Umoja wa Mataifa umeamua juu ya washiriki wa mazungumzo juu ya mgogoro wa Syria, lakini uamuzi haujafikiwa juu ya Iran.
Mataifa 31 yamealikwa pamoja na wajumbe wa upande wa upinzani wa Syria, Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya mataifa ya Kiarabu, Umoja wa Ulaya, na Jumuiya ya ushirikiano wa nchi za Kiislamu.
Mazungumzo hayo yamepangwa kufanyika Januari 24, na yataongozwa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon. Umoja wa Mataifa unakadiria kuwa takribani watu laki moja na 26 elfu wameuawa tangu kuanza kwa mgogoro wa Syria mwezi Machi mwaka 2011.
Na DW.DE