Showing posts with label 2017 at 11:19AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:19AM. Show all posts
Huddah Monroe “Nachukia Sana Tendo la Ngono..Najuta Kujiingiza Huko”

Huddah Monroe “Nachukia Sana Tendo la Ngono..Najuta Kujiingiza Huko”

Kila mtu ana mabaya na mazuri yake katika maisha. Mrembo Huddah Monroe ambaye anafahamka sana kwenye mitandao ya kijamii ameonyesha kujutia kuingia katika mahusiano.
Licha ya kuwa na mvuto hasa kwa wanaume, mrembo huyo ameonyesha kuchukia maisha yake ya kimahusiano na anatamani bora asingejiingiza katika tendo la ngono na mtu yeyote kwa sababu wakiachana na mtu huyo huwa anajutia kuingia naye kwenye mahusiano.
Huddah amepost kupitia Snap Chat yake ambayo inaelezea kuwa anajutia kitendo hicho na tena anakereka hasa anapoachana na mtu huo na baadae mtu huyo ambaye anamuoana mbaya kwa wakati huo anakuwa akimfua warudiane.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2u0VFAR
via IFTTT


Mume ajinyonga kwa Ugomvi wake na mke wake

Mume ajinyonga kwa Ugomvi wake na mke wake

Askari wakiwa wamebeba mwili wa marehemu Luhende Lusangija
**
Mwanaume aliyefahamika kwa jina la Luhende Lusangija(34) mkazi mtaa wa Mwinamila Kata ya Ngokolo manispaa ya Shinyanga amekutwa amejinyonga nyumbani kwake kutokana na kile kilichotajwa kuwa mke wake alikuwa anauza mali za familia kutokana na mikopo aliyokuwa anadaiwa.
Tukio hilo limetokea Jumamosi June 3,2017 majira ya saa 11 alfajiri ambapo marehemu akiwa na watoto wake watatu nyumbani, aliamka na kisha kuchukua mtandio huku watoto wake wakiwa wamelala, na kuamua kujitundika kitanzi sebuleni, na kusababisha kifo chake papo hapo.
Mashuhuda wa tukio hilo walisema mwanamme huyo amejiua kutokana na kwa kile kinachodaiwa kuwa na ugomvi wa siku nyingi na mke wake ambaye siku kabla ya tukio alikuwa ameshaukimbia mji wake.
Wakisimuliza tukio hilo majirani zake Safina Javali, alisema marehemu alikuwa na ugomvi na mkewe muda mrefu ambapo walikuwa wakipigana kila siku, kwa kile kinachodaiwa kuwa mwanamke alikuwa akikopa mikopo, na baada ya kushindwa kuirejesha alikuwa akiuza vitu vya ndani wakati mumewe akiwa safarini kwenye majukumu yake ya kikazi.
“Juzi alipokuja mwanaume kutoka safarini akakuta kitanda kimefungwa kwenda kuuzwa, ili mwanamke alipe deni la mikopo aliyokuwa akiichukua, ndipo ugomvi mkubwa ulipozuka hadi kusababisha mwanamke kuukimbia mji wake na kwenda kusiko julikana,”alisema Javali.
Aliongeza kuwa baada ya tukio hilo kutokea walimsikia mtoto wake mkubwa wa miaka 7 majira ya saa moja asubuhi akilia kwa uchungu na kupiga kelele, kuwa baba yake amekufa kwa kujinyonga na walipofika kwenye mji huo na kuchungulia mlangoni ndipo wakamuona amenin’ginia kwenye paa la sebuleni akiwa ameshafariki.
Naye mwenye nyumba Halma Issa ambapo marehemu alikuwa mpangaji wake, alisema mji huo ulikuwa na ugomvi wa mara kwa mara, na walikuwa wakiwasuluhisha lakini ugomvi wao ulikuwa pale pale, na walipopata taarifa ya kifo chake walifika eneo la tukio kasha kuwasiliana na uongozi wa mtaa ilikufuata taratibu za kisheria.
Aidha mwenyekiti wa mtaa huo wa Mwinamila Ngokolo mjini Shinyanga Yohana Munisa, alikiri kupokea taarifa za marehemu huyo majira ya saa moja asubuhi, na alipofika eneo la tukio alimkuta Lusangija akiwa tayari amejinyonga, ndipo akatoa taarifa polisi ambapo nao wakafika ili kuuchukua mwili wa marehemu.
Kwa upande wake Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga Elias Mwita alithibitisha kutokea kwa tukio hilo, na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga, huku ndugu wa marehemu wakitafutwa ili kuuchukua mwili huo kwa taratibu za mazishi.
Na Marco Maduhu-Malunde1 blog

