Showing posts with label July 18. Show all posts
Showing posts with label July 18. Show all posts
Watu 4 Wanashikiliwa Na Polisi Mkoani Morogoro Kwa Tuhuma Za Kukutwa Na Dola Bandia Na Gongo Lita 268

Watu 4 Wanashikiliwa Na Polisi Mkoani Morogoro Kwa Tuhuma Za Kukutwa Na Dola Bandia Na Gongo Lita 268

Jeshi la polisi mkoani Morogoro limewakamata watu nane kwa tuhuma za kupatikana na dola bandia za kimarekani 66 ambazo kama zingekuwa halali kila moja
ingekuwa na thamani ya dola mia moja, pombe haramu ya gongo lita 268, simu za magendo, chaja pamoja na betri zake. 
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Urlich Matei amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kwa nyakati tofauti akiwemo mfanyabiashara Haji Athumani
aliyekuwa akitokea Dar es Salaam kuelekea Makambako akiwa na simu 748 za aina mbalimbali, betri 650 za simu na chaja 830 akiwa kazihifadhi kwenye mfuko wa
sandarusi bila kuwa na stakabadhi kuonesha uhalali wa bidhaa hizo. 
Katika tukio jingine jeshi hilo la polisi linamshikilia Mwajuma Said mkazi wa Tungi akiwa na dola bandia 66 za kimarekani ambapo kama zingekuwa halali kila moja
ingekuwa na thamani ya dola 100, mabunda tisa ya makaratasi yaliyotengenezwa mfano wa fedha sambamba na watuhumiwa wengine sita zaidi kwa kutengeneza na
kuuza pombe haramu ya Gongo ambapo lita 268 za pombe hiyo na pikipiki iliyokuwa ikisafirisha vimekamatwa.

from Blogger http://ift.tt/2veUnCW
via IFTTT


sababu ya Watoto wa Nne kufariki dunia ndani ya Gari , Zanzibar

sababu ya Watoto wa Nne kufariki dunia ndani ya Gari , Zanzibar

Watoto wanne wamekutwa ndani ya gari lililokuwa limeegeshwa eneo la Jang’ombe, Mkoa wa Mjini Unguja.Watoto hao wote walio na umri usiozidi miaka miwili na nusu walipotea nyumbani kwao tangu Jumapili asubuhi na hawakuonekana tena hadi jioni walipokutwa kwenye gari hilo jekundu wakiwa wameshafariki dunia.
Related image
Watoto hao ni Haytham Mustafa Abubakar, mwenye umri wa miaka miwili, Muslim Hamza Bakari (2), Dodo Mohamed Malali (miwili na miezi sita) na Munawar Ahmed Khamis (miwili na miezi sita).
Watoto hao, ambao walikuwa wakiishi Jang’ombe mjini Unguja, walizikwa jana makaburi ya Mwanakerekwe.
Maswali yaliyoibuka ni namna gani waliingia ndani ya gari, kama milango ilikuwa wazi au imefungwa na iwapo hakukuwa na mtu yeyote wakati watoto hao wakiingia ndani ya gari hilo.
Kamanda wa polisi wa mkoa, Hassan Nassir Ali alisema watoto hao walikutwa ndani ya gari aina ya Toyota Vitz.

Amina Mohamed Haroun, ambaye ni mzazi wa marehemu Haytham, alikuwa akijiuliza maswali kuhusu vifo hivyo alipohojiwa na Mwananchi.“Sijui vipi wanangu hawa wameingizwa ndani ya gari hiyo na kusababisha kifo chao kwa kuwa si kawaida yao kufanya hivyo,” alisema.

