Duru katika serikali ya Misri zimeeleza kuwa kuna uungwaji mkubwa wa asilimia 90 wa katiba mpya baada ya kura ya maoni.
Zoezi la kuhesabu kura kutokana na kura ya maoni iliyofanyika kwa siku mbili limeanza, lakini inaweza kuchukua siku tatu zaidi matokeo kutangazwa rasmi.
Waandamanaji wachache walijitokeza jana kuliko ilivyokuwa siku ya Jumanne , wakati watu tisa walipouwawa katika mapambano kati ya polisi na wafuasi wa rais aliyeondolewa madarakani Mohammed Mursi.
Mwandishi wa DW nchini Misri Karim el-Kahoury amesema haijulikani iwapo kura hiyo itaaminika.
Kura hiyo ya maoni inaonekana kuwa hatua muhimu kwa mpango wa nchi hiyo kurejesha serikali ya kidemokrasia, lakini wakosoaji wameshutumu madaraka mapya mswada huo wa katiba unaotoa kwa jeshi.
Kundi la Udugu wa Kiislamu lilikuwa kundi pekee kubwa ambapo limekuwa likipinga katiba hiyo. Kundi hilo limepigwa marufuku mwaka jana na kuelezwa kuwa ni kundi la kigaidi.
Na DW.DE