso wa simu yako yako kama inavyoonekana hapo chini.
7. Utaingia kwenye sura au uso mpya yaani ”New interface” Kama inavyoonekana hapo chini. Tumia Batani ya kupunguzia sauti kwenda kwenye Tcard_update_20160415 chagua kwa kutumia Batani ya Kuwashia
8. Hapo ‘Installation’ itaanza na ikishakamilika utaona uso ”interfcae’‘ ya simu yako kama inavyoonekana hapo chini. Kisha chagua Reboot system now.
9. Simu itajianzisha yaani itaji-reboot/Restart. Hapo itachukua muda hadi dakika 5 mpaka 10
10. Baada ya kukamilika kwa hatua ya simu kujianzisha yaani ”reboot process”, Fanya marekebisho ya simu yaliyokuwapo awali kutoka kiwandani yaani fanya ‘Factory Reset‘ ili kuhakikisha hupati tatizo lolote.
Pia baada ya hatua ya reboot kukamilika unapaswa uwe na HiOS na Marshmallow 6.0 kwenye simu yako ya Tecno Camon C8.

from Blogger http://ift.tt/2nFkF0K
via IFTTT


Kategori

Kategori