Mazungumzo ya amani ya Syria yaahirishwa

Pande zinazohasimiana nchini Syria hazitakutana tena leo kwa mazungumzo yao ya  amani mjini Geneva, baada ya  kikao cha asubuhi kuvunjika huku utawala wa Rais Bashar al-Assad ukiishutumu Marekani kuwapa silaha waasi.
Baada ya kutangaza kuanza kwa kikao cha leo  msemaji wa Umoja wa mataifa alisema katika taarifa baadae kwamba hakuna mkutano uliopangwa  kufanyika alaasiri. Mwanachama  wa ujumbe wa upinzani Rima Fleihan  aliliambia Shirika la habari AFP kwamba mpatanishi wa Umoja wa mataifa Lakhdar Brahimi ameuahirisha mkutano, kwa sababu utawala wa Syria hautowi ushirikiano katika suala lolote leo, si masuala ya msaada wa kibinaadamu wala utawala wa mpito.
Na Dw.DeSwahili