WATU wawili wakazi wa Jijini Mbeya wamefariki katika matukio mawili tofati likiwemo la mtu kumfumania binamu yake na mpenzi wake nyumbani kwake katika maeneo ya Inyala jijini hapa.
Kamanda wa Polisi Mkoani Mbeya, Ahmed Msangi alisema, tukio la kwanza lilitokea siku ya mwaka Mpya (Juzi) majira ya saa 10:00 katika maeneo ya Inyala halmashauri ya jiji la Mbeya.
Alisema kuwa katika tukio hilo, Huruma Laiton akufa wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa mkoa wa Mbeya baada ya kupigwa mateke na Mme wake baada ya kufumaniwa akiwa chumbani na binamu wa mmumewe.
Alisema kuwa marehemu afumaniwa na mumewe, Mwakabenga Ezekiel mke wake akiwa ndani na Binadamu yake.
Alisema kuwa mwili wa marehemu umehifadhiwa katika huspitali ya rufaa jijini Mbeya.
Msangi alisema kuwa katika tukio la Pili lilitokea katika maeneo ya Itezi mashariki kata ya Itezi Jijini Mbeya Christopher Myamba, alifariki dunia baada ya kuchomwa kisu shingomi na Ndele baada ya kuzuka ugomvi.
Mgogoro huo ulitokea baada ya marehemu kukutana na kundi la vijana waliwa wa,elewa na kuzuga ugomvi ambao ulisababisha marehemu kuchomwa kisu.
Msangi alisema kuwa mara baada kifo cha marehemu mwili wa marehemu umehifadhiwa katika chuma cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Rufaa Mbeya.
Alisema kuwa kufuatia tukio hilo linamtafuta mtuhumiwa na ametoa wito kwa wakazi wa Jiji la Mbeya kuwa mwenye taarifa atoe taarifa ili kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo.