CAMEROON WAANGUKIA PUA HUKU WARENO WAKIVUTWA SHATI #CONFCUP

Michuano ya Confederation Cup imeendelea tena hii leo kwa michezo miwili kupigwa ambapo mchezo wa kwanza ulikuwa kati ya Ureno na Chile na wa pili ukawa kati ya Cameroon na timu ya taifa ya Mexico.
Katila mchezo wa kwanza Ureno walilazumishwa suluhu ya mabao mawili kwa mawili ambapo Ricardo Quaresma alitangulia kuifungia Ureno dakika ya 36 kabla ya Chicharito kusawazisha katika dakika ya 42.
Kipindi cha pili Ureno walionekana huenda wangeweza kuibuka kidedea kwani dakika ya 86 Cedric Soares aliiparia Ureno bao la pili lakini dakika ya 90 Hector Moreno akaswazisha na mchezo ukaisha mbili kwa mbili.
Baada ya hapo kulipigwa mtanange mwingine ambapo wawakilishi wetu Afrika timu ya taifa ya Cameroon waliingia uwanjanj kuikabili timu ya taifa na mabingwa wa Copa America Chile.
Mchezo huu ulionekana kama Cameroon wanaweza kupata hata walau alama moja kwani hadi dakika ya 80 walikuwa hawajaruhusu wavu wa goli lao kuguswa.
Lakini ilipofika dakika ya 82 kiungo wa klabu ya Bayern Munich Artulo Vidal aliwanyanyua kwenye viti mashabiki wa Chile kabla ya Eduardo Vargas kufunga bao la pili na la mwisho katika mchezo huo.
Leo usiku kutakuwa na mchezo mwinhine ambapo mabingwa wa dunia klabu ya Ujerumani watakuwa uwanjani kukipiga dhidi ya Australia.
 ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2srs57r
via IFTTT