ROMBO: MCHUNGAJI ASWEKWA LUMANDE BAADA YA WAUMINI ALIOKUWA AKIWABATIZA MTONI KUFARIKI

Jeshi la Polisi nchini linamshikilia Mchungaji baada ya waumini wake wawili kufa maji alipokuwa akiwafanyia ubatizo kwenye mto Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro.
Kwa mujibu wa msemaji wa Polisi, watu hao walizidiwa na nguvu kubwa ya mkondo wa maji ya mto Ungwasi uliopo wilayani Rombo.
Mpaka sasa bado haijajulikana Mchungaji huyo pamoja na waumini wengine wa Kanisa la Shalom waliokuwa wanaendelea na zoezi hilo walivyookoka. Hawa ni waumini wa Kanisa lililopo wilayani hapo.
Makanisa mengi barani Afrika yanatumia njia hii ya kubatiza waumini mtoni badala ya makanisani kwakuwa kwa kufanya hivyo, ni sawa na ubatizo aliofanyiwa Yesu Kristo katika Mto Jordan.
Shuguli hii ya ubatizo kwa waumini wa madhehebu ya dini ya Kikristo huashiria kufutiwa kwa madhambi na kuanza kwa maisha mapya.

from Blogger http://ift.tt/2uDGYaG
via IFTTT