from Blogger http://ift.tt/2qSrmhV
via IFTTT


Fahamu Usiyoyajua Kuhusu Ugonjwa wa Malaria..!!!

Malaria ni nini? Malaria ni ugonjwa wa kuambukizana unaoletwa na chembe chembe zinazoitwa plasmodium.Chembe chembe hizi huingia ndani ya mwili wa binadamu baada ya kuumwa na mbu wa kike kwa jina Anopheles. Mbu mwenye chembe chembe za plasmodium anapomuuma mtu,humuingizia baadhi ya mate yenye viini vya kuambukizana kwenye kidonda hivyo kusabaza Malaria. Viini hivi husafiri hadi kwenye maini ambapo hukaa hadi vifikie ukomavu. Viini hivi baadaye huingia na mtu kama huyu akiumwa na mbu,mbu huyu hubeba chembe chembe hizi na anaweza kumuambukiza mtu atakaye muuma.
Kuna aina 4 za Malaria: P. vivax, P. malariae, P. ovale na P. falciparum. Zimepewa majina kulingana na aina ya plasmodium inayozisababisha. Aina 3 za kwanza sio hatari lakini Falciparumni hatari sana na hata inaweza kusababisha kifo. Hii ni kwa sababu ikishaingia tu mwilini huzaana kwa wingi ndani ya damu.. Hii ni kwa sababu chembe chembe nyekundu za damu(ambazo husambaza oksijeni mwilini)zilizoadhirika huwa nzito na haziwezi kuingia kwenye kapilari. Hii husababisha kufa kwa sehemu ya ubongo,maini,mapafu,figo na matumbo kwa sababu ya ukosefu wa oksijeni. Hali hii inaweza kusababisha kifo kama haita tibiwa haraka.
Malaria hutambulika vipi?
Baridi,kuuma kwa misuli na kichwa zinaweza kuwa dalili za magonjwa mengi mengine. Njia ya pekee unayoweza kudhihirisha kama una Malaria ni kuenda hiospitalini kupimwa damu. Watu wengi wanaotoka sehemu zilizoadhirika na Malaria pindi wanapoona dalili hizi huenda kwenye maduka ya kuuza madawa kununua dawa za kupambana na Malaria. Huu sio ushauri mzuri. Ni muhimu kupimwa damu ili aina ya plasmodium inayosababisha maradhi yako itambulike na upewe matibabu yanayostahili.
Nani yuko kwenye hatari ya kuambukizwa Malaria?
Watoto wachanga,watoto na akina mama waja wazito wako kwenye hatarikubwa ya kushambuliwa hata kufa kutokana na Malaria. Watoto wachanga na watoto wako kwenye hatari kwa sababu wameambukizwa mara chache nahawajajenga 
kinga dhidi ya chembechembe hiziVamizi la Malaria kwa wanawake wajawazito kalikwa sababu kinga yao dhidi ya maradhi huwa chini wakati wa uja uzito. Malaria huongeza tishio kwa mtoto ambaye hajazaliwa kama kuzaliwa kabla ya wakati 
kutimia, uaviaji wa mimba, maambukizi ya sehemu za siri, uzani mdogo wa mtoto anapozaliwa, kupoteza uja uzito na pia ugonjwa huu unaweza kumsababishia mama kifo.
Naweza jilinda vipi dhidi ya Malaria?
Msafiri: Kama unasafiri hadi kwenye eneo linalolotambulika kwa Malaria,mtembelee daktari wako ili akupe dawa mahsusi ya kupambana na Malaria ya eneo unalotembelea.Hakikisha umefuata maelezo vizuri.