“Tena jambo kubwa linalosikitisha, tulikwenda hadi kwenye gari hilo lakini hatukuwaona mara moja.”Amina pia amepoteza mtoto wa ndugu yake aitwaye Dodo Mohamed Malali katika tukio hilo.
Amina alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kufuatilia kwa undani tukio hilo ili kubaini chanzo cha vifo vya watoto wao.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walisema mpaka sasa hawajabaini chanzo cha watoto hao kuingia katika gari hiyo kwa kuangalia umri wao.
Ahmed Hamisi, ambaye ni mzazi wa Munawar, alisema waliwapata watoto hao saa mbili usiku na kwamba gari hilo limekuwa eneo hilo kwa muda mrefu kwa kuwa mmiliki amesafiri.
Hamis alisema alishirikiana na majirani kuvunja milango ya gari hilo na kufanikiwa kuwatoa watoto hao wakiwa wameshafariki.
Maryam Juma Mohamed, ambaye ni jirani wa familia za watoto hao, alisema awali watoto hao walionekana kiwanjani kwake wakicheza na kuna wakati walikuwa wakipigana.
“Baada ya kuwaona wanapigana kutokana na sababu zao za kitoto tuliwaamulia na ndipo walipoondoka sehemu hiyo na kutafuta sehemu nyingine. Hatukuwa na wasiwasi nao kwa kuwa ni jambo la kawaida wao kuranda mtaani kisha wanarudi nyumbani kwao,” alisema.
Alisema ilichukua kama saa tatu tangu walipoonekana uwanjani kwake kabla ya familia za watoto kuingiwa na wasiwasi.
Alisema walishirikiana kwa pamoja na wazazi wa watoto hao kuwasaka sambamba na kupeleka taarifa vituo vya polisi, bandarini na maeneo mengine kuhusu kupotea kwao.

“Tulihangaika sana hadi usiku lakini tulishindwa kuwaona. Ila ghafla tukiwa tumekaa karibu na eneo linalolazwa gari, tukasikia sauti kama mara tatu hivi inasema ‘watoto wamo ndani ya gari jekundu’. Tulihamanika kusikia sauti hiyo, ijapokuwa tulikuwa na wasiwasi mkubwa na sauti hiyo inayotoka wakati mtoaji hatujamjua nani. Lakini tulikwenda hadi kwenye gari na kuwakuta watoto hao wakiwa wanatokwa na mapovu mdomoni,” alisema.

Sheha wa Shehia ya Jang’ombe, Khamis Ahmada Salum alisema walifanya jitihada ikiwa ni pamoja na kufika eneo la maegesho ya magari, lakini hawakuwaona.
“Inashangaza kusikia watoto hao wameonekana ndani ya gari hilo wakati sisi tuliangalia zaidi ya mara tatu ndani. Ijapokuwa gari lina vioo vyeusi, tuliangalia lakini hatukuwaona. Mimi kusikia wameonakana humo, inanishangaza sana,” alisema sheha huyo.
Akizungumzia hilo, Kamanda Ali alisema kuwa Jeshi la Polisi litafanya mahojiano na wamiliki wa eneo hilo pamoja na mmliki wa gari hilo ambaye kwa sasa inadaiwa kuwa yuko Tanzania Bara.
Daktari wa zamu wa Mnazi Mmoja aliyewapokea watoto hao, Dk Makame Zubeir Chinjo alisema walifikishwa hospitalini hapo wakiwa tayari wameshafariki dunia.
Alisema uchunguzi wa awali umebaini walifariki baada ya kukosa hewa ndani ya gari.

from Blogger http://ift.tt/2tckk4E
via IFTTT


Mganga wa Kienyeji apigwa nyundo miaka 30 jela

Mganga wa Kienyeji apigwa nyundo miaka 30 jela

Moja ya kesi zilizokuwa gumzo janaJuly 17, 2017 katika Mahakama ya wilaya ya Kinondoni ni pamoja na kesi namba 21/2017 ya ubakaji ambayo ilikuwa inamkabili Mganga wa kienyeji Wilson Mkomi mwenye umri wa 30.
Mahakama hiyo imemtia hatiani Mshtakiwa na kumuhukumu kifungo cha miaka 30 jela katika kosa la ubakaji ambalo alilitenda December 29, 2016 maeneo ya Kawe Ukwamani, Kinondoni.
Hukumu hiyo imetolewa na Hakimu wa Mahakama hiyo Joyce Mushi ambapo alisema mshtakiwa ametiwa hatiani kwa kosa la ubakaji hivyo anahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.

