Showing posts with label 2017 at 11:26AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:26AM. Show all posts
Bunge Lashindwa Kutoa Adhabu Kwa Joshua Nassari Kwa Kudharau Mamlaka ya Bunge

Bunge Lashindwa Kutoa Adhabu Kwa Joshua Nassari Kwa Kudharau Mamlaka ya Bunge

Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge imelibebesha Bunge mzigo kuhusu shauri la Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari la kuidharau Mamlaka ya Spika na Bunge baada ya kutopendekeza adhabu kwa mbunge huyo.
Nassari anatuhumiwa kuidharau mamlaka hiyo wakati Bunge lilipokuwa likijadili bajeti ya Wizara ya Maji na Umwagiliaji, Juni Mwaka jana.
Akisoma mapendekezo ya kamati hiyo leo (Jumatano) mbele ya Bunge, Mwenyekiti wa kamati hiyo, George Mkuchika amesema kamati hiyo imemtia hatiani kwa makosa ya kuidharau Mamlaka ya Spika.
“Joshua Nassari aliitika wito wa Kamati bila kuleta usumbufu wa aina yoyote na alipohojiwa na kamati alikiri wazi kosa lake na kuomba radhi kwa Mheshimiwa Spika na Bunge,”amesema.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sUml7X
via IFTTT


CAG Afichua Ufisadi Mkubwa Serikalini..Aeleza Jinsi Misamaha ya Kodi Inavyoitafuna Nchi..!!!

CAG Afichua Ufisadi Mkubwa Serikalini..Aeleza Jinsi Misamaha ya Kodi Inavyoitafuna Nchi..!!!

Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Prof. Mussa Assad, imebaini kuwapo kwa matumizi mabaya ya msamaha wa kodi wa shilingi bilioni 3.46, uliotolewa kwa walengwa wawili walioagiza jumla ya magari 238 mwaka wa fedha wa 2015/16.
Akiwasilisha ripoti ya matokeo ya ukaguzi kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30, 2016 katika mkutano wa saba na kikao cha saba cha Bunge, Prof. Assad amesema, msamaha huo wa kodi ulitolewa, lakini magari hayo yalisajiliwa kwa majina ya watu tofauti na wale waliopewa msamaha.
Hata hivyo, amesema walengwa wote waliopewa msahaa huo walikana kuhusika na magari hayo, hali inayoonyesha bado kuna uhitaji wa kuboresha udhibiti na ufuatiliaji wa masuala ya misamaha ya kodi.
Katika udhibiti wa misahaha ya mafuta yanayoingizwa nchini kwa ajili ya matumizi ya migodi, Prof. Assad amesema katika ukaguzi walioufanya Mei 31, mwaka jana, wamebaini lita za mafuta 4,248,802 yaliyosafirishwa kutoka jijini Dar es salaam kati ya Oktoba 2014 na Disemba 2015 kwa ajili ya matumizi ya mgodi wa Buzwagi, Bulyankulu na Geita, nyaraka za uthibitisho hazikuweza kufika vituo husika na kuonesha mafuta hayo yaliyosamehewa kodi yalitumika tofauti na makusudi.
Pia hiyo imebaini lita 20,791,072 za mafuta yenye msamaha wa kodi wa shilingi bilioni 10.17 kwa ajili ya mgodi wa Buzwagi katika kipindi cha miezi 18 kuanzia Julai 2014 hadi Disemba 2015, yalisafirishwa kwenda kampuni ya M/S Agreeko mkandarasi msaidizi ambaye hakuwa mhusika wa msamaha huo.
Kutokana na matumizi hayo mabaya ya msamaha wa kodi, Prof. Assad ameishauri Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kufanya uchunguzi wa mafuta yote ambayo hayana ushahidi kama yamesafirishwa vituo vya uchimbaji madini na kukusanya kodi inayodaiwa kiasi cha shilingi bilioni 1.599 na kodi ya shilingi bilioni 10.17 iliyosamehewa na kupelekwa kwa wakandarasi wasiohusika na msamaha huo.
Aidha, amesema serikali inatakiwa kuhakikisha usimamizi unaimarishwa juu ya matumizi ya misamaha inayotolewa kwa mujibu wa sheria ili kuepuka hasara kwa serikali kutokana na matumizi mabaya ya misamaha ya kodi.

from Blogger http://ift.tt/2pg2PPp
via IFTTT


Mbowe Azua Jipya..Adai Bajeti ya Serikali Haitekeleziki..Wajiandaa Kuipinga Bungeni

Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema wataipinga bungeni bajeti ya serikali ya mwaka wa fedha wa 2017/18 kwani haina msaada wowote kwa wananchi wa hali ya chini na wanaamini fedha hizo hazitapatikana kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo.
Mbowe amesisitiza mwaka jana wabunge wa kambi ya upinzani walieleza wazi kuwa bajeti ya mwaka huu isingetekelezeka na ndio kilichotokea kwani mpaka sasa asilimia 34 pekee ya pesa zote za maendeleo ndizo zimetolewa.
Tazama video Mtoto amvua kofia Papa Francis

from Blogger http://ift.tt/2ob5zzM
via IFTTT


Sakata la Makonda: Ruge wa Clouds Media Ahojiwa na Polisi…!!!