Wenyeji wa maeneo yalioadhirika na Malaria: Mbu wa aina ya anopheles hupenda kuuma watu nyakati za macheo na machweo kwa hivyo ni bora kujikinga nyakati hizi.Wakati wa machweo unaweza keti ndani ya nyumba iliyoekewa dawa na usiku unaweza kulala neti iliyotibiwa.
Haribu sehemu mbu wanapozaliana: Kipindi cha mwisho katika ukuaji wa mbu hufanyika majini.Mbu wa aina ya anopheles hupendelea maji yasiyo ya chumvi.Ni muhimu kuharibu ama kunyunyuzia na dawa sehemu zote ambazo mbu wanaweza kutaga mayai.Unafaa kutoa chupa,ndoo ama chochote ambacho kinaweza kusimamisha maji,bacillus thuringiensis(Bti) dawa asili ya kuua wadudu kutoka BioVision inaweza kutumiwa kuua mbu wachanga bila kuharibu maji.
Watoto na mama waja wazito lazima wakingwe na Malaria: Nchini Kenya,wanawake waja wazito wana haki ya kupata matibabu 2 ya bure na neti zilizotibiwa. Chukua moja kutoka katiki kliniki yako.
Neti zilizotibiwa: Kila mtu anapaswa kupata neti iliyotibiwa.Kuna aina mbili ya neti hizi nchini Kenya ambazo zinauwa mbu pindi tu wadudu hawa wanapozigusa.Kuna zile zinazopaswa kutibiwa kila baada ya miezi 6nba PowerTabs na zile zinazodumukwa miaka 3 hadi 5 baada ya kutibiwa
Ni zipi dalili za Malaria?
Dalili za Malaria ni kama zile za Flu; homa, baridi na kuuma kwa misuli na kichwa. Watu wengine hupatwa na kichefuchefu, kutapika na kuharisha. Vipindi vya baridi, homa na kutokwa na jasho hujirudia kila siku moja, mbili au tatu. Watu wenye aina ya P. falciparum wanaweza kupata Malaria ya ubongo ambayo husababisha kuishiwa na fahamu ama kuchanganyikiwa kiakili.
Tiba ya Malaria
Tiba ya Malaria inategemea mambo kadhaa:
Hali ya mgonjwa (mtoto, mama mja mzito, mtu mzima, ni kali ama sio kali)
Nguvu ya dawa dhidi ya ambukizo la viini vya plasmodium.
Eneo la kijiografia ambalo mtu aliambukizwa. Kwa mfano, P.falciparuminayopatikana katika nchi za Mashariki ya kati inaweza kutibiwa na dawa ya chloroquine, lakini inayopatikana Africa, katika nchi zilizo kusini mwa jangwa la Sahara haitibiki kwa chloroquine.
Aina ya plasmodium inayodhuru mgonjwa. Malaria yasiyo makali hutibiwa na dawa za kumeza ilhali wagonjwa wenye P. falciparum kali hulazwa hospitalini na kupewa sindano ya maji.
Kwa bahati mbaya aina fulani za plasmodium zimeleta upinzani dhidi ya dawa ya chloroquine.
TAZAMA HARMORAPA ALIVYO TIMUA MBIO BAADA YA KUIONA BASTOLA

from Blogger http://ift.tt/2og0zXb
via IFTTT


Ruge Afunguka Yote ilivyokuwa Paul Makonda Kuvamia Kituo cha Clouds FM Usiku na Askari…Ataka Aombe Radhi