from Blogger http://ift.tt/2uvQJHf
via IFTTT


Mume asimulia jinsi mke wake na watoto 4 walivyompa kipigo

Mume asimulia jinsi mke wake na watoto 4 walivyompa kipigo

– Mwanamume mmoja Kiambu amejitokeza kufichua jinsi alitandikwa na mkewe kwa muda mrefu 
– Mwanamume huyo vilevile alifichua jinsi mkewe alivyotengeneza vyeti bandia vya kifo chake na kuuza nyumba yake 
– Kisaha alitoweka na naibu chifu wa eneo hilo aliyemsaidia kumhangaisha mwanamume huyo 
– Alimwacha na watoto wanne, yule mdogo akiwa na miezi tisa Mwanamume mmoja Kiambu amegeuka gumzo mitaani baada ya kujitokeza kufichua jinsi aliyekuwa mkewe alivyompiga mara kadha kabla ya kutoweka na naibu chifu wa eneo hilo. 
Habari Nyingine: Wakenya wamshambulia binti wa gavana wa NASA kwa kujihusisha na “ukahaba” James Njenga alizungumza na Citizen TV kuhusu amsaibu yake na jinsi ameweza kuyashinda na kuishi maisha ya kawaida. 
Njenga hakuwa mtu maskini wala mlevui wakati mkewe waliyezaa pamoja watoto wanne alipomtema baada ya miaka kadha ya kumdhulumu.

from Blogger http://ift.tt/2tCBPe1
via IFTTT


WAZIRI MWINYI: WASIONTAKA KUJIUNGA JKT AJIRA WATAZISIKIA BOMBANI

WAZIRI MWINYI: WASIONTAKA KUJIUNGA JKT AJIRA WATAZISIKIA BOMBANI

Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi amesema vijana ambao watakaidi wito wa kuhudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa Sheria watakuwa wamekaidi amri halali na majina yao yatapelekwa mamlaka za ajira kwa ajili ya hatua dhidi yao.
Kauli hiyo ameitoa wakati JKT ikiendelea na mchakato wa kufufua kambi tano nchini ili kufanikisha uwezeshaji wa vijana wanaomaliza Elimu ya juu ya Sekondari kujiunga na Jeshi hilo kwa kujitolea na kwa mujibu wa Sheria.
Awali, ilikuwa lazima kwa wahitimu wa Elimu ya juu ya sekondari na vyuo kujiunga na mafunzo ya mwaka mmoja wa JKT kabla ya kuendelea na masomo au kuanza ajira, na baadaye muda ukapunguzwa. Lakini sasa, wanaojiunga ni wale wanaoitwa tu.
Waziri Mwinyi alisema uchaguzi wa vijana wanaotakiwa kujiunga na mafunzo hayo unafanyika bila kutumia kigezo chochote zaidi ya kuwa mhitimu wa kidato cha sita.
“Yeyote ambaye jina lake linakuwa kwenye orodha ya wanaotakiwa kuhudhuria mafunzo, ni lazima akahudhurie na asipoenda anakuwa amekiuka amri halali. Majina ya walioteuliwa yalionesha waliohudhuria na waliokaidi tunayapeleka katika mamlaka za ajira,” alisema Dkt. Mwinyi.
Alisema orodha ya vijana ambao wanatakiwa kuhudhuria mafunzo hutolewa kwa awamu ili wote waweze kupata fursa ya kuhudhuria, lakini wakati mwingine hufikia wakati muda wa kujiunga na vyuo ukiwa umeshafika.
“Wale ambao wanakuwa wamechelewa kupata mafunzo kwa sababu muda wa vyuo kufunguliwa unakuwa umefika, hawatachukuliwa hatua na wanatambulika,” alisema Dkt. Mwinyi.
Hivi karibuni wakati wa hafla ya kufunga mafunzo ya JKT kwa vijana wa kujitolea katika kambi ya 838 KJ Maramba wilayani Mkinga, Brigedia Jenerali John Mbungo alisema jeshi hilo linakusudia kufufua kambi tano.
Alizitaja kambi hizo kuwa ni 826 Mpwapwa mkoani Dodoma, 845 Itaka (Songwe), 846 na 847 zilizoko Rukwa na 836 na 839 Makuyuni (Arusha) ambayo imeshaanza kupokea vijana ambao wanaendelea na mafunzo.
Alisema huo ni utekelezaji wa azma ya serikali ya kuwezesha vijana wenye sifa za kujiunga mafunzo ya JKT kwa kujitolea na wahitimu wa kidato cha sita kuhudhuria mafunzo hayo.
HT @ MWANANCHI

