Showing posts with label 2017 at 12:29PM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 12:29PM. Show all posts
DONALD Trump Aionya Tena Korea Kaskazini….

DONALD Trump Aionya Tena Korea Kaskazini….

Rais wa Marekani Donald Trump kwa mara nyingine ametoa onyo dhidi ya Korea Kaskazini kupitia mtandao wa twitter, akisema kuwa Pyongyang inatafuta matatizo.
Pia aliitaka China ambayo ni mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kujaribu kukabiliana na jirani wake huyo.
Bwana Trump alipendekeza kuwa China itapata makubaliano bora ya kibiashara ikiwa itafanya hivyo, lakini akaongeza kuwa Marekani haitaogopa kutatua tatizo la Korea Kaskazini bila ya Uchina.
Bwana Trump alitoa matamshi kama hayo wiki moja iliyopita lakini tangu wakati huo msukosuko umekuwa mkubwa.
Marekani imetuma meli za kivita kuenda kwa maji ya rasi ya Korea hatua ambayo imeighadhabisha Korea Kaskazini.

from Blogger http://ift.tt/2p70w0M
via IFTTT


Noma Sanaaa..Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Aunga Mkono Jacob Zuma Atolewe Madarkani Haraka Sana..!!!

Noma Sanaaa..Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Aunga Mkono Jacob Zuma Atolewe Madarkani Haraka Sana..!!!

Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki amewataka wabunge wa chama tawala cha ANC kutenda yanayowafaa raia wa nchi hiyo na sio kile kitakachofaidisha chama wakati wa kujadili mswada wa kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma, wiki ijayo.
Wito wa Mbeki huenda ukawakera wanaomuunga mkono Zuma ambao wameapa kuupinga mswada huo vikali bungeni, kulingana na tovuti ya IOL.
Upinzani unadai kuwa Zuma ni fisadi na kwamba alimfuta kazi aliyekuwa Waziri wa Fedha, Pravin Gordhan licha ya kuwa Gordhan aliheshimika sana.
Wadadisi wa mambo wanasema hatua hiyo ya Zuma ilikuwa kwa ajili ya kuchukua usukani katika wizara ya fedha.
Hatahivyo, Zuma anakanusha madai hayo ya ufisadi na kudai kuwa yeye kufanya mabadiliko katika baraza la mawaziri na ni kwa manufaa ya raia.
Kulingana na tovuti hiyo, Mbeki amesema kuwa wabunge wanafaa kuwa sauti ya wananchi na wala sio sauti ya vyama vya kisiasa.
Anasema huu ni wakati wa Afrika Kusini kujua ukweli kuhusu uhusiano wa kikatiba kati ya wananchi na viongozi wao wa kisiasa.

from Blogger http://ift.tt/2p4Vuop
via IFTTT


Mbasha Afichua JPM Alivyomfanyia ya Diamond..!!!

Hii ilikuwa stori lakini haikuandikwa! Mwimbaji wa Nyimbo za Injili Bongo, Emmanuel Mbasha amefichua jambo kwa kueleza kwamba, aliyemmuingiza yeye pamoja na mtalaka wake, Flora Mbasha katika masuala ya siasa, alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli. 
Akizungumza katika mahojiano maalum na Risasi Jumamosi, Mbasha alifunguka kuwa, Rais Magufuli alimpigia simu akiwa studio kama alivyomfanyia staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ hivi karibuni, Clouds TV.
Mbasha alifunguka mambo mengi lakini suala zima la historia yake kisiasa, alisema Rais Magufuli ndiye ilikuwa chachu ya yeye na Flora kujiunga na Chama Tawala, Chama cha Mapinduzi (CCM). “Nakumbuka ilikuwa ni mwaka 2005, nilikuwa na aliyekuwa mke wangu, Flora. Tulienda Clouds FM, wakati huo walikuwa kule Kitega Uchumi, Posta.
Tulikuwa tumeenda kutambulisha wimbo wetu, wakumbuka ulikuwa ni ule Tanzania, sasa baada ya Kipindi cha Gospo Track kuishia, Mtangazaji George Njogopa alinitaka niseme namba ili wadau waweze kutusaidia.
a hivi mbele baada ya kipindi kuisha, sisi tulikuwa tunashuka ghorofani, ghafla nikasikia simu inaiita. “Nikapokea, aliyepiga alijitambulisha kwa jina la John.
Akaniambia kuwa hayupo Dar, ila akirudi atanitafuta ili aweze kunisaidia,” alisema Mbasha.
Mbasha alisema hakuwa na imani kama kweli John atamtafuta tena na hakujua pia alikuwa anataka kumsaidia kivipi, lakini kama zari, baada ya wiki kupita, alipigiwa simu na kuambiwa aende Posta.
“Yaani sikuamini, John akapiga simu, akatuelekeza twende Posta, nikashangaa anatuambia tuingie Wizara ya Ujenzi. Tukaingia, akatuambia tumuambie mlinzi kuwa tunakwenda kwa Waziri Magufuli.
“Moyo wangu ukapiga paah! Nikamuambia Flora, hakuamini. Tukapanda hadi ghorofa ya pili. Tulipofika, tukakaa kwenye foleni kisha tukaingia na kukutana na Waziri John Magufuli,” alisema Mbasha.
Baada ya macho yao kuamini wamekutana na waziri, Mbasha anasema aliwakaribisha chai, wakafanya mazungumzo mafupi na tangu hapo, wakashawishika kujiunga na CCM, wakawa washiriki shughuli mbalimbali za serikali pamoja na za chama hicho tawala.
“Tangu hapo, mheshimiwa alikuwa karibu sana na sisi. Akawa anatushauri njia nzuri za kupita ili tufanikiwe.
“Nakumbuka tulianza na shughuli ya uzinduzi wa Barabara ya Msamvu.
“ Tukaendelea hivyo na ikawa kila unaposikia shughuli ya uzinduzi, na sisi lazima tuwepo. Baadaye akatukutanisha na Rais Benjamin Mkapa, kisha Jakaya Kikwete, sisi tukawa kama watoto wa CCM,”alisema Mbasha.
Mwaka 2014, Mbasha na Flora waliachana baada ya Mbasha kudaiwa kumbaka shemejie kisha wanandoa hao kushutuhumiana vikali.
Mbasha alimtuhumu Flora kuhusika na ‘mpango’mchafu ili aweze kumtia hatiani mumewe, lakini hata hivyo kesi iliunguruma na hatimaye Mbasha aliachiwa huru baada ya upande wa Jamhuri kushindwa kuthibitisha mashtaka

