Showing posts with label BRAACKING NEWSSSS. Show all posts
Showing posts with label BRAACKING NEWSSSS. Show all posts

BREAKING NYUZZZZ.....: MH. KASSIM MAJALIWA APITISHWA KUWA WAZIRI MKUU WA TANZANIA


Waziri Mkuu mpya Mh. Kassim Majaliwa.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, muda mfupi uliopita limepitisha jina la Mbunge wa Jimbo la Rwangwa, Mh. Kassim Majaliwa kuwa Waziri Mkuu wa kwanza wa Serikali ya awamu ya tano baada ya jina lake kupelekwa Bungeni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.

Mh. Majaliwa amepitishwa kwa kura 258 sawa na asilimia 73.5% ya kura zote za ndio.

BREACKING NEWSSSSSSS MAJINA MATANO YA WAGOMBEA YATANGAZA SOMA HAPA WALIOPITISHWA WANAWAKE WAWILI WATANGAZWA, MAGUFULI, MEMBE, MAKAMBA, AMINA SALUMU, ASHA ROSE MIGILO

Majina matano yatolewa tayari majira ya saa saba na nusu Nape Nnauye, atangaza live Star TV kutoka Dodoma, yafuatayo ni majina yaliyopita na wanawake wawili.

Taarifa kutoka kamati kuu ya CCM, Kupita StarTv Kuna Bernard Membe, January Makamba, john Magufulu huku wana wake wakiwa wawili, Asha Rose Migiro na Amina Salum Ally,

Leo jumamosi mda wowote majina mitatu yanaweza kutangazwa ni kwa mujibu wa napa Nnauye msemaji wa CCM.

   
Breaking news: Dar (BONGO) Kumechafuka kwa baadhi ya maeneo kutokana na kudi la Panya road

Breaking news: Dar (BONGO) Kumechafuka kwa baadhi ya maeneo kutokana na kudi la Panya road

Baadhi ya maeneo kjatika jiji la dar kumechafuka baada ya kikundi cha Panya Road kuingia mtaani na kupola na kuwateka watu kwa kuwaweka chini ya ulinzi wao na kupola.

Kasha wanaingingia ndani katika nyumba za watu Mwananyamara, na maeneo mengine na katika foreni za baramabani kupora watu walioko katika magali.

Habari zinasema kuwa watu jijini hapo wanahangaika huku na kule kwa kukimbia wakihofia kukutana na kundi hilo linalotumia silaha za jadi.
Ifuatayo ni sauti ya mtangazaji wa Clouds Fm akizungumza katika kipindi chao cha Amplifier  muda si mrefu…BOFYA HAPA……..
Awali ilielezwa kuwa kudi hilo limeingia mtaani kwa lengo la kulipiza kisasi kwa watu walio waua vibaka wawatatu na zimeanza kutokea purukushani hizo majira ya saa  10 baada ya kuwazika nduguzao hao walio uwawa siku ya mkesa wa mwaka mpya.

Kuweni watulivu wanaDar kwani jeshi la ulinzi litawadhibiti watu hao kwani nji wachache kuliko inavyodhaniwa.

More News Update Your Mind, Tutaendelea kukujuza 

Chanzo Clouds Fm Dar na kuandikwa na Elimtaa Media



AJALI MBAYA YATOKEA MBALIZI MAGARI ZAIDI YA MATANO YAGONGWA.




 Magari yakiwa yamegongwa Mbalizi Mbeya

Watu mbalimbali wakiwa wanashangaa ajali hiyo iliyosababisha Gari moja kugonga magari mengine zaidi ya matano
Mashuhuda wakiwa wanashuhudia ajali hiyo


Watu wakiwa wanaongezeka kushuhudia ajali hiyo





PICHA NA MBEYA YETU BLOG
Ajali yaua 13 wakiwemo watatu wa Familia moja Singida

Ajali yaua 13 wakiwemo watatu wa Familia moja Singida

WADAU TUNAOMBA RADHI KAMA KUNA PICHA ITAKUKWAZA KUFUATIA AJALI HII ILIYOTOKEA LEO MKOANI SINGIDA.
DSC05846
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP Geofrey Kamwela, akitoa taarifa ya ajali ya Noah T.730 BUX kuongwa na Lori aina ya Scania T.687 AXB katika barabara kuu ya Singida- Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi.Abiria 13 waliokuwa kwenye Noah wamefariki dunia na watatu wamepata majeraha madogo madogo.Ajali hiyo imetokea leo.(Picha na Gasper Andrew).
IMG-20140120-WA0000
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoa wa Singida, wakitoa miili ya abiria wa Noah T.730 BUX waliofariki baada ya gari hilo kugongwa na lori aina ya Scania T.687 AXB kwenye barabara kuu ya Singida – Dodoma leo. Noah hiyo ilikuwa ikitoea Itigi wilayani Manyoni akienda Singida mjini.(Picha na Nathaniel Limu).
IMG-20140120-WA0001
IMG-20140120-WA0002