from Blogger http://ift.tt/2vygjbJ
via IFTTT


KUBENEA: NDUGAI HATOSHI KUWA SPIKA WA BUNGE

KUBENEA: NDUGAI HATOSHI KUWA SPIKA WA BUNGE

Mbunge wa Ubungo Saed Kubenea amemshukia Spika wa Bunge, Job Ndugai, akimtuhumu kuendelea na tabia ya kuwaonea Wabunge wa vyama vya upinzani hasa chama hicho.
Kubenea amesema Ndugai hatoshi kuendelea kuwa kwenye nafasi hiyo kwa sababu amewahi kupata kashfa ya kumpiga ndugu yake ambaye alikuwa mgombea mwenzake wa nafasi ya ubunge Jimbo la Kongwa. Kubenea alitoa shutuma hizo jana wakati akizungumza na wapiga kura wake katika mkutano wa hadhara kwenye Kata ya Manzese, Wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Alisema Ndugai alifanya tukio hilo wakati wa kinyang’anyiro cha kura za maoni ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015. “Simshangia Ndugai kwa sababu alimchapa ndugu yake, Mgogo mwenzake leo amewafungia wabunge wa upinzani akiwamo Mbunge wa Kawe, Halima Mdee,” alisema Kubenea.
Mbali na hilo, aliwataka vijana na wanawake kuanzisha vikundi vya VICOBA ili kunufaika na mikopo inayotolewa na Serikali na mfuko wa jimbo hilo kwa ajili ya kuendeleza maisha yao na kukuza uchumi. Alisema wananchi wa kata hiyo na wa Jimbo la Ubungo wana fursa ya kunufaika na fedha za mfuko wa jimbo ambazo amekuwa akizitoa katika vikundi mbalimbali ili kuwaletea wananchi wake maendeleo.
Pia aliahidi kutoa fedha kwa ajili ya ukarabati wa kituo cha Polisi cha Manzese ili wananchi wapate ulinzi kutoka kwa Jeshi la Polisi. Diwani wa Kata ya Manzese, Ramadhani Kwangaya, alisema kata hiyo ina vikundi visivyopungua 15 vyenye watu zaidi ya 75 na kila mmoja alipatiwa Sh. 315,000 na zaidi ya Sh. milioni 200 zilitolewa kupitia mfuko wa jimbo.
Alisema shughuli nyingi za miradi ya maendeleo zilichelewa kwa sababu kulikuwa na mgawanyo wa Halmashauri ya Kinondoni na kuwa na Halmashauri mbili ya Ubungo na Kinondoni. “Msishangae kimya kirefu bila kuwa na mradi. Manispaa mpya ya Ubungo ilianza Novemba mwaka jana na shughuli rasmi zilianza Januari mwaka huu. Hivyo tulichelewa kurejea kwenu kuwaeleza kile tulichokusanya na kuanza kutekeleza na ndio sababu ilifanya miradi mingi katika kata yetu kuchelewa,” alisema Kwangaya.

