Karibu miaka tisa baada ya shambulio la bomu lililosababisha kifo cha waziri mkuu wa zamani wa Lebanon Rafik Hariri (Pichani) pamoja na watu wengine 22, kesi imeanza leo dhidi ya watuhumiwa wanne kutoka kundi la Hezboullah wanaotuhumiwa kupanga njama za mauaji hayo ya kimadhehebu.
Kesi hiyo imeanza kusikilizwa huku ghasia za kimadhehebu zikiendelea nchini Lebanon, ambako bomu lililotegwa katika gari liliripuka mapema leo karibu na mpaka wa nchi hiyo na Syria.
Mtoto wa kiume wa Hariri , kama baba yake, pia waziri mkuu wa zamani , yuko mjini The Hague akihudhuria kikao cha kesi hiyo pamoja na ndugu wengine wa famili za wahanga wa shambulio la Febrauri 14, mwaka 2005.
Lakini watuhumiwa hawako mahakamani kutokana na kundi la Hezbullah kuapa kwamba hawatawakamata watu hao. Jaji David Re amesema waendesha mashtaka watawaita mashahidi kadha katika kesi ambayo huenda ikachukua miezi kadha.