Showing posts with label 2017 at 04:27PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 04:27PM. Show all posts
MADHARA YA KAFEINI (CAFFEINE) NDANI YA MWILI WA BINADAMU

MADHARA YA KAFEINI (CAFFEINE) NDANI YA MWILI WA BINADAMU

Watu wengi huianza siku yao kwa kunywa vinywaji mbalimbali kama chai, soda juisi au maji. Unapovitumia vinywaji hivi mara nyingi huwazi kama vina madhara katika afya.
Reports_Coffee
Vinywaji kama vile soda, kahawa, chai na vile vya kuongeza nguvu huwa vina aina ya Kafeini (Caffeine) ambayo huwa na madhara mengi mwilini pale vinapotumika kwa wingi.
Kwa upande mmoja vinywaji hivi huwa na faida. Utafiti umeonyesha kuwa huchangamsha, kukupa nguvu na kuiweka akili katika hali ya utulivu hasa unapoianza siku.

Vilevile vinywaji hivi kama vile kahawa huwa na madhara pale ambapo vinapotumika kwa muda mrefu na kwa mazoea.

Haya hapa ni baadhi ya madhara yanayoweza kusababishwa na Kafeini

Mfumo wa mmeng’enyo wa chakula

Kafeini huongeza kiwango cha asidi katika tumbo na hupunguza kiwango cha maji mwilini.

Mfumo wa damu na hewa

Kafeini inapoingia katika damu huchukua muda wa saa moja mpaka mbili kufikia maeneo mbalimbali ya mwili, hii itasababisha msukumo wa damu kuongezeka ndani ya muda mfupi. Kwa hivyo kiwango kikubwa cha Kafeini katika mwili kinaweza kupandisha kasi ya mapigo ya moyo na kusababisha matatizo katika mfumo wa hewa.

Mfumo wa uzazi

Kafeini husafiri katika damu na kuifikia ‘placenta’, hivyo kwa mama mjamzito, matumizi ya vinywaji vyenye Kafeini huweza kuathiri mapigo ya moyo ya mtoto aliyeko tumboni. Vilevile Kafeini huweza kuharibu mimba na kuifanya itoke.

Huathiri mifupa na misuli ya mwili

Kafeini inaweza kuvuruga mfumo wa kimetaboliki na ufyonzaji wa wa madini ya calcium ambayo huathiri mifupa na kusinyaa kwa misuli. Pia husababisha kupungua kwa uzito wa mifupa na hii huiweka mifupa ya mwili katika hatari ya kuvunjika kirahisi. Inatambulika kuwa Kafeini husababisha kutolewa kwa madini ya calcium katika mifupa kupitia mfumo wa mkojo.

Mfumo wa figo

Kafeini huzifanya figo kutoa maji mengi nje ya mwili. Hivyo matumizi ya muda mrefu ya vinywaji vyenye Kafeini husababisha kemikali iitwayo ‘oxalates’ ambayo ikiungana na damu hutengeneza ‘calcium oxalates’ ambayo husababisha uwepo wa vijimawe vingi katika figo.

Watu wengi waliojizoesha kutumia kahawa na chai yamkini hawapendelei kusikia madhara ya Kafeini kiafya. ila kupitia ujumbe huu inabidi kupunguza matumizi ya vinywaji hivi mara kwa mara.

Kama umekuwa ukitumia vinywaji vyenye Kafeini kwa muda mrefu na ukaviacha kwa haraka, yawezekana ukapata kizunguzungu, maumivu ya kichwa, uchovu, muwasho na hata kukosa umakini katika kazi.

from Blogger http://ift.tt/2o6sonl
via IFTTT


Jinsi ya kuficha Mafaili na vitu vyako Muhimu ndani ya Calculator kwenye Smartphone yako

Jinsi ya kuficha Mafaili na vitu vyako Muhimu ndani ya Calculator kwenye Smartphone yako