from Blogger http://ift.tt/2uvTmsH
via IFTTT


WAZIRI LUKUVI ATUA TANGA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

WAZIRI LUKUVI ATUA TANGA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi awasili mkoani Tanga kutatua migogoro ya ardhi inayoukabili mkoa huo pamoja na mikoa inayopakana nayo.
Katika ziara hii Waziri Lukuvi leo amekutana na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Martin Shigela na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera ili kutatua migogoro ya mipaka iliopo kati ya Wilaya ya Kiteto Iliyopo Mkoani Manyara na Wilaya ya Kilindi iliyopo mkoani Tanga ikiwa muendeleo zo wa mikutano ya kuutafutia ufumbuzi mgogoro huu ambao umesababisha uvunjifu wa amani.
Waziri Lukuvi anatekeleza agizo la Waziri Mkuu Mhe. Khassim Majaliwa ambae alimuagiza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi kutatua mgogoro huu uliodumu kwa miaka mingi kati ya Wilaya hizo mbili pindi alipofanya ziara yake mkoani Tanga.
Ikumbukwe mnamo tarehe 18 Januari, 2017 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alifanya ziara Wilayani Kilindi katika Kijiji cha Mafisa na kuzungumza na wanachi Kijijini hapo kuhusiana na mgogoro huo na kutoa maagizo kwa viongozi wa kuchaguliwa kuacha kutumia nafasi zao vibaya kuongoza kwa mihemko au ushabiki kwa kuwa kufanya hivyo kunapelekea wananchi kufuata ushabiki na kuvunja sheria zilizopo.
Ili kutekeleza agizo hili wakuu wa mikoa hii miwili wakiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wamekutana ikiwa ni muendelezo wa vikao vya kulitafutia ufumbuzi suala hili.
Aidha, wawakilishi wa wakazi wa kata ya Mnazi wilayani Lushoto na viongozi wa Halmashauri ya Lushoto walimlalamikia Waziri Lukuvi kuhusu mashamba matatu ya Mnazi yaliyotelekezwa na mmiliki wa mashamba hayo ajulikanae kwa jina la Le-Mash Enterprises Limited.
Baada ya Waziri Lukuvi kusikiliza malalamiko hayo, ameahidi kutembelea mashamba hayo kesho ili kujionea hali halisi na kuwasikiliza wananchi ambao wanakabiliwa na mgogoro huu ambao umekuwepo kwa miaka mingi.

from Blogger http://ift.tt/2tlO1Ve
via IFTTT


MAPIPA YA SUMU YADAKWA MGODINI HUKO MKOANI MOROGORO

MAPIPA YA SUMU YADAKWA MGODINI HUKO MKOANI MOROGORO

Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limefanya ukaguzi wa kushtukiza katika eneo la mgodi wa Mgalai wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro linalofanya uchenjuaji wa dhahabu na kukamata mapipa 20 yenye kemikali za sumu. Pia, Kampuni hiyo inadaiwa kufanya shughuli zake kinyume na taratibu.
Timu ya wataalamu wa NEMC kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Mvomero walifika kwenye mgodi huo umbali wa kilomita 130 kutoka Makao Makuu ya Wilaya ya Mvoero jana mchana na kushuhudia shughuli mbalimbali zikiendelea katika mgodi huo huku michirizi ya zinazodaiwa kuwa ni kemikali za sumu zikiwa zinachuruzika kuelekea mto uliopo jirani unaotumiwa na wananchi wa Kata ya Pemba na maeneo mengine kwa shughuli za kibinadamu.
Hata hivyo, wahusika wa mgodi huo walikataa kutoa ushirikiano kwa timu hiyo, lakini baada ya askari Polisi waliokuwa wameongozana na wajumbe hao kutishia kutumia nguvu, ndipo waliokuwa mgodini hapo wakaruhusu ukaguzi ufanyike ambapo walibaini makosa kadhaa likiwamo kumilikiwa kwa mapipa zaidi ya 20 yenye kemikali za sumu ambayo ni hatari kwa maisha ya viumbe hai, na rekodi zimeonesha kuwa yalishaingizwa mapipa 83 ya sumu hiyo mgodini humo kwa mujibu wa Meneja wa Ofisi ya Mkemia Mkuu Kanda ya Kati, Mussa Kuzumia.
Wakili Mkuu wa Serikali kutoka NEMC, Bernard Kongolaa amesema kuwa kampuni hiyo inaendesha shughuli zake kinyume na taratibu licha ya kupewa zuio na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Ofisi ya Mazingira Wilaya na Ofisi ya Madini Mkoa, lakini walikiuka na kuendelea na shughuli zao watawachukulia hatua za kisheria, ikiwamo kufikishwa.

