Rais Obama
Marekani imesema, mkataba huo ni sehemu muhimu ya kurejesha amani na utawala wa sheria nchini Sudan Kusini.
Rais Obama ametaja kutiwa sahihi kwa mapatano hayo kama hatua muhimu ya kurejelea amani ya kudumu.
Hata hivyo Marekani imeonya kuwa mzozo huo bado haujatatuliwa na kutoa wito kwa pande zinazozozana kutekeleza mkataba huo mara moja.
''Tunatoa wito wa viongozi wa Sudan Kusini kuheshimu mkataba huo na kuhakisha kuwa mazungumzo zaidi kuhusu jinsi ya kutatua mzozo wa kisiasa unaokumba taifa hilo yanaendelea'' Alisema msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Marekani Mary Harf.
Zaidi ya watu 500,000 wamelazimika kutoroka makwao kutokana na vurugu hizo za mwezi mmoja