Umoja wa Mataifa unajiandaa
kutoa ombi kubwa zaidi la misaada duniani. Sehemu kubwa ya msaada huu
itawanednea watu wa Syria wanaokumbwa na mgogoro wa kisiasa.
Shirika la chakula duniani linasema kuwa watu milioni saba nchini Syria wanahitaji msaada.Mjumbe wa misaada katika Umoja wa Mataifa Valerie Amos ameambia BBC kuwa mzozo wa kibinadamu unaoendelea kukithiri nchini Syria, ni moja ya mizozo mikubwa zaidi ya kibinadamu kushuhudiwa katika miaka ya hivi karibuni.
Ni mzozo mbaya sana ikilinganishwa na hali ilivyo sasa. Wananchi wanne wa Syria kati ya watano, wana wasiwasi kuwa chakula kinapungua kulingana ripoti hiyo mpya.
Hii ni dalili ya vita vilivyo vibaya nchini Syria na janga la kibinadamu linaloambatana na vita hivyo.
Ombi la leo la msaada zaidi linanuia kuwasidia wananchi wa Syria ambao wana mahitaji zaidi na wengine zaidi ya milioni mbili waliotoroka vita na kuingia katika nchi jirani.
Bi Valeri Amos, amesema kuwa anapokea ujumbe wa kusikitisha sana kutoka kwa wakimbizi wenyewe.
Kampeini ya kuomba msaada kwa niaba ya watu wa Syria miezi kadha ailiyopita, ilikuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa na ilichangisha dola bilioni nne. Mgogoro wa Syria ni mbaya sana sasa hivi ikilinganishwa na miezi kadhaa iliyopita.
Ombi la msaada hii leo linanuia kuwasaida watu milioni tisa ndani ya Syria na wengine milioni mbili waliokimbilia katika nchi jirani nusu yao ikiwa watoto. Bi Amos anasema anatarajia kuwa dunia itaona umuhimu wa kushirikiana katika janga hili linalokabili watu wa Syria.
BBCSwahili