Showing posts with label 2017 at 09:46AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 09:46AM. Show all posts
DAR:MENO YA TEMBO YENYE KILO 376 YAKAMATWA NA SERIKALI

DAR:MENO YA TEMBO YENYE KILO 376 YAKAMATWA NA SERIKALI

Waziri wa Maliasli na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe amesema serikali imefanikiwa kukamata jumla ya meno ya tembo 28 katika ghala moja lililopo Mbezi Beach jijini Dar es salaam, yenye uzito wa takribani kilo 376.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri Maghembe amesema meno hayo yaliyokamatwa tarehe 13 na 14 mwezi wa nane mwaka huu yanaonekana ni ya tembo waliouawa miaka ya nyuma ikikadiriwa kuuawa miaka ya 2013 au 2014 na wahalifu hao kuyaweka majumbani mwao huku wakiendelea kutafuta masoko.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Mghembe akizungumza na waandishi wa habari wakati alipokuwa akiwaonesha jumla ya meno ya tembo 28 yakiwa na takribani kilo 376 yaliyokamatwa kwenye ghala katika eneo la Mbezi Beach hivi karibuni. Jumla ya watuhumiwa wa ujangili wapatao 6 tayari wameshakamatwa akiwemo Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa na Imam wa msikiti wa Huda wa Mbezi Beach, Aboubakar Zuberi Segumi ( Picha na Lusungu Helela- WMU)
Waziri Maghembe amesema tayari hadi hivi sasa watuhumiwa sita wa ujangili wameshakamtwa akiwemo Mohamedi Yahya Mohamed, almaarufu Mpemba, Aboubakar Zuberi Seguni mkazi wa Mbezi Beach ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali za mtaa na imamu wa msikiti wa Huda uliopo Mbezi, Juma Saleh Jebo mkazi wa Manzese jijini Dar es salaam, Hamisi Rashid Omary mkazi wa Mbezi, Amir Bakari Shelukindo Mkazi wa Gairo Morogoro na Ahmed Shabani Bakari mkazi wa Mkuranga.
Wakati akiwataja watuhumiwa hao, Waziri Maghembe alisema vita dhidi ya ujangili ni ngumu kwa vile hata baadhi ya watu wasiotegemewa katika jamii kujihusisha nayo nao wamo, akitolea mfano wa mtuhumiwa, Bakari Zuberi Seguni mkazi wa Mbezi Beach ambaye pia ni mwenyekiti wa serikali za mtaa na imamu wa msikiti wa Huda uliopo Mbezi kuwa yeye ni mfano katika jamii kwa kuwa ni kiongozi wa kiserikali lakini pia ni mtu wa Mungu ambaye ni ngumu kufikiria ni miongoni mwa washirika wa biashara hiyo haramu.
Aliongeza kuwa, Tanzania kupitia Wizara yake inataka kufuta kabisa biashara ya meno ya tembo kama China walivyofanya licha ya kuwa uuzaji wa meno ya tembo kwa sasa mara baada ya kufuta soko la wazi imekuwa ikiendelea kwa njia ya mtandao.
Katika hatua nyingine , Waziri Maghemba alipaza sauti kwa mataifa kama vile Vietnam na Thailand kuacha kujihusisha na biashara hiyo na kuiomba jumuiya ya Kimataifa kuingilia ili tembo waendelee kuwepo kwa faida ya kizazi kijacho na badae na dunia kwa ujumla.
Aidha, Waziri Maghembe amesema Tanzania na Dunia kwa ujumla imepata pigo kubwa baada ya kutokea kwa mauaji ya Mkurugenzi wa Palm Foundation, Wayne Lotter raia wa Afrika Kusini yaliyotokea usiku wa jana Masaki jijini Dar es Salaam kwa kuwa alikuwa mstari wa mbele katika kuisaidia serikali katika vita dhidi ya Ujangili.

from Blogger http://ift.tt/2xhCLXd
via IFTTT


Maajabu..Namba ya Simu ya Ben Saanane (Msaidizi wa Mbowe) Aliyetoweka Yatumika Whats App

Maajabu..Namba ya Simu ya Ben Saanane (Msaidizi wa Mbowe) Aliyetoweka Yatumika Whats App

Wakati hofu ikiwa imetenda baada ya jumla ya miezi minane kupita tangu alipopotea kwenye mazingira ya kutatanisha, matumaini mapya yameanza kuibuka baada ya simu yake kuonekana imetumika kwenye mitandao ya kijamii.
Ben Saanane ambaye alikuwa msaidizi wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alitoweka mwaka jana na kumekuwapo na hisia nyingi kuwa huenda alishafariki dunia kutokana na kuwa, hakuna yeyote anayefahamu alipo kijana huyo aliyekuwa akichipukia katika siasa nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa gazeti la TanzaniaDaima, simu ya Ben jana alitumika majira ya saa tatu asubuhi ambapo ilionekana namba yake ikijitoa kwenye makundi ya WhatsApp. Imeelezwa kuwa namba yake ilijitoa kwenye makundi mengi huku ikiwaacha na mshangao mkubwa wajumbe (members) wa makundi hayo.
Hofu ya kuwa kijana huyo hayupo hai ilichangiwa na jibu alilolitoa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa bungeni ambapo alisema, “familia ya mtajwa (Ben Saanane) aliyetangulia mbele za haki au vinginevyo, uchunguzi wa suala lake utakapokamilika, taarifa rasmi itatolewa.”
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo alipokuwa akijibu swali la Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe Aprili 20 mwaka huu aliyetaka kujua kwanini serikali imekuwa kimya sana kwenye suala la kupotea kwa msaidizi wake.
Namba ya Ben Saanane iliyotoka kwenye makundi ya whatsapp ni 0768078523 ambayo imesajiliwa kwa jina lake na amekuwa akiitumia kabla ya kutoweka.
Makundi ambayo namba hiyo inadaiwa kujitoa ni pamoja na Jukwaa la Siasa, Chadema Tanzania, Friends of Bavicha, Tanzania nchi yetu sote na Bantu Politics Tz Kwanza.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano, Uenezi na Mambo ya Nje wa CHADEMA, John Mrema alisema kuwa tukio hilo limewashtua sana kuona mtu ambaye ametoweka simu yake ikitumika kujitoa kwenye makundi ya whatsapp. Aidha, alihoji Polisi wanachukua hatua gani kujua alipo au simu yake ilipo.
Kwa upande wa familia yake, Erasto Saanane ambaye ni mdogo wake Ben alisema kuwa hawajui kama ni yeye au ni nani anatumia simu hiyo kwani hata kwenye kundi la familia amejitoa.
Ndugu huyo alisema hata rafiki zake Ben walisema kwenye makundi mengine amejiondoa pia, na kuwa Jumatano iliyopita ukurasa wake wa Facebook ulitumika ukimuonyesha yupo Tengeru, Arusha.
Aidha baada ya kuona kaka yake amejitoa kwenye makundi hayo, alitoa taarifa katika kituo cha polisi Tabata, na kuwa uchunguzi wa suala hilo umeanza.

from Blogger http://ift.tt/2qOIbug
via IFTTT


Kategori

Kategori