Showing posts with label 2017 at 02:49PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 02:49PM. Show all posts

PAUL Makonda: Nina Imani Roma na Wenzake Watapatikana Kabla ya Jumapili Hii

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda, ameahidi Roma Mkatoliki, Moni pamoja na wengine wawili watapatikana Jumapili hii baada ya wasanii hao kutekwa na watu wasiojulikana Jumatano hii wakiwa Tongwe Record.

Alisema hayo jana akiwa nyumbani kwake Masaki jijini Dar es salaam, muda mchache baada ya kutembelewa na wasanii ambao walimtaka mkuu huyo kuwasaidia kupatikana kwa wasanii hao.
Akiongea na waandishi mbele ya wasanii hao, RC Makonda alisema kila mtanzania ana nafasi ya kumtafuta Roma na wenzake kwa kuwa hakuna anayejua watu hao wako wapi.
“Natoa pole kwa ndugu pamoja na marafiki, hakuna mtu ambaye anaweza kupotelewa na mtu akawa na furaha na bahati mbaya tunahangaika kujua wapi waliko. Nitumie fursa hii kuwaambia wananchi wa mkoa wa Dar es salaam kwamba tunapopotelewa na ndugu zetu katika mazingira ambayo hatuyafahamu sio wakati ya kuyarusha rusha maneno na kufika hatua tunapoteza ushahidi,” alisema RC Makonda.
Alisema tayari ameliagiza jeshi la polisi kufuatia suala hilo kwa ukaribu zaidi ili kupata ufumbuzi mapema huku akiahidi mpaka Jumapili hii watu wao watakuwa wamepatikana.
==>Msikilize hapo chini akiongea

from Blogger http://ift.tt/2npISsh
via IFTTT


WALICHOSEMA POLISI KUHUSU KUTEKWA KWA ROMA MKATOLIKI

WALICHOSEMA POLISI KUHUSU KUTEKWA KWA ROMA MKATOLIKI

Habari za kukamatwa mwanamuziki ROMA Mkatoliki zinaendelea kuchukua sura mpya tangu alipochukuliwa na watu wasiojulikana akiwa katika studio za Tongwe zilizopo Masaki, Dar es Salaam.
Kituo cha Runinga cha Azam TV kimefanya mazungumzo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Suzan Kaganda kuhusu kukamatwa kwa ROMA kama kuna taarifa zozote kutoka kwenye jeshi hilo.
RPC Kaganda amewambia kuwa kwa sasa bado hawana taarifa yoyote na hivyo kuwataka wananchi kutulia wakati wao wakiendelea na uchunguzi na baada ya masaa 48 watatoa taarifa kuhusu hatua waliyofia.
Taarifa hiyo inakuja wakati mke wa ROMA, Nancy akiendelea kuomba vyombo vya usalama na Watanzania kwa ujumla kuungana kumtafuta mumewe ambaye amedai kuwa bado anamuhitaji na hata familia inamtegemea.

from Blogger http://ift.tt/2nKMjov
via IFTTT


Kimenukaa..Gwajima Afunguka Mazito Kanisani Kwake..Adai Ametishiwa Kifo na Hata Maliza Wiki Hii Akiwa Salama..!!!

Kimenukaa..Gwajima Afunguka Mazito Kanisani Kwake..Adai Ametishiwa Kifo na Hata Maliza Wiki Hii Akiwa Salama..!!!

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Josephat Gwajima amesema kuwa ametishiwa kifo na kundi la watu asiowafahamu.
Gwajima amesema hayo alipokuwa akihubiri katika kanisa lake Ubungo, Jijini Dar es Salaam na kudaiwa kuwa vitisho hivyo vilikuja kwa njia ya ujumbe ukimtahadharisha kuwa hatamaliza wiki inayoanza.
Gwajima ni miongoni mwa washukiwa waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

from Blogger http://ift.tt/2osYBXD
via IFTTT


Kategori

Kategori