from Blogger http://ift.tt/2u4IlgR
via IFTTT


MATONYA KUISHI NCHINI KENYA KWAHUSISHWA NA DAWA ZA KULEVYA

MATONYA KUISHI NCHINI KENYA KWAHUSISHWA NA DAWA ZA KULEVYA

Msanii wa muziki wa kizazi kipya toka jijini Tanga, Matonya amekimbilia nchini Kenya. Matonya yupo nchini humo kwa muda wa miezi mitatu sasa na inasadikiwa kuwa ana mpango wa kuyafanya kuwa makazi yake ya kudumu.
Baada ya kuhamia huko rasmi, Matonya amekuwa msanii wa pili wa Bongofleva baada ya kufuata nyayo za aliyekuwa msanii mkubwa katika miondoko hiyo, Mr. Nice anayesemekana kuishi maeneo ya Thika.
Tovuti ya TUKO.co.ke imeripoti kuwa mwanamuziki huyo amekuwa nchini Kenya kwa miezi mitatu iliyopita na kwamba amesema kuwa anategemea kuifanya nchi hiyo kuwa makazi yake ya kudumu. Akizungumza na Mzazi Willy M. Tuva, Matonya alikataa madai hayo ya kuhamia nchini Kenya ili akwepe mashtaka yanayomkabili ya kuhusika na madawa ya kulevya nchini Tanzania.
“Sijakimbia Tanzania kwa sababu ulizosema,” amesema Matonya, ambaye Wakenya wengi walimtambua na kumpenda kwa ngoma yake ya Vaileti. “Mliona orodha ya waliosadikiwa kujihusisha na madawa ya kulevya. Jina la Matonya halikuwamo kwenye orodha hiyo. Mimi ni mtu safi na haya mengine unayosikia ni maneno tu yanayosemwa kunichafulia jina.”
Matonya alisema haya alipokuwa kwenye mahojiano na kipindi cha Mambo Mseto cha mtangazaji anayejulikana kwa jina maarufu kama Mzazi wa kituo cha redio cha Citizen na kuongeza kuwa bado yupo nchini Kenya kusimamia miradi yake aliyoianzisha.
Matonya, ambaye tangu aachie ngoma yake ya ‘Nyumba Ndogo,’ amekuwa mwanamuziki wa pili toka Tanzania kuhamia nchini Kenya baada ya Mr. Nice wakati muimbaji wa nyimbo za Injili, Rose Muhando anasemekana pia kuwa yupo kwenye mpango wa kuhamia nchini Kenya.

from Blogger http://ift.tt/2u3FD9H
via IFTTT


ROMBO: MCHUNGAJI ASWEKWA LUMANDE BAADA YA WAUMINI ALIOKUWA AKIWABATIZA MTONI KUFARIKI

ROMBO: MCHUNGAJI ASWEKWA LUMANDE BAADA YA WAUMINI ALIOKUWA AKIWABATIZA MTONI KUFARIKI

Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Mchungaji baada ya waumini wake wawili kufa maji alipokuwa akiwafanyia ubatizo kwenye mto Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa msemaji wa Polisi, watu hao walizidiwa na nguvu kubwa ya mkondo wa maji ya mto Ungwasi uliopo wilayani Rombo.
Mpaka sasa bado haijajulikana Mchungaji huyo pamoja na waumini wengine wa Kanisa la Shalom waliokuwa wanaendelea na zoezi hilo walivyookoka. Hawa ni waumini wa Kanisa lililopo wilayani hapo.
Makanisa mengi barani Afrika yanatumia njia hii ya kubatiza waumini mtoni badala ya makanisani kwakuwa kwa kufanya hivyo, ni sawa na ubatizo aliofanyiwa Yesu Kristo katika Mto Jordan.
Shuguli hii ya ubatizo kwa waumini wa madhehebu ya dini ya Kikristo huashiria kufutiwa kwa madhambi na kuanza kwa maisha mapya.

