Showing posts with label 2017 at 12:05PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:05PM. Show all posts
CAMEROON WAANGUKIA PUA HUKU WARENO WAKIVUTWA SHATI #CONFCUP

CAMEROON WAANGUKIA PUA HUKU WARENO WAKIVUTWA SHATI #CONFCUP

Michuano ya Confederation Cup imeendelea tena hii leo kwa michezo miwili kupigwa ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya Ureno na Chile na wa pili ukawa kati ya Cameroon na timu ya taifa ya Mexico.
Katila mchezo wa kwanza Ureno walilazumishwa suluhu ya mabao mawili kwa mawili ambapo Ricardo Quaresma alitangulia kuifungia Ureno dakika ya 36 kabla ya Chicharito kusawazisha katika dakika ya 42.
Kipindi cha pili Ureno walionekana huenda wangeweza kuibuka kidedea kwani dakika ya 86 Cedric Soares aliiparia Ureno bao la pili lakini dakika ya 90 Hector Moreno akaswazisha na mchezo ukaisha mbili kwa mbili.
Baada ya hapo kulipigwa mtanange mwingine ambapo wawakilishi wetu Afrika timu ya taifa ya Cameroon waliingia uwanjanj kuikabili timu ya taifa na mabingwa wa Copa America Chile.
Mchezo huu ulionekana kama Cameroon wanaweza kupata hata walau alama moja kwani hadi dakika ya 80 walikuwa hawajaruhusu wavu wa goli lao kuguswa.
Lakini ilipofika dakika ya 82 kiungo wa klabu ya Bayern Munich Artulo Vidal aliwanyanyua kwenye viti mashabiki wa Chile kabla ya Eduardo Vargas kufunga bao la pili na la mwisho katika mchezo huo.
Leo usiku kutakuwa na mchezo mwinhine ambapo mabingwa wa dunia klabu ya Ujerumani watakuwa uwanjani kukipiga dhidi ya Australia.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2srs57r
via IFTTT


Kimenukaa..Polisi Waanza Kamata Kamata kwa Wakazi wa Mabondeni,15 Tayari Wapo Selo..!!!

Watu kumi na tano wamekamatwa na jeshi la polisi kanda maalumu ya Dar es Salamu kwa kosa la kukaidi agizo la serikali lililowataka kuondoka maeneo ya mabondeni.
Kamanda wa polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam Saimon Sirro amesema watu hao wamekamatwa na kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka ya kukaidi kuhama maeneo hatarishi na kwamba eneo hilo ni mali ya halmashauri ya manispaa ya Ilala.
Hata hivyo kamanda Sirro amesema hali ya usalama katika jiji la Dar es Salaam imetengamaa, ambapo jeshi hilo limefanikiwa kudhibiti vikundi vya kihalifu.
Aidha jeshi hilo limefanikiwa kuwakamata wezi wa magari na uchunguzi bado unaendelea.

from Blogger http://ift.tt/2mTu3KM
via IFTTT


Kimenukaaa…Wema Sepetu Mbioni Kukumbwa na Hukumu Kali na Ya Kihistoria…!!!

Upelelezi wa kesi ya kukutwa na bangi inayomkabili Msanii maarufu nchini wa fani ya uigizaji wa filamu, Wema Sepetu (28) na wenzake wawili akiwemo mfanyakazi wake wa ndani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu upo katika hatua za mwisho kukamilika.
Wakili wa Serikali Constantine Kakula ameeleza hayo jana (Jumatano) mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Simba aliuhimiza upande wa mashtaka wajitahidi kuukamilisha na kesi imeahirishwa hadi Aprili 11 ,2017. 
Mbali na Wema wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni mfanyakazi wake wa ndani, Angelina Msigwa (21) na Matrida Seleman Abbas (16) aliyetambuliwa kuwa ni mkulima wote wanatetewa na wakili Hekima Mwesigwa.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://ift.tt/2ms2574
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


from Blogger http://ift.tt/2nHB7cw
via IFTTT


Kategori

Kategori