Kama ilivyozoeleka watu wengi tuna video, picha au vitu ambavyo tumeweka kwenye smartphone zetu, ambavyo si vizuri vikaonekana kwa kila mtu. Tatizo la smartphone ni kwamba kila mshikaji utaekutana nae juma au saidi atataka aangalie muundo, uwezo, kamera na toleo lake. Na inakuwa vigumu kuweza kumkatalia mtu hasa kama ni rafiki yako wa karibu sana.
Jinsi ya kuficha Mafaili na vitu vyako Muhimu ndani ya Calculator kwenye Smartphone yako
Ukisema utengeneze folda ambalo linaonekana kwa urahisi halafu uweke picha, video na faili zako za siri lazima watashitukia na kutambua kilichomo ndani. Siku za nyuma , tulikuwa tunatengeneza folda halafu tunaliandika ‘virus’ na kuweka vitu vya siri humo ili kumtisha mtu asiweze kufungua kutokana na jina la folda hilo akizani ni kirusi kweli. Ila siku hizi ujanja huu kila mtu anaujua. Wakati kukiwa na njia nyingi tu za kuweza kuficha vitu vyako vya siri kwenye smartphone yako, leo nitakuonesha namna ya kuficha vitu vyako vya siri katika App unayoitumia kila siku ya Calculator.
Ndiyo, Calculator! kuna app inayoitwa ‘Smart Hide Calculator’ ambayo unaweza ukaitumia kukokotoa mahesabu pia inaweza tumika kuficha vitu vyako vya siri na muhimu kwa watu wadukuzi wa mambo. Smart Hide Calculator ni app ambayo unaweza ukahifadhi picha, video na faili zako muhimu kwa siri kwenye mgongo wa Calculator. Unachotakiwa ni kuweka namba ya siri kisha unabonyeza sawa sawa ‘=’ kisha vitu vyako vitaonekana ndani ya app hiyo.
Fuata hatua zifuatazo kuweza kutumia app hiyo.
Hatua ya 1. Kwanza kabisa, pakua kisha ingiza app ya Smart Hide Calculator kwenye Google Playstore au bonyeza link ifuatayo >> Pakua hapa Smart Hide Calculator
Pakua ‘Smart Hide Calculator’ Playstore
Hatua ya 2. Fungua App yako itakutaka uingize namba ya siri. Hakikisha kuweka namba ya siri ambayo ni ngumu kwa mtu kuweza kuitambua na rahisi kwa wewe kuikumbuka kwa sababu hiyo ndiyo itatumika kufungua na kufungia vitu vyako vya siri ndani ya calculator hiyo.
Ingiza namba ya siri
Hatua ya 3. Baada ya kuhakiki namba ya siri, wewe na mtu yeyote atakayefungua simu yako ataiona app hiyo kama calculator ya kawaida kabisa.
Muonekano wa Calculator hiyo
Hatua ya 4. Ili kuingiza vitu vyako vya siri, unatakiwa kuingiza namba yako ya siri kisha bonyeza kitufe cha sawa sawa ‘=’ ili kufungua vitu vya ndani.
Fungua vitu vyako vya ndani ya app hiyo
Hatua ya 5. Baada ya kufunguka ndani utaona mipangilio ya kuficha mafaili (Hide Files), kuyaondoa mafichoni (Unhide Files), kubadili namba ya siri (Change Password) nakadhalika.
Muonekano wa ndani wa app hiyo
Bonyeza kwenye ‘Hide Files’ kisha chagua mahali ulipo hifadhi vitu vyako kama video, picha, miziki au faili unazotaka kuzificha.
Chagua mahali ulipoweka vitu vyako
Bonyeza ‘OK’ kuficha vitu vyako muhimu ndani ya app inayoaminika duniani, Calculator yako. Kama ukitaka kuyafichua mafaili yako fungua hiyo Calculator kisha chagua ‘Unhide Files’ na faili zako zitakuwa nje ya Calculator hiyo.
Bonyeza kwenye ‘Unhide Files’ kufichua vitu vyako
Kama ukisahau namba ya siri, usijali, unaweza ukairudisha namba yako ya siri kwa kuandika namba hizi 123456789+987654321
Namba ambazo zitakusaidia kama ukisahau namba yako ya siri
App ya Smart Hide Calculator kiufupi ni moja kati ya app nzuri kwa kuficha faili na vitu vyako muhimu kwenye smartphone yako.

from Blogger http://ift.tt/2o6whc9
via IFTTT


Imefichukaa..Hivi Ndivyo Mitandao ya Whatspp na Instagram Inavyoaua Watu Wengi Bila Kujijuaโ€ฆ!!!!

Imefichukaa..Hivi Ndivyo Mitandao ya Whatspp na Instagram Inavyoaua Watu Wengi Bila Kujijua…!!!!

Wanasayansi wamethibitisha kuwa mitandao ya kijamii ndicho chanzo cha magonjwa mbalimbali yakiwamo ya akili na kulemaa kwa mishipa ya shingo.
Wanasayansi wanaeleza kuwa mitandao ya kijamii kama vile facebook, twitter, whatsApp na instagram, ujumbe wa simu na michezo ya kwenye intaneti husababisha magonjwa ya akili, uraibu na kujeruhiwa kwa shingo na uti wa mgongo kunakosababishwa na kuinamia simu muda mrefu.
Tovuti ya Neck Institute (London) imeeleza kuwa madhara ya shingo na uti wa mgongo yanayosababishwa na matumizi ya simu kwa muda mrefu hasa kwa kuandika ujumbe mfupi au Text Neck Syndrome, huathiri mamilioni ya watu duniani.
Daktari bingwa wa neva za fahamu (neurologist) wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Profesa William Matuja amesema bado hakuna ushahidi wa kisayansi kama matumizi ya simu yanaathiri mishipa ya shingo, lakini namna ya matumizi yake yalivyo yanaathiri misuli.
Profesa Matuja amesema kuinamia simu muda mrefu kunasababisha maumivu ya mgongo, shingo na hata kichwa.
Daktari wa mishipa ya fahamu, wa Florida nchini Marekani, Dean Fishman amesema mishipa ya shingo hasa kwa sehemu ya nyuma huathirika kutokana na kuandika ujumbe mfupi kila mara na kwa muda mrefu, kwa sababu kitendo hicho kinamfanya mtumiaji kuiinamia simu.

from Blogger http://ift.tt/2nOrTws
via IFTTT


Kategori

Kategori