from Blogger http://ift.tt/2uDGYaG
via IFTTT


MAPYA , TRA YAMTOSA NGELEJA NA FEDHA ZA ESCROW

MAPYA , TRA YAMTOSA NGELEJA NA FEDHA ZA ESCROW

Waziri wa Nishati na Madini wa zamani Ngeleja ni mmoja kati ya watu waliopokea mgawo wa fedhazinazodaiwa kuwa zao la kashfa ya Tegeta Escrow, lakini akatangaza kuzirejesha kwa TRA Jumatatu iliyopita.
Februari 2014, Ngeleja ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Sengerema (CCM) aligaiwa Sh. milioni 40.4 na mfanyabiashara maarufu James Rugemalira ambaye mwanzoni mwa mwezi alifikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka 12, yakiwamo ya kughushi na utakatishaji fedha.
Hata hivyo, wakati Ngeleja akithibitisha kwa risiti mbele ya waandishi wa habari kuziingiza fedha hizo katika akaunti ya TRA, mamlaka hiyo imesema haizitambui. TRA imesema haina mpango wowote wa kufuatilia fedha hizo kwa sababu shughuli yake ni kukusanya
kodi.
Akizungumza na Nipashe mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Elimu kwa Umma wa TRA, Richard Kayombo alisema mamlaka hiyo inahusika na kuhakikisha serikali inakusanya kodi stahiki na siyo urejeshaji wa fedha za kashfa kama Escrow.
Kayombo alitoa ufafanuzi huo wakati alipoulizwa na Nipashe juu ya utaratibu rasmi uliopo wa urejeshaji wa fedha hizo endapo wanufaika zaidi wa mgawo wa Rugemalira watataka kufuata nyayo za Ngeleja.
Akifafanua zaidi juu ya suala hilo, Kayombo alisema TRA haihusiki na fedha zilizochotwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kwa kuwa hazikuwa mali yake.
Aidha, Kayombo alisema TRA haiwezi kuzizungumzia fedha hizo kwa kuwa hazijawahi kuwa mali yake na kuelekeza watafutwe wenye fedha hizo kwa ufafanuzi zaidi.
“Fedha za Escrow zinaihusu vipi TRA? Tunawezaje kukaa na kuzungumzia fedha ambazo si zetu?” Alisema Kayombo. “Mimi nashauri watafutwe wenyewe wazungumze kama wanataka kurejesha… siyo sisi.”
Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Tundu Lissu aliiambia Nipashe wiki iliyopita kuwa uamuzi wa Ngeleja kupeleka fedha za hizo TRA unazua maswali zaidi kwa kuwa alipewa na Rugemarila, na viongozi wa awamu ya nne ya serikali walisema siyo za umma bali mtu binafsi.
Lakini akizungumza jijini Jumatatu iliyopita Ngeleja alisema amerejesha mgawo huo kwa TRA kwa kuwa pamoja na sababu nyingine, ili kujiweka kando na kashfa.
Alisema aliyetoa mgawo huo ameshakamatwa na Takukuru na ana kesi inayoendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Huku akionyesha stakabadhi ya malipo ya Benki ya CRDB tawi la Tower, Ngeleja alisema pia “nimeamua kurejesha fedha hizi hata kama aliyenipa msaada bado ni mtuhumiwa, kwa vile hajathibitika kupatikana na hatia, kwa sababu sitaki kuwa sehemu ya kashfa au tuhuma hizo.”
“Nimesononeshwa na kufadhaika sana kuona kuwa msaada niliopewa sasa unahusishwa na tuhuma.” Alisema alipokea mgawo huo Februari 12, 2014 na Januari 15, 2015 alilipa kodi kwa TRA kiasi cha Sh. 13,138,125 ikiwa ni sawa na asilimia 30 ya msaada huo aliopewa.
Hakusema ni kwa nini ulipita muda mrefu kati ya kupokea na malipo ya kodi.
Baada ya Ngeleja kurejesha fedha hizo palikuwa na wito kutoka kwa wanasiasa na wanaharakati waliotaka wote waliopata mgawo huo kurejesha fedha hizo kwa TRA kama alivyofanya waziri huyo wa zamani.
MASHTAKA 12