Stori iliyotrend jana siku nzima kuhusu Mkuu wa Mkoa Paul Makonda Kuvamia kituo cha Polisi na Bunduki usiku wa Ijumaa imedhibitishwa leo na Mkurugenzi wa Kituo hicho Ruge Mutahaba akiongea katika kipindi cha 360
Ruge Mutahaba amefunguka A to Z na Kuelelezea tukio lilivyotokea mpaka Mkuu huyo wa mkoa kuchukua recordings za dada ambaye alirekodiwa na Shilawadu lakini hawakuweza kurusha kwa vile stori haukubalance….
Ruge Amedai Makonda ni Rafiki yake lakini kwa hilo inabidi aombe radhi Watanzania Kwa vile Radio ya Clouds inasikilizwa na watu wengi Tanzania…..

from Blogger http://ift.tt/2mZoVVJ
via IFTTT


Rungwe Amkalia Kooni Makonda Sakata la Vyeti..!!!

Rais wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA), Hashim Rungwe Spunda amemshauri Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujitokeza hadharani na kutoa ufafanuzi juu ya utata wa jina lake unaozidi kuvuma mitandaoni
Utata huo unadaiwa kutokana na mkuu huyo wa mkoa kutumia cheti cha mtu mwingine cha kidato cha nne kujiendeleza kielimu. 
Rungwe ametoa ushauri huo kupitia kipindi cha maswali na majibu cha Kikaangoni , akimsisitiza Makonda kuweka ukweli mezani na kuacha kupiga chenga za mchangani kwa maana akiendelea kukaa kimya watu wanazidi kuamini uvumi huo.
“Namshauri Mkuu wa mkoa ambaye ni kama mwanangu, atoke azungumze ili kumaliza huu utata wa vyeti, asimsumbue Rais ana mambo mengi” Amesema Rungwe
Pia, amemtaka kuacha kulia madhabahuni, kwakuwa hilo halitamsaidia kwa kuwa kulia siyo jibu, na atambue kuwa ofisi hiyo aliyopo sasa siyo yake bali ni wananchi, hivyo kila alichokikuta atakiacha.
“Siku moja nafungua ‘ipad’ yangu namuona Mkuu wa Mkoa analia mbele ya kanisa halafu mchungaji anambembeleza kama mjukuu wangu, mimi namwambia kulia kwake hakusaidii kitu yeye anapaswa kusema ukweli tu kama hilo jina siyo la lake halisi ila ni la kisanii sisi tutamuelewa”. Alisema Rungwe
Kwa upande mwingine, Rungwe ambaye ni wakili msomi, ametoa ushauri wa kisheria kwa watu wenye ushahidi na suala hilo kwenda mahakamani kwa kuwa sheria inaruhusu mashtaka binafsi, ingawa bado Jamhuri itahitajika zaidi kuisimamia kesi hiyo.
Aidha Rungwe aliendelea kufunguka kwa kumtaka Makonda kuacha kung’ang’ania nafasi ambazo anastahili katika nafasi hiyo huku akimpiga kijembe kuwa mwanaume hachagui kazi aende akabebe hata zege kama hana ujuzi wa kufanya.
Kwa upande mwingine Mzee Spunda amemuomba Rais Magufuli kuliingilia kati suala hilo kama alivyofanya kwa maafisa wengine wa serikali.
Rungwe alilazimika kutoa ushauri huo kutokana na swali aliloulizwa kuhusiana na maoni yake kuhusu vita dhidi ya dawa kulevya ambapo amesema kuwa anaunga mkono vita hiyo, isipokuwa njia iliyotumika ya kutaja majina ya watu hadharani bila uhakika, haikuwa nzuri.