from Blogger http://ift.tt/2mZwZFH
via IFTTT


Rais Magufuli akubali ombi la kuipatia Kenya Madaktari 500

Tanzania imekubali ombi la kuipatia Kenya madaktari 500 watakaoisaidia nchi hiyo kukabiliana na tatizo la uhaba wa madaktari katika vituo vyake vya tiba hasa baada ya kutokea kwa mgomo wa madaktari nchini humo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amekubali kutoa madaktari hao leo tarehe 18 Machi, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam, baada ya kufanya mazungumzo na ujumbe wa viongozi wa Wizara ya Afya ya Kenya uliotumwa na Rais wa nchi hiyo Mhe. Uhuru Kenya.
Kiongozi wa ujumbe huo ambaye ni Waziri wa Afya wa Kenya Mhe. Dkt. Cleopa Mailu amemueleza Mhe. Rais Magufuli kuwa baada ya kutokea mgomo wa madaktari pamoja na uamuzi wa nchi hiyo kugatua madaraka katika sekta ya afya, imebainika kuwa nchi hiyo ina upungufu mkubwa wa madaktari ambao hauwezi kumalizwa kwa kutegemea madaktari wanaosomeshwa nchini humo bali kupata madaktari kutoka nje ya nchi.
Mhe. Jack Ranguma amesema Kenya ipo tayari kuwalipa stahili zote madaktari 500 watakaopatiwa kutoka Tanzania ikiwa ni pamoja na mishahara na nyumba za kuishi.
Nae Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania Mhe. Ummy Mwalimu amesema Wizara yake ipo tayari kutoa madaktari hao haraka iwezekanavyo kwa kuwa Tanzania inao madaktari wengi wazuri ambao wamemaliza masomo yao na hawajapata ajira, na wengine wamemaliza mikataba yao ya kazi na bado wana uwezo wa kufanya kazi.
“Kwa hiyo nitoe wito kwa madaktari wote Tanzania ambao hawapo katika utumishi wa umma, hawapo katika hospitali teule na ambao hawapo katika hospitali za mashirika yasiyo ya kiserikali wanaolipwa na Serikali, waombe nafasi hizi.
Vigezo vikubwa ambavyo tutaviangalia ni kwanza awe amemaliza mafunzo ya vitendo (Internship) na pili awe amesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika, kwa hiyo leo hii tutatoa tangazo na tumefurahi sana kwa sababu tunao madaktari wa kutosha ndani ya nchi na tunaweza kuwapeleka Kenya” amesema Mhe. Ummy Mwalimu.
Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Magufuli amesema Tanzania imekubali ombi hilo kwa kuwa Kenya ni ndugu, jirani na rafiki wa kweli wa Tanzania na amemtaka Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Mhe. Ummy Mwalimu kuharakisha mchakato wa kuwapata madaktari hao ili wawahi kwenda Kenya kutekeleza jukumu hilo.
“Matatizo ya Kenya ni matatizo ya Tanzania, tutawapatia madaktari hao 500 ili wakatoe huduma ya matibabu kwa ndugu zetu waliopo Kenya, na kwa kuwa mmenihakikishia kuwa madaktari wangu mtawalipa mishahara inavyotakiwa, mtawapa nyumba za kuishi, na mtahakikisha wanafanya kazi katika mazingira mazuri na salama mimi sina tatizo na naamini mambo yatakwenda vizuri” amesema Mhe. Rais Magufuli.

from Blogger http://ift.tt/2nChpzF
via IFTTT


Kategori

Kategori