Mkosoaji wa ikulu ya Kremlin na tajiri wa mafuta Mikhail Khordovsky amewasili nchini Ujerumani,baada ya kuwachiliwa kutoka gerezani nchini Urusi .
Khordovsky, ambaye aliwahi kuwa mpinzani wa rais Vladmir Putin, amepewa msamaha kufuatia hukumu ya kifungo cha miaka 10 jela, kwa makosa ya udanganyifu wa kodi na wizi.

Gen-Sher alikutana na Khodorvsky wakati alipowasili mjini Berlin, ambako atakutana na familia yake.
Na DW.DE