Maelfu ya watu wameachwa bila makao kutokana na vita hivyo
Waakilishi wa serikali ya Sudan Kusini wanasema kuwa serikali imetia saini mkataba wa kusitisha vita na waasi.
Kulingana na mkataba huo uliotiwa saini mjini Addisa Ababa Ethiopia, mapiganao yanapaswa kusitishwa katika muda wa masaa 24.Aidha mkataba huo unatarajiwa kusitisha vita vya mwezi mmoja vilivyoanza tarehe 15 Disemba mwaka jana kati ya waasi na serikali.
Mazungumzo ya amani yamekuwa yakikumbwa na matatizo kuhusu swala la wafungwa 11 wa kisiasa ambao bwana Riek Machar anayeongoza waasi alitaka waachiliwe kama sharti la kutia saini mkataba wa amani.