Showing posts with label 2017 at 10:21AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 10:21AM. Show all posts
Matokeo ya mechi za Ndondo Cup leo Juni 27, 2017

Matokeo ya mechi za Ndondo Cup leo Juni 27, 2017

Misosi FC imekuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza hatua ya 16 bora ya michuano ya Ndondo Cup 2017 baada ya kupata ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Mdandu Investment mechi iliyopigwa uwanja wa Kinesi pale V. Wanyama Street, Shekilango.
Laurent Mugila aliifungia Misosi bao la kwanza dakika ya 17 kipindi cha kwanza kabla ya Fuluzuri kufunga goli la pili dakika ya 40 na matokeo kuwa Misosi 2-0 Mdandu hadi mapumziko.
Maganga akapasia kamba tena dakika ya 63 kipindi cha pili likiwa ni bao la tatu na la ushindi kwa Misosi ambao wanaongoza kundi lao wakiwa na pointi sita baada kushinda mechi zao mbili za kwanza mfululizo huku wakiwa wamebakiza mechi moja ya hatua ya makundi.
Kwenye uwanja wa Mwl. Nyerere, Magomeni, Buguruni wamepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Kibo Kombaini.
Goli pekee katika mchezo huo limefungwa na Twaha Magoha dakika ya 30 kipindi cha kwanza na kudumu hadi dakika ya 90 ya mchezo huo.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2uhg6ZQ
via IFTTT


Endapo Ben Pol Akinikataa, ‘Nitajiua kwa Ajili yake’ – Ebitoke

Endapo Ben Pol Akinikataa, ‘Nitajiua kwa Ajili yake’ – Ebitoke

Aliyesema mahaba niue hakukosea kabisa kwani hii imekuja kujidhihirisha kwa mchekeshaji mrembo Ebitoke ambaye karibia mwezi mmoja sasa anahangaika kuwinda penzi la Ben Pol.
Ebitoke amesema kwa sasa mahaba yake yote yapo kwa Ben Pol na endapo atashindwa kupata penzi lake basi yupo tayari kupoteza uhai wake.
“Hapana Ben Pol hawezi kuacha kuwa na mimi, nitafanya kila njia ili aweze kuwa na mimi ,”amesema Ebitoke huku akisisitiza kuwa yupo tayari hata kujiua kwa ajili ya Ben Pol.
“Hata roho nitaweza kujitoa….ndiyo nitajiua kwa ajili yake.. ndiyo nitajiua kwa ajili yake… sitofanya dhambi kwa kujiua kwa ajili yake,”amesema Ebitoke kwenye mahojiano yake na Times FM.
Hata hivyo mrembo huyo mchekeshaji haswaa amesisitiza kuwa watu wasishangae maamuzi yake ya kujiua endapo atakataliwa na Ben Pol kwani mapenzi ni upofu na yana hisia kali moyoni
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2rBIYLf
via IFTTT


Binti afariki akifanyiwa upasuaji kuongeza makalio!

Binti wa miaka 25 amefariki baada ya upasuaji wa kuongeza makalio kwenda ndivyo sivyo, kwa mujibu wa polisi Ranika Hall kutoka Missouri Marekani amekumbwa na umauti katika kliniki ya mambo ya urembo mjini Miami ambako alikuwa anafanyiwa upasuaji.
Marehemu Ranika Hall enzi za uhai wake.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi Kliniki ambamo mama huyo alikuwa akifanyiwa upasuaji wa kuongeza makalio ilipiga simu kuomba msaada majira ya saa tatu usiku siku ya alhamisi baada ya binti huyo kuonesha dalili za kushindwa kupumua. Hata hivyo dada huyo alifariki dunia saa moja baada ya kufikishwa hospitali.
Mwaka uliopita mwanamke mmoja alifariki katika kliniki hiyo hiyo na akifanyiwa upasuaji kama huu, hii imepelekea idara za polisi kuanzisha uchunguzi.
Makalio makubwa yamekuwa ni mtindo kwa miaka ya karibuni na kuwafanya wanawake wengi kuyatafuta kwa njia mbalimbali zikiwemo njia za kufanyiwa upasuaji na upandikizaji wa nyama.
Ukuaji wa teknolojia na sayansi za kimatibabu kumefanya suala la kukuza matiti na matako kuwa bei nafuu na kwa mara nyingi kufanyika bila kupoteza uhai wa mtu ingawa bado kumekuwa na mazungumzo makubwa juu ya athari zake baadae kwa mtu aliyefanya maboresho ya namna hii katika mwili wake.
Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2nOeFBQ
via IFTTT


Kategori

Kategori