Pichani juu na chini ni Baadhi ya miili ya abiria wa Noah T,730 BUX waliofariki leo kwenye ajali iliyotokea eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi baada ya kugongwa na lori T.687 AXB.(Picha na Nathaniel Limu).
DSC05836
DSC05822 Gari aina ya Noah T,730 BUX linavyoonekana baada ya kugongwa na Lori.
DSC05820
DSC05824
ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia mkoani Singida leo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK, kugongwa na Lori aina ya Scania.
Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa  1.32 asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida,SACP ,Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni na lilikuwa na safari ya kuja Singida mjini.
Amesema hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu,bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia  maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida
Alitaja waliotambuliwa na makazi yao kwenye mabano kuwa ni Omari Shaban (44) na mke wake Salma Omari  na mtoto wao Nyamumwi Omari (10) wote wakazi wa Itigi mjini.
Kamwela alitaja wengine kuwa ni Haji Mohammed (29) (Msisi),Mtunku Rashidi (68) (Sajaranda),Salehe Hamisi (28) (Sajanranda),Samir Shaban (20) (Puma),Mwaleki Nkuwi (35) (Ikungi),Athumani Kalemba (38) na Ramadhan Mkenga (Sajaranda).Katika ajali hiyo,abiria watatu walinusurika na kupata majeraha madogo madogo.
Amefafanua juu ya ajali hiyo,Kamanda huyo alisema kuwa lori aina ya scania T.687 AXB wakati likipishana na noah,lilihama upande wake na kuifuata noah ambayo ilikuwa upande wake wa kushoto,na kuligonga na kisha kuliburuza kati zaidi ya 15.
“Kwa sasa bado hatujajua chanzo cha ajali hiyo mbaya ingawa baadhi ya watu wanadai kuwa huenda dereva wa lori alisisia na kusababisha lori hilo kuhama upande wake na kufuata noah.Uchuguzi utakapokamilika,tutatoa taarifa hiyo”,amesema.
Wakati huo huo,mganga mfawidhi wa hospitali ya mkoa mjini Singida,Dk.Banuba Deogratius amekiri kupokea miili ya abiria hao 13 na kusema kati yao,watoto ni wawili.

TRENI YA GONGWA NA LORI MBEYA

Baadhi ya mashuhuda wa ajali iliyo husisha gari mbili na Trani wakitoa  gali ndogo chini ya uvungu wa roli


Lori liliopata ajali maeneo ya Iyunga sehemu palipokuwa kiwanda cha Zana za Kilimo reli inapo katisha. 








Askali wa usalama barabarani akiwa eneo la tukio














USIKU wa leo majira ya saa 1 usiku katika maeneo ya Ituta Iyunga Lori limegonga Tren iliyo kuwa ikuwa ikitoka Zambia kuelekea Dar es Salaam na kusababisha Gari moja ndogo kuingia chini ya roli hilo.

Elimtaa imefika eneo la tukio na kushuhudia roli hilo likiwa limeharibika mbele na kuhama barabarani katika maeneo ya Ituta karibu na kilipo kuwa kiwanda cha zana za Kilimo ambapo Reli inakatika barabara kuu ya Mbeya – Tunduma.

Mashuhuda wameiambia elimtaa kuwa gali hiyo yenye namba za usajili T 961 BTE ilikuwa inatoka Tunduma na kuelekea Dar es salaam.


Tukio hilo limesababisha kuwapo kwa gali ndogo kuingia chini ya roli hilo ambao limegonga treni.

Mashuhuda wameongeza kuwa gari dogo hyo ilikuwa ikitoka Mbalizi kuingia jijini Mbeya na ilikuwa na namba za usajili T 494 AQF.
Endelea kutufuatilia kwa hab ari zaidi ELIMTAA 'More news Update your news'



Kategori

Kategori