Kuibuka ghafla kwa ugomvi katika baadhi ya kaunti za Kenya kunatoa
changamoto kwa vyombo vya usalama vya serikali ambavyo tayari
vinapambana na chembechemce za ugaidi ndani ya nchi, maofisa wasema.
Kaunti za Turkana, Pokot Magharibi, Tana River, Mandera, Marsabit na Isiolo, ambazo zimekuwa zikishughudia mapigano ya kudumu ya kikabila, hivi karibuni zilishughudia ongezeko kidogo la vurugu .
Mapigano yanayoendelea baina ya jamii za Turkana na Pokot zimegharimu maisha ya watu zaidi ya 30 kutoka tarehe 18 Novemba wakati mapigano yalipoanza. Mapigano baina ya jamii za Gabra na Borana katika kaunti ya Marsabit yanendelea kupamba moto na yamegharimu maisha ya watu wapatao 12, ikiwa ni pamoja na maofisa polisi, na kuwafanya wengine maelfu kukosa makaazi kutoka Agosti.
Wakati serikali inajaribu kukabili hali hiyo, mizozo inachemka kidogokidogo katika kaunti nyingine zaidi ya kumi inayotarajiwa kuwa tishio la usalama kama masuala yanayosababisha hayatasuluhishwa kwa wakati, Mratibu wa Mkoa wa Magharibi James ole Seriani aliiambia Sabahi.
Seriani ni mjumbe wa Kamati ya Taifa ya Uendeshaji kuhusu Ujengaji Amani na Kukabili Mizozo (NSC) ambayo imekuwa ikipima na kuchambua vyanzo vya mizozo katika taifa lote kwa kipindi cha miezi miwili iliyopita.
Katika matokeo ya awali, kwa mujibu wa Seriani, kamati ilizitaja Nyamira, Kisii, Kiambu, Murang'a, Kwale, Taita-Taveta, Makueni, Meru, Narok, Migori, Kisumu, Vihiga, Kajiado, Machakos, Trans-Nzoia na Nakuru kama kaunti zilizo katika hatari ya kuongezeka kwa vurugu. Kamati itatoa ripoti ya mwisho kuhusu matokeo yake na mapendekezo mapema mwezi Januari, alisema.
Seriani aliiambia Sabahi kwamba migogoro baina ya kaunti ni kuhusu mipaka ya kiutawala na haki ya rasilimali ambayo imeibuka tangu kukabidhi madaraka kulipofanywa na serikali za kaunti zilizoanzishwa ili kuchukua nafasi ya utawala wa majimbo.
Ili kuzuia kuongezeka kwa migogoro, magavana wa kaunti wanapaswa kuunda kamati zenye jukumu la kushughulikia masuala hayo mara kwa mara, Seriani alisema. "Kamati inaweza kuwa maalumu, ya kudumu au vyote viwili. Kaunti hizo zinazokumbwa na mgogoro pia zitenge fedha kwa ajili ya kuleta amani," alisema.
Katika Kaunti ya Mandera, Gavana Ali Ibrahim Roba alisema alikuwa akiwaandaa wataalamu wa kusuluhisha migogoro ili kutatua mapigano ya kila mara ya koo katika kaunti yake.

"Katika kipindi ambacho serikali inapambana na vitisho vya al-Shabaab, migogoro hii ya ndani ni vurugu zisizo na msingi. Cha kushangaza, masuala yaliyo mengi katika mgogoro yanaweza kutatuliwa kupitia maafikiano," Seriani aliiambia Sabahi.
Vurugu baina ya koo zazuia mapambano dhidi ya al-Shabaab
Katibu Mkuu wa Wizara ya mambo ya Ndani na Uratibu ya Serikali ya Taifa Mutea Iringo alisema serikali ya kitaifa ilikuwa inashirikiana kwa karibu na serikali za kaunti ili kumaliza migogoro, lakini katika baadhi ya kaunti, wanasiasa wanachochea vurugu kupitia hotuba zao."Tumewaonya wanasiasa na hata magavana kwamba hakuna aliye juu ya sheria," Iringo aliiambia Sabahi. "Serikali haitasita kuwashitaki wale wanaochochea vurugu."
"Vikosi vyetu vilivyo vingi tumevipa kazi ya kupambana na ugaidi," aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba nchi nzima inapaswa kulenga katika kupambana na adui mkuu wa Kenya, al-Shabaab, sio wenyewe kwa wenyewe.
"Tunapokuwa na migogoro hii ya ndani na baina ya kaunti, tunalazimika kuchepusha vikosi vyetu vya ulinzi," alisema. "Kimsingi, hili linaipa al-Shabaab upenyo wa kupanga shughuli zao za kutisha kwa sababu hatuwafikirii."Mwenyekiti wa Baraza la Magavana Isaac Ruto aliiambia Sabahi kwamba baraza lilikuwa likifanya mipango ya kozi za mafunzo kuhusu usuluhishi wa migogoro na upatanishi kwa magavana wote 47 na manaibu wao.
"Magavana wapo katika makubaliano ya kutafuta au kutoa msaada pale utakapohitajika," alisema Ruto, ambaye ni gavana wa Kaunti ya Bomet.Viongozi katika kaunti ambazo hazina migogoro watashiriki katika mchakato wa amani na sio kuwa kimya wakati wengine wanapopigana na kuuana, alisema.
"Kaunti zenye amani zitapaswa kuingilia kati kaunti ambazo amani yake imetishiwa," alisema. "Hii ni kwa sababu mgogoro uliopo, Garissa kwa njia moja utaziathiri kauni za Bomet au Nairobi."Magavana wanaodhaniwa kutofungamana na upande wowote na wasiokuwa na matakwa fulani na upande wa mgogoro watashirikishwa katika utatuzi wa migogoro katika kaunti nyingine, alisema Ruto. Magavana wa kaunti wanatakiwa kuendeleza uhusiano mzuri na wengine ili kuhakikisha usalamana unatoa fursa za kiuchumi kwa wananchi wao, alisema.
Katika Kaunti ya Mandera, Gavana Ali Ibrahim Roba alisema alikuwa akiwaandaa wataalamu wa kusuluhisha migogoro ili kutatua mapigano ya kila mara ya koo katika kaunti yake.
"Tumekuwa na sehemu yetu ya mapigano ya koo ikiwa ni pamoja na mwaka huu [kati ya Gare na Degodia] ambako watu walipoteza maisha," alisema. "Masuala yanayolimbikizwa, kama malalamiko ya baadhi ya koo kwamba wamekuwa wakiwekwa pembeni katika kazi, yameshughulikiwa."Katika kila kijiji, wazee wa jamii wamekuwa wakifanya kazi ya kubwa katika kutatua migogoro, alisema Roba, lakini kwa kuajiri wataalamu wa usuluhishi wa migogoro wanafanya jitihada za hatua nyingine zaidi.
"Ni mfumo mzuri wa kisheria na tunauamini, na hautavunjwa hata baada ya kuwaajiri maofisa usuluhishi wa migogoro," alisema.Na Sabahioline.com