DOWNLOAD APPS YA TZTOWN HAPA

http://ift.tt/2ms2574
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE


from Blogger http://ift.tt/2mwdcg2
via IFTTT


Maalim Seif Aagiza Wafuasi Wake Kupambana na Prof Lipumba,Awataka Wasimruhusu Aingize Mguu Wake Zanzibar..!!!

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wafuasi wa chama hicho kulinda ofisi kuu ya Zanzibar dhidi ya uvamizi unaotarajiwa kufanyika.
Akizungumza jana visiwani hapa, Maalim Seif alisema amepata taarifa kuwa Profesa Ibrahim Lipumba na kundi lake wanajiandaa kuvamia makao makuu ya chama hicho Zanzibar.
Alitoa onyo kwa mtu yeyote ambaye atasogea kwenye makao makuu hayo kwa nia ya kufanya fujo, na kuwataka wanachama watiifu wa Zanzibar kuzilinda ofisi hizo.
Aidha, Maalim Seif alimshambulia mwenyekiti anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa, Prof. Lipumba kwa kudai kuwavua madaraka wakurugenzi wa CUF Zanzibar na kuteua wakurugenzi wapya.
Akizungumza na wafuasi wake makao makuu ya CUF yaliopo Mtendeni, Maalim Seif alisema Prof. Lipumba hana mamlaka hayo kwani sio mwanachama tena wa chama hicho.
“Kitendo cha Lipumba kuwafukuza wakurugenzi wa CUF Zanzibar na kuwateua wengine, hana uwezo huo kwa sababu yeye si mwanachama,” alisema Maalim Seif.
“Na hata angekuwa mwenyekiti halali, (bado) hana uwezo huo kwani wakurugenzi huthibitishwa na baraza kuu la taifa.”
“Vijana nawaambieni suala la kulinda ofisi hii ambayo ni makao makuu pamoja na ofisi ya wilaya iliyopo Kilimahewa Zanzibar sio kazi ya walinzi pekee,” alisema Maalim Seif.
“Kila mwanachama azilinde ofisi ili Lipumba na watu wake wasisogee.”
Aidha, kiongozi huyo mkongwe kisiasa alimtaka Lipumba kutoshindana na yeye kwani hawalingani.
Alisema yeye amekuwa na mvuto mkubwa kwa wana CUF na ndiyo maana kila chaguzi amekuwa akipata kura nyingi tofauti na yeye.
Alisema Wazanzibar wana hamu ya serikali ya Zanzibar kuongozwa na CUF hivyo aliwataka wafuasi wa CUF kutowapa nafasi wasaliti wa chama hicho kukivuruga chama.
SALAM ZIMFIKIE
Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi CUF Maalim Seif Sharif Hamad amemlaumu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja kwa kuandaa jeshi lake kupambana naye akiwa katika ziara za kichama katika mkoa huo.
“Salamu zimfikie Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja,” alisema Maalim Seif. “Na aandae tu hayo mabomu na mimi ziara yangu nitafanya.”
“Hakuna wa kunizuia wakati mimi ndiyo katibu mkuu wa CUF ambae nawatembelea wanachama wangu.”
Akizungumza na Nipashe, Kamanda Juma Sadi alimtaka Maalim Seif kupeleka ushahidi wa tuhuma alizotupa dhidi yake.
“Hayo maneno kapewa na nani? Na kama kapewa na wafuasi wake basi wanamdanganya, mimi sijaapa kusema maneno hayo aliyoyadai Maalim Seif dhidi yangu,”alisema Kamanda Sadi.
Kamanda huyo alifafanua kuwa mikutano ya hadhara kwa vyama vya siasa imepigwa marufuku Tanzania nzima, lakini vikao vya ndani hakuna katazo hilo ilimradi havivunji sheria za nchi.
WANANCHI WAOMBA SERIKALI KUODOA TAKA KIZIMBANI MAKAMBAKO MKOANI NJOMBE

from Blogger http://ift.tt/2n900Bm
via IFTTT


Kategori

Kategori