CDU, CSU, SPD kusaini mkataba wa muungano mkuu

Viongozi wa vyama vyenye nguvu zaidi nchini Ujerumani - muungano wa wahafidhina CDU na CSU, na kile cha SPD wanajiandaa kusaini makubaliano ya kuunda serikali hii leo, ambayo yataiwezesha serikali mpya kuanza kazi. 

Kwa pamoja vyama vya CDU/CSU na SPD vina jumla ya asilimia 80 ya viti bungeni, na kuifanya hii kuwa mara ya tatu tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia, kwa Ujerumani kutawaliwa na kile kinachoitwa "muungano mkuu".
Kutokana na serikali kuwa na wingi mkubwa, upo wasiwasi iwapo sauti ya vya vidogo itaweza kusikika katika bunge jipya. 
Viongozi wa vyama hivyo vitatu wanatarajiwa kusaini mkataba wa muungano wenye kurasa 185 majira ya saa saba na nusu saa za hapa Ujerumani. 
Baada ya kusainiwa kwa mktaba huo, Merkel anatarajiwa kuteuliwa tena kuwa Kansela katika kikao cha bunge kesho Jumanne.
Na Dw.de