Rugemalira na mwenzake, mmiliki wa Kampuni ya Pan African Power (PAP), Harbinder Singh Sethi walisomewa mashtaka 12 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Julai 3.
Mashtaka hayo ni pamoja na ya kugushi, utakatishaji fedha na kusababisha hasara ya dola zaMarekani milioni 22.1 na Sh. bilioni 309.4 kwa serikali.
Novemba 26, 2014, Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliwasilisha mjini Dodoma ripoti ya uchunguzi wa kashfa Tegeta Escrow ambapo ilisema Sh. bilioni 306 zilichotwa kutoka Benki Kuu kinyume cha sheria.
Mwenyekiti wa kamati hiyo wakati huo, Zitto Kabwe alisoma ripoti na kulithibitishia Bunge kwamba viongozi na wafanyakazi wa Serikali, wafanyabiashara, viongozi na taasisi za dini, mabenki na watu binafsi walihusika katika ufisadi.
Ripoti ya PAC ilianika orodha ya waliopata mgawo huo kuwa mbali na Ngeleja ni aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Prof. Anna Tibaijuka na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wa zamani, Andrew Chenge ambao kila mmoja alipata Sh. bilioni 1.6.
Wengine ni ofisa katika Ofisi ya Rais wakati huo, Shabani Ngurumo aliyepewa Sh. milioni 80, Jaji wa Mahakama Kuu, Eudes Ruhangisa alipata Sh. milioni 404.25 na aliyekuwa mjumbe wa Bodi ya Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco), Dk. Enos Bukuku, aliyepewa Sh. milioni 161.7.
Katika ripoti hiyo Waziri wa Nishati na Madini wa serikali ya awamu ya tatu, Daniel Yona, Mbunge wa zamani wa Sumbawanga Mjini, Paul Kimiti, aliyekuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji (TIC), Emmanuel Ole Naiko na Jaji wa zamani wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Aloisius Mujulizi walitajwa kupatiwa Sh. milioni 40.4 kila mmoja.
Wengine ni ofisa wa TRA, Lucy Apollo Sh. milioni 80.8, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usajili wa Vizazi na Vifo (Rita), Philip Saliboko Sh. milioni 40.2, maaskofu Methodius Kilaini Sh. milioni 80.9 na Eusebius Nzingirwa Sh. milioni 40.4, Padri Alphonce Twimannye Sh. milioni 40.4, maofisa wa Rita Placidus Luoga Sh. milioni 121.2 na Theophil Rugozobwa Sh. milioni 323.4.
BAJETI WIZARA
Mgawo waliopata wabunge, maofisa wa serikali na viongozi wa dini kutoka kwa Rugemalira unatosha bajeti ya mwaka mzima ya miradi ya maendeleo ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Nipashe imegundua.
Katika miaka mitatu iliyopita ya bajeti (2014/15, 2015/16 na 2016/17), wizara hiyo ambayo kwa sasa iko chini ya Waziri Dk. Harrison Mwakyembe, ilitengewa bajeti ya Sh. bilioni tatu kila mwaka, ikiongoza wizara zote 18 kwa kuwa na bajeti ndogo zaidi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Wakati wizara hiyo ikiambulia Sh. bilioni moja (theluthi ya bajeti yake ya maendeleo) hadi inapofika robo tatu ya mwaka wa bajeti katika miaka hiyo mitatu, imebainika Sh. bilioni 4.77 zinazodaiwa zao la kashfa ya uchotwaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow walizopatiwa waheshimiwa hao zingetosha kugharamia kikamilifu miradi ya maendeleo ya wizara hiyo kwa mwaka mzima na ‘chenji’
ya Sh. bilioni 1.7 ikabaki.
Katika mwaka uliopita wa fedha, kwa mfano, kati ya Sh. bilioni tatu zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya wizara hiyo, ni Sh. bilioni 1.19 tu (asilimia 40) ndizo zilizokuwa zimetolewa hadi Aprili 30, mwaka huu kwa mujibu wa Dk. Mwakyembe.
Chanzo: Nipashe

from Blogger http://ift.tt/2vwVsp4
via IFTTT


Kategori

Kategori