Vyanzo vya uhakika vinaeleza kwamba asubuhi ya leo kulikuwa na kikao cha wafanyakazi wa Clouds. Kikao hicho kiliitishwa na Mkurugenzi wao wa Vipindi na Uzalishaji bwana Ruge Mutahaba ambaye aliwaeleza wafanyakazi wote juu ya kituo chao kuvamiwa siku ya Ijumaa.
Baada ya hilo na mengine yanayohusu tukio hilo, Ruge alitakiwa kuripoti katika kituo cha Polisi cha Oysterbay. Mpaka sasa Ruge anashikiliwa Polisi hao.
Hofu kubwa imetanda kwa wafanyakazi wa Clouds na sasa mabosi wao wanaonekana kuwa mashakani baada ya kuvuja kwa video ya CCTV inayomuonyesha Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akivamia ofisi hizo za Clouds.

from Blogger http://ift.tt/2mZx9Nq
via IFTTT


Watu Wanataka Chakula na Siyo Ndege โ€“ Rungwe

Watu Wanataka Chakula na Siyo Ndege – Rungwe

Mwenyekiti wa CHAUMMA, Hashim Rungwe Spunda ameishauri serikali kuweka mkazo zaidi katika kuhakikisha watanzania wanapa chakula, badala ya kuwekeza kwenye mambo mengine, ikiwemo ununuzi wa ndege.
Rungwe akiwa katika kipindi cha KIKAANGONI cha EATV, amesema kwa sasa nchini hali ni mbaya, na watanzania wengi wanasumbuliwa na njaa huku maisha yakizi kuwa magumu, na kuikumbusha serikali kuwa ilipaswa kutengeneza vituo vya afya vya kisasa vyenye madawa ya kutosha pamoja na kuhakikisha mahitaji muhimu ya wananchi yanapatikana na siyo kutumia fedha za umma kununulia ndege na ujenzi wa reli za treni za umeme ambazo haziwanufaishi watanzania wa kawaida.
“Mimi sikosoi mambo anayoyafanya Mh. Rais , Pesa za ndege ingekuwa ni mimi ningetengeneza vituo vya afya vya kisasa, madawa yangepatikana kwa wingi lakini pia majiko katika shule ili watoto wanywe uji, Unatengeneza reli unabebaba nini ? umekuwa kuli wa nchi zingine, watu wako hawana chochote cha kusafirisha kwenda kuuza huko Afrika Mashariki” Alisema Rungwe
Amebainisha kuwa ndege zilizonunuliwa na serikali hivi sasa hazipati abiria kwa kuwa watu wana njaa, huku akitolea mfano siku moja aliposafiri katika ndege hiyo “Mimi mwenyewe wala sijasimulia, nilipanda ndege kutoka Dar kwenda Arusha, abiria walikuwa 18 tu, yaani ndege ya abiria 98 lakini inaondoka na abiria 18, mimi mwenyewe nimeshuhudia”
Aidha Rungwe amesema vijana wa taifa wanapaswa kushiriki katika suala la uzalishaji wa chakula na siyo kutelekezwa mitaani kitendo ambacho kinawapelekea ushawishi wa kujiingiza katika matumizi ya uvutaji wa bangi.
Hata hivyo Rungwe amesisitiza kwamba wananchi wana njaa hivyo serikali inawajibu wa kuhakikisha chakula kinakuwepo kingi kwa kuwa hilo ndilo jukumu lake hasa ikizingatiwa kwamba wananchi wanalipa kodi.
“Matatizo makubwa tuliyo nayo sisi nchini ni uongozi tu, anayekusanya kodi ndiye mwenye kupanga pesa itumike vipi. Huwezi ukamwambia mtu akalime wakati hana vifaa atatumia mawe? Arudi kwenye stone age? Vijana wanaingia kwenye madawa kwa kukosa shughuli za kufanya”. Kauli ya Rungwe
Rungwe amesesema yeye angepatiwa nafasi ya kuongoza taifa la Tanzania kipaumbele cha kwanza kutoka kwake kingekuwa ni chakula ili wananchi waone tija ya kuishi kwenye nchi yao.

from Blogger http://ift.tt/2mBjHOT
via IFTTT


Kategori

Kategori