Mataifa ya magharibi na ya Kiarabu yameahidi kutoa dola bilioni 2.4 kwa ajili ya misaada ya kiutu ya Umoja wa mataifa katika mzozo wa Syria.
Ahadi za michango zilitolewa jana nchini Kuwait katika mkutano wa siku moja wa kimataifa, na umefanyika kufuatia tahadhari iliyotolewa na Umoja wa Mataifa kwamba nusu ya Wasyria , zaidi ya milioni tisa wanahitaji msaada wa haraka.
Mkutano huo umefanyika ili kuusaidia Umoja wa Mataifa kufikia lengo lake la misaada kwa Syria linalofikia kiasi cha dola bilioni 6.5, ikiwa ni wito mkubwa wa kuomba msaada kuwahi kutolewa na Umoja wa Mataifa.
Pia mkutano huo umefanyika kabla ya mazungumzo ya amani ya Syria yaliyopangwa kufanyika nchini Uswisi Jumatano wiki ijayo, ambayo kuna matumaini kuwa makundi kutoka upinzani na serikali ya Syria yatahudhuria.
Na DW.DESwahili