Showing posts with label Kutoka pembe ya Afrika. Show all posts
Showing posts with label Kutoka pembe ya Afrika. Show all posts
Ngome nyengine ya Al-Shabaab yaanguka

Ngome nyengine ya Al-Shabaab yaanguka

Mwanajeshi wa AU akiweka doria
Mji wa bandari wa Barawe nchini Somalia ambao ulikuwa umetajwa kuwa ngome ya mwisho ya kundi la Al shabaab umethibitiwa na vikosi vya serikali vikisaidiwa na wanajeshi wa muungano wa Afrika.
Mji wa Barawe ulio umbali wa kilomita 200 Kusini Mashariki mwa mji mkuu wa Mogadishu umekuwa chini ya udhibiti wa wanagambo wa Al Shabaab kwa miaka sita.
Muungano wa Afrika unasema kuwa wanamgambo wamekuwa wakiutumia mji huo kama kituo cha kupanga mashambulizi dhidi ya mji mkuu Mogadishu.
Wapiganaji wa Al-Shabaab walianza kuondoka katika mji huo siku chache zilizopita.
Al-Shabaab wapata pigo Somalia

Al-Shabaab wapata pigo Somalia

Wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab
Wanajeshi nchini Somali wameidhibiti milima ya Galgala kutoka kwa wapiganaji wa kundi la Al-Shabaab,kulingana na utawala wa eneo hilo.
Wanamgambo hao walikuwa wakiidhibiti milima hiyo ya Kaskazini mwa taifa hilo kwa miaka kadhaa.
Waziri wa habari wa Puntland amesema kuwa kamanda wa Alshabaab katika eneo hilo alisalimu amri miezi minne iliopita.
Kundi hilo linaloshirikiana na lile la Al-Qaeda lina makao yake makuu kusini na katikati mwa somalia ambapo vikosi vya Umoja wa Afrika vinafanya mashambulizi.
Abdiweli Hirsi Abdille,ambaye ni waziri wa habari wa jimbo la kaskazini mashariki mwa Somalia Puntland amesema kuwa vikosi vya serikali vimeliteka jimbo hilo la Glagala katika mashambulizi yaliotekelezwa alfajiri.
Hatahivyo hakutoa maelezo yoyote kuhusu wafungwa ama waliojeruhiwa.
Lakini kituo cha redio cha Al Furqan,kinachojulikana kwa kuwapendelea wapiganaji wa Al-Shabaab kimeripoti kwamba magari mawili ya kijeshi yaliharibiwa na wanajeshi 16 kuuawa.
Galgala ni eneo la kipekee la Puntland ambalo limekuwa chini ya udhibiti wa Alshabaab.
Kamanda wa Al-Shabaab katika eneo hilo Said Atom alijiunga na vikosi vya serikali mwaka huu na kuwawacha wapiganaji wake katika jimbo la Puntland.
Wapiganaji wa Al-Shabaab wamefurushwa kutoka miji mikuu katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni ,lakini bado wanadhibiti miji midogo katika maeneo ya mashambani.
 Mwandishi wa BBC Ann Waithera afariki

Mwandishi wa BBC Ann Waithera afariki

Marehemu Ann Waithera
Shirika la habari la BBC limempoteza mwandishi wa habari Ann Waithera.
Ann alikuwa anafanya kazi na BBC katika ofisi za Nairobi na amekuwa akiugua Saratani ya Ubongo kwa karibu miaka miwili.
Ann aliwahi kuwa ripota wa BBC mjini Addis Ababa Ethiopia. Mazishi yake yatafanyika siku ya Alhamisi mjini Nairobi.
Kabla ya kujiunga na BBC Ann alifanya kazi na shirika la habari la Nation Media Group nchini Kenya na Citizen TV kama mtangazaji. Ann alikuwa na umri wa miaka 39.
Wandishi wenza wa Ann BBC wameelezea watakavyomkumbuka Ann katika enzi zake alipokuwa anafanya kazi nao.
Razvan Scortea mmoja wa wakuu wa BBC amesema : "Nimeshtushwa sana na kifo cha Ann. Alikuwa mtu mzuri , mwerevu mpenda watu na mwenye matumaini kwa kila jambo. Mungu ambariki.''
Mkuu wa BBC Afrika Solomon Mugera ameelezea kuwa ni jambo la kuhuzunisha sana kumpoteza Ann.
''Nimehuzinika sana. Anne alikuwa mwandishi mahiri . Kila nilipomtembelea nilivutiwa sana na matumaini ya Ann kupona. Hata katika mkesha wa krismasi, nilipozungumza na Ann alikuwa mcheshi sana. Nakumbuka Ann ndiye alikuwa mwandishi wetu wa kwanza mwenye uwezo wa kuripoti katika lugha zaidi ya moja mjini Addis Ababa Ethiopia,'' alisema Solomon
Mkuu wa idhaa ya kiswahili ya BBC Ali Saleh naye pia ameelezea kushtushwa kwake na kifo cha Ann akimkumbuka kama mwandishi mahiri na mwenye kujitolea kwa kazi zake.
'Nakumbuka kufanya naye kazi kabla ya yeye kwenda Addis Ababa, na kufanya mipango ya kila alichotarajiwa kufanya. Matumaini mengi ila yamekatizwa mapema mno.'' alisema Elizabeth Blunt aliyekuwa mwandishi wa BBC mjini Addis Ababa kabla ya Ann kuchukua usukani kutoka kwake.
"Anne alikuwa mmoja wa waandishi mahiri wa BBC nchini Kenya . Kifo kimetupokonya mmoja wa waandishi wenye talanta kuu Afrika Mashariki.'' Kauli ya David Okwemba mhariri mkuu wa ofisi ya BBC Nairobi Kenya.
Mhariri mkuu wa idhaa ya Hausa mjini London Mansur Liman, ametuma rambi rambi kwa familia ya Ann, akiwaombea utulivu wakati huu mgumu
Na BBCSwahili
Kimataifa Asubuhi hii: Serikali yatwaa miji kutoka kwa waasi

Kimataifa Asubuhi hii: Serikali yatwaa miji kutoka kwa waasi


Wiki jana wanajeshi wa serikali walifanikiwa kukomboa miji kadhaa iliyokuwa imetekwa na waasi.
Rais Obama
Jamii ya Kimataifa imeafiki mkataba wa kusitisha mapigano kati ya waasi na serikali ya Sudan Kusini uliosainiwa hiyo jana mjini Addis Ababa Ethiopia.
Marekani imesema, mkataba huo ni sehemu muhimu ya kurejesha amani na utawala wa sheria nchini Sudan Kusini.
Rais Obama ametaja kutiwa sahihi kwa mapatano hayo kama hatua muhimu ya kurejelea amani ya kudumu.
Hata hivyo Marekani imeonya kuwa mzozo huo bado haujatatuliwa na kutoa wito kwa pande zinazozozana kutekeleza mkataba huo mara moja.
''Tunatoa wito wa viongozi wa Sudan Kusini kuheshimu mkataba huo na kuhakisha kuwa mazungumzo zaidi kuhusu jinsi ya kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa hilo yanaendelea'' Alisema msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Mary Harf.
Zaidi ya watu 500,000 wamelazimika kutoroka makwao kutokana na vurugu hizo za mwezi mmoja

Kategori

Kategori