Kesi ya Mursi kusikilizwa tena Februari 22

Kesi dhidi ya rais wa zamani wa Misri, Mohammed Mursi, na viongozi 21 wa Udugu wa Kiislamu kuhusiana na mashtaka ya kutoroka jela wakati wa mapinduzi ya 2011, imeahirishwa. Mursi na washtakiwa wengine walifikishwa mahakamani leo mjini Cairo, huku rais huyo wa zamani akiwa katika kizuizi kilichojengwa kwa chuma.
Akiwa amevaa mavazi meupe ya mfungwa wa jela Mursi alimkaripia jaji kwa hasira, akimuuuliza niambie wewe ni nani. Jumla ya washtakiwa 129 wanahusika na kesi hiyo. Mbali na wanachama wa Udugu wa kiislamu, wengine ni wapiganaji wa kundi la Wapalestina la Hamas na Hezbollah nchini Lebanon, ambao walikimbia jela wakati wa vuguvugu la siku 18 dhidi ya rais Hosni Mubarak lilipopamba moto 2011