Hazem Beblawi
Waziri Mkuu wa Mpito wa Misri
ameambia BBC kuwa wafuasi wa chama cha Muslim Brotherhood wanaweza
kushiriki Uchaguzi Mkuu ikiwa watalaani ghasia na machafuko.
Hazem Beblawi alisema kuwa kura ya maoni ya
mwezi uliopita kuhusu Katiba mpya ilikuwa hatua ya kwanza kurejesha
demokrasia na kuwa itafuatwa na Uchaguzi wa urais na ubunge katika
kipindi cha miezi sita ijayo.Lakini vugu vugu la Muslim Brotherhood, ambalo liliorodheshwa kuwa kundi la kigaidi hivi karibuni, limekanusha madai ya kuhusika na ghasia zinazokumba Misri.
Chama hicho cha Muslim Brotherhood, kiliongoza serikali ya kwanza kuwahi kuchaguziliwa kwa njia ya demokrasia nchini Misri, ambayo iliondolewa madarakani miezi sita iliyopita na jeshi.
Kiongozi wake Mohammed Morsi anakabiliwa na mashtaka kadhaa